Makapuku Forum

Makapuku Forum

Chelsea wana Kipa mzuri sana, haikuwa rahisi kwa mtoto wa Afrika kusimama kwenye milingoti ya Chelsea, huwa sio kawaida kwa makipa wetu kucheza EPL

Mpaka sasa Edouard Mendy

Mechi -4
Cleansheet -3

The wall
Screenshot_20210913-184722_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

NINI NACHOKIONA KWA YANGA AFRIKA HIVI SASA?

Mimi nitakuwa Mtu wa mwisho kuamini kuwa Yanga watakuwa na msimu mbaya sana, nitakuwa wa mwisho pia kuamini kuwa Yanga itapata matokeo mazuri mapema hii

Well ofcourse! Kwenye Football yetu ya Afrika haswa Kusini mwa jangwa la Sahara, sehemu ambayo football sio biashara kubwa kuna vitu vitatu, Yanga wanisikilize vyema tu

Kuna kitu kinaitwa GRB MODEL! Yes this is the model! G for Growth (Ukuaji), R for Result Oriented (Matokeo na Mataji) and B for Business (Biashara) hivi ndio vitu vitatu muhimu kwa huu ukanda wetu

Hoja yangu ni nini? Yanga wapo wapi?

Well hoja yangu ni kuwa Yanga kwasasa wapo kwenye GROWTH yani Ukuaji! Yanga si wamesajili? Wamesajili wachezaji watakaoikuza timu, haswa wenye uzoefu

Wazoefu ni kama hao wakina Heritier Makambo, Djuma Shaban, Jesus Moloko, Yannick Bangala, Djigui Diarra na wengine ambao ni push to start, kisha wachezaji Yoso kama Yusuph Athuman na wengine watakua kupitia timu

Hii ndio hatua waliopo kwenye GRB MODEL, na ndipo hapa watapitia magumu kidogo kwakuwa timu unajitafuta ili iende hatua inayofuata!

Kwenye hii hatua ya GROWTH nini kinapaswa kufanywa ila hakifanyiki? Hapa kuna shida ya KIUTAWALA! Yes kinachofanya Yanga wasiondoke hapa mapema ni Hiyo, ni kama wanataka kuivuka hii hatua lakini ni muhimu sana

Manchester United hawapo na Ole kwa bahati mbaya licha ya matokeo mabovu, Liverpool hawakuwa na Klopp kwa bahati mbaya na hata wale Simba wakati Sven anashinda kwa mbinde hawakubaki nae kwa bahati mbaya

Umesema shida ya Yanga ni KIUTAWALA? Yes! Hapo kuna shida, hawajaikubali hii hatua, wanataka shortcut na hii inazalisha presha kubwa kwa Wachezaji!

Nini kifanyike? Watawala waufuate mfumo wa Yanga na sio Yanga watoke kuufuata mfumo wao! Wataipoteza

Nataka nielezee GRB MODEL kama darasa kwa Yanga kupitia SIMBA maana wamefanikiwa sana, naomba andiko lijalo niwaambie kitu kuhusu SIMBA kwenye model hii! NITAREJEA

Screenshot_20210913-185511_Instagram.jpg
 
Achilia mbali ubora wake na uzoefu lakini Moja ya sababu iliyopelekea Bangala Litombo kuondoshwa pale FAR Rabat ya kocha Sven ni suala la utovu wa nidhamu

Bado haijaelezwa sababu ya Nabi kushindwa kumchezesha katika mechi muhimu ya jana
Screenshot_20210913-190257_Instagram.jpg
 
Tatizo mnaaminishwa sana vitu vya kipumbavu kuliko uhalisia, timu imara ya kushindana inaandaliwa kwa mikakati na siyo blabla, mpira una ABC's zake na lazima ziheshimike, uliwahi kuona wapi tangu dunia inaumbwa timu inawaacha kwa mkupuo magolikipa wake wawili tegemezi?

Lazima tukubaliane vilabu vyetu havina watu sahihi (watalaam) wanaofanya maamuzi, mipango endelevu pamoja na uchumi wa kuviwezesha kusajili wachezaji wenye uwezo wa kuja kuvisaidia kupata matokeo mazuri ya papo kwa papo kama wengi tunavyotaka, matokeo yake tunajikita kusajili wachezaji wenye majina makubwa badala ya kusajili wachezaji bora.
Screenshot_20210913-190448_Instagram.jpg
 
SENZO, MPISHI KWENDA NIGERIA LEO
.
Taarifa za hivi punde ni kwamba Yanga hawataki kukwama sehemu ndio maana hawaangalii tu mchezo wa jana na sasa Senzo ataondoka leo Jumatatu) mapema kwenda Nigeria.
.
Mbali na Senzo pia ataambatana na mpishi maalum wa Yanga anayewaandalia chakula kule kambini kwao Avic Kigamboni anaenda kuungana na kiongozi wake kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa kwenye misosi.
.
Uhakika kwamba matajiri wa Yanga jana hawakulala na sasa wanafanya taratibu za kupata ndege maalum ya Shirika la Tanzania litakaloipeleka timu hiyo siku mbili kabla ya mchezo.
.
Yanga tayari wana taarifa za kutosha kwamba Rivers wanaweza kuwaandalia mazingira magumu katika hatua za kuingia nchini humo lakini pia Senzo anatakiwa kwenda kuweka kila kitu juu ya hoteli na wapi watafanyia maandalizi yao.
Screenshot_20210913-190723_Instagram.jpg
 
Mjumbe wa Kamati ya Mashindano Yanga, Mhandisi Hersi Said akiwