Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kampuni ya simu za mkononi ya Apple inatarajia leo hii kuonesha matoleo mapya aina nne ya Iphone 13 ambayo ni iPhone 13 mini, iPhone 13, iPhone 13 Pro na iPhone 13 Pro Max.

Hata hivyo imeelezwa kwamba hakuna matarajio makubwa ya mabadiliko kwenye muonrkano wa simu hizi mpya bali mabadiliko makubwa yanayotarajiwa ni processor yenye spidi zaidi, camera yenye picha nzuri zenye ubora zaidi na betri ambayo inakaa na chaji kwa muda mrefu.

Apple pia iatarajiwa kutambulisha aina mpya ya apple watch ambayo itakua na kioo kikubwa tofauti na sasa, pia inatarajiwa wataonesha aina mpya ya airpods pro, iPad na Macbook.
Screenshot_20210914-165442_Instagram.jpg
 
Mkandarasi wa Serikali anayehusika na utengenezaji wa vifaa vya ulinzi Nchini Israel ametambulisha kifaa kipya cha kijeshi ambacho kinajiendesha chenyewe kwa kutumia teknolojia mpya ambayo inakiwezesha pia kufanya doria, kutoa taarifa, kukabiliana na adui ikiwemo kufyatua risasi papohapo.

Robot hiyo yenye matairi manne imetengenezwa pia kwa nia ya kuepusha vifo vya Wanajeshi na kuwaondolea hatari ya kushambuliwa wawapo kwenye doria hasa mipakani, kifaa hiki kinaongozwa na Binadamu ambae anaweza kukaa umbali mrefu na anaweza kutumia tablet kukiongoza huku kikiwa kimebeba bunduki mbili aina ya machine guns, kikiwa na camera pamoja na sensa.

Wataalamu wanasema teknolojia ya kifaa hiki ni bora zaidi kuliko hata magari mengine ya kivita yaliyotengenezwa kwenye miaka 15 iliyopita ambapo kwa sasa katika kufanya doria kwenye mipaka yake Jeshi la Israel linatumia kifaa kingine kinachojiendesha chenyewe ambacho ni kidogo kuliko hiki kiitwacho Jaguar.
Screenshot_20210914-165733_Instagram.jpg
 
“Sensa ya mwaka 2022 itatusaidia kujua hali ya ongezeko la Watu na hali ya uhamaji na itatusaidia kupima maendeleo yaliyopatikana tangu kufanyika Sensa ya mwisho mwaka 2012, itatuwezesha pia Serikali kuandaa sera na mipango ya maendeleo ya muda mfupi na muda mrefu”

“Sensa ya mwaka 2022, itasaidia kugawa namna ya kupeleka huduma kwa Wananchi kulingana na idadi ya Watu na mahitaji ya Watu kwenye maeneo, bila takwimu huwezi kushughulikia changamoto za ajira, huwezi kujua uwiano wa ugawaji rasilimali”

“Dodoso za Sensa ya mwaka 2022 itakwenda pia kuangalia majengo na anuani za makazi, Sensa zilizopita hatukuwahi kuchukua idadi ya majengo, tutaweza kupiga ndege wawili kwa jiwe moja na kuokoa fedha za Serikali” ———Rais Samia leo Dodoma akizindua mpango wa sensa itakayofanyika Tanzania nzima mwaka 2022.
Screenshot_20210914-165846_Instagram.jpg
 
Hatimaye Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amechanjwa chanjo ya Covid-19 jana baada ya kukataa kuchanjwa chanjo hiyo kwa miezi sita akihofia haikuwa salama, inaaminika amechomwa ya Mordena na ambayo aligoma kuchomwa ni AstraZeneca lakini Maafisa wa Serikali wamekataa kuthibitisha kuwa ni chanjo gani amechanja.

“Chanjo inabaki kuwa suluhisho bora la kupambana na Corona nawaomba wengine wote wakachanjwe” ———Rais Felix

Congo imeripoti maambukizi ya Covid 19 56,000 na vifo 1066 lakini tangu kuanza kutolewa kwa chanjo idadi ya maambukizi na vifo inaripotiwa kupungua, tayari Nchi hiyo imepokea dozi za Mordena za ziada 250,000 na pia imepokea chanjo za Johnson & Johnson, AstraZeneca na Pfizer.
Screenshot_20210914-165954_Instagram.jpg
 
: • Inaelezwa kwamba Nchini Tanzania kuanzia January 2021 hadi August 2021 Watanzania zaidi ya 300 walikuwa wameuwawa na Watanzania wenzao kwa visa mbalimbali ikiwemo ushirikina, migogoro ya mifugo na mazao pamoja na tuhuma za ushirikina ambapo kwenye wivu wa mapenzi idadi ya vifo imeongezeka September hii baada ya Mwanaume kutengeneza juisi yenye sumu na kujiua yeye na Mpenzi wake.

Tukio jingine la September hii ni kutoka Manyara ambako Mwanaume aitwae Samwel Alfred (52) wa Kijiji cha Magara Babati mkoani Manyara anatuhumiwa kumuua Kijana Michael Jackson (25) baada ya kumfumania akifanya mapenzi na Mke wake Habiba Said (22) kwenye zizi la ng'ombe.

Samwel alimkatakata Michael Jackson kwa panga hadi kumuua na kuzitenganisha sehemu mbalimbali za mwili wake ambapo RPC Manyara Merrison Mwakyoma amesema "Habiba alivyojaribu kuzuia pia alikatwa mkono ambao umetenganishwa kabisa"

"Baada ya hapo Samwel alikwenda kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji na kumwambia nenda kule nimemfuma Mke wangu akifanya mapenzi kwenye zizi la ng'ombe, baada ya hapo akaenda kwa Mke wa Marehemu Michael Jackson na kumwambia nenda mumeo nimfuma akifanya mapenzi na Mke wangu" ——— RPC Mwakyoma.
Screenshot_20210914-170144_Instagram.jpg
 
Mkazi wa Mtaa wa Nyahanga Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Steven Felician Samandari (25) ambae alikua Mlinzi wa Kampuni ya Mast Holding ameuwawa kwa kuchomwa kisu tumboni na Mtu ambae bado jina lake halijafahamika ambae aliruka fensi kwenye Guest House na Bar aliyokua akilinda Steven.

Mtuhumiwa huyo anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua kwa kisu Mlinzi huyo aliyekua akimzuia kuingia eneo hilo usiku kumfuata Mpenzi wake ambae ni Muhudumu wa Guest House hiyo.

Kamanda wa Polisi Shinyanga George Kyando amesema Guest House hiyo ambayo ina Bar hapohapo ilikua imeshafungwa usiku huo na Mtuhumiwa alipofika kutaka kuingia aliambiwa arudi kesho yake kwani muda wa kazi umeshaisha ila hakukubalianana hilo.

“Kilichofata ni yeye kuruka fensi na kuingia, Mlinzi alipomuona akamkamata ili kumtoa nje lakini kumbe alikua na kisu, akamchoma Mlinzi huyo ambae alifia palepale kutokana na kutokwa na damu nyingi, Mtuhumiwa amekimbia lakini tunamshikilia Muhudumu na hadi sasa amegoma kumtaja Mtuhumiwa" ——— RPC Kyando.
Screenshot_20210914-170300_Instagram.jpg
 
Serikali ya Ujerumani na Tanzania wametia saini mkataba wa Sh68 bilioni kwa ajili ya kuimarisha miradi ya uhifadhi katika Hifadhi za Taifa nchini.

Mkataba huo umelenga miradi mikubwa miwili ambayo ni mfumo wa ikolojia wa Katavi na Mahale wenye thamani ya Sh46 bilioni na mradi wenye thamani ya Sh22 bilioni wa maendeleo ya uhifadhi katika mfumo wa Ikolojia ya Serengeti.

Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania.
Screenshot_20210914-170534_Instagram.jpg
 
Young Boys v Man United saa 1:45
Sevilla v Salzburg saa 1:45
FC Dynamo Kiev v Benfica saa 4:00
Barcelona v Bayern saa 4:00
Villarreal v Atalanta saa 4:00
Lille v Wolfsburg saa 4:00
Malmö v Juventus saa 4:00
Chelsea v FC Zenit saa 4:00
Screenshot_20210914-170640_Instagram.jpg
 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka viongozi wa Serikali kuanzia ngazi za vitongoji, vijiji, kata na Wilaya kuhakikisha wanaunda kamati za maridhiano kwa ajili ya kusuluhisha migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikijitokeza katika baadhi ya maeneo na kuleta madhara kwa jamii.

Ulega alitoa agizo hilo kwenye ziara aliyoifanya katika Kijiji cha Nakiu kilichopo wilayani Kilwa, Mkoani Lindi Septemba 13, 2021 baada ya kupokea kero zilizohusu migogoro mingi iliyoanza kujitokeza katika Wilaya hiyo inayowahusisha wakulima na wafugaji.
Screenshot_20210914-170807_Instagram.jpg
 
Aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumpa fursa ya kuwa waziri.
“Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake.

Nawashukuru Wizara na taasisi zake kwa ushirikiano walionipa. Nashukuru wadau wa Tehama kwa ushirikiano mlionipa. Hongera sana Dk Ashatu kwa kuteuliwa. Kazi Iendelee” ameandika.

Juzi Samia alifanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri kwa kutengua uteuzi wa mawaziri watatu akiwamo Ndugulile na kuteua wapya wanne ambao ni Dk Ashatu Kijaji, Dk Stergomena Tax, January Makamba na Profesa Makame Mbarawa.

Ndugulile uteuzi wake ulienguliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Dk Kijaji ambaye ni mbunge wa Kondoa Vijijini.
Screenshot_20210914-171227_Instagram.jpg
 
Kikosi Cha BIASHARA UNITED kimerejea Nchini salama ambapo kilienda kucheza mchezo wa awali Kombe la Shirikisho CAF dhidi ya DIKHIL FC ya Djibouti

Na kufanikiwa kushinda mchezo huo Kwa bao Moja kwa Nunge, goli likifungwa na Kijana mdogo Denis Nkane

Timu ya Shaffih Dauda imezungumza na uongozi wa Biashara United kupitia Meneja wao wa timu, Frank Wabare na amesema

Mikakati yetu ni ile ile, sisi ni WANAJESHI wa MPAKANI haturudi nyuma, moto tumeshauwasha lazima tutauzima wenyewe na huu moto hakuna wa kuuzima yoyote kwaiyo sisi tutafanya mambo makubwa

Hatutaki kuzalilisha Taifa letu, hatutaki kuwazalilisha mashabiki na wapenzi wa Biashara United, Mara na popote

Tunachohitaji ni Furaha ambayo tuliileta Djibouti basi waione live kwani walimiss kuona live, tunataka waone kwamba hatukubahatisha

Kuhusu kikosi ni kilelee kwa Mujibu wa Mwalimu asilimia 100% na watu wategemee mambo makubwa kutoka kwa Biashara United
Screenshot_20210914-171424_Instagram.jpg
 
Champions League

Cristiano Ronaldo the Teacher & Jadon Sancho the Student

Vijana wana bahati ya kucheza timu mmoja na Legend mwenye UEFA tano
Screenshot_20210914-171610_Instagram.jpg
 
Yanga imempa mechi mbili Kocha Wake mkuu nabi Ili kujua Hatima yake ndani ya klabu hiyo mechi izo ni Mechi ya Rivers Huko Nigeria Caf Cl na Simba Mechi ya Ngao Ya jamii Swali Kwenu:

1.Hivi Kwa Jinsi ulivo iona timu ya Yanga kwenye michezo yake miwili Iliyopita ya Zesco na Rivers Tatizo Liko wapi Kwa kocha ,Maandalizi au Wachezaji?

2.Maandalizi Walio yafanya Yanga Msimu huu na Aina ya wachezaji walio sajili walikuwa ni sahihi na hitaji la mwalim ili kuziba mapengo ya Nafasi zilizo achwa na Wachezaji walio ondoka Kutokana na Alichokiona msimu iliopita?

3.Yanga waliacha Wachezaji Wake Wengi muhmu wakiwemo makipa Wote wawili Na kusajili zaidi ya wachezaji 10 wapya Je unadhani muda Uliokuepo ulitosha Kwa kocha kujenga timu na kupata Muunganiko bora wakwenda kucheza CAF CL na Kutwaa Ubingwa wa Ligi baada ya Kipindi kirefu?

4.Unadhani yanga kama Wakimfukuza Kocha Wao Mkuu Ndio itakuwa Sululisho Kwako na kupata matokeo Mazuri?

5.Hivi Unadhani Yanga inakwama Wapi Ukiangalia Wamefanya Usajili mzuri kwa mujibu wao wana kocha Wa Viwango, Waalimu wazuri Wa Mazoezi na Viongozi Wazuri Shida iko wapi Tukiachana na Kocha?
Screenshot_20210914-171827_Instagram.jpg
 
VIONGOZI WANAHITAJI CONGOLE KWENYE HILI

Hivi wajua?

Pamoja na mambo yote hayo lakini Klabu ya Yanga imejipanga bwana, ilichungulia mbali na kuamua kufanya yale ya kiufundi zaidi

Kama ujuavyo Klabu hua inasajili sehemu mbalimbali kwamaana ya watu wa mataifa tofauti na wenye kuzungumza lugha mbalimbali na hii wakati mwingine huleta shida hasa kwenye kuelewana

Lakini uongozi ukaona ujiongeze sehemu hii na kuleta Mtu sahihii na muhimu kwa wakati huu ambapo umesajili watu wa nguvu.

Sasa katika eneo hilo la Lugha ikamleta huyu hapa KARIM HELASI kutoka Nchini Dr Congo ili atumike kwenye kuunganisha watu kwenye Upande huo

Mr Karim yeye anayo uwezo Mkubwa wa kuzungumza Lugha Saba bila shida yoyote ile, anazungumza

Kiswahili, Kifaransa, Kingereza, Kireno, Kilingala, Kiarabu na Kihespagnol

Ni msomi kweli huyu, amesoma na anaijua kazi yake

Screenshot_20210914-172240_Instagram.jpg
 
"Hakuna shida kuhusu biriani litakuwepo kama kawaida, ila sasa tunatarget zaidi experience ambayo Mashabiki wataipata kwa kufika uwanjani ambayo haijawahi kupatikana popote pale" Mulamu, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Simba

Kwenye POWER BREAKFAST ya CLOUDS FM
Screenshot_20210914-172457_Instagram.jpg
 
Mambo kama haya unayapata sasa hivi kwenye Academy ya Manchester United

Ukitoka Old Trafford kumshuhudia Baba yake basi unaenda Carrington kushuhudia vitu vya Mwanae

Cristiano Jr is Red now.
Screenshot_20210914-172828_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom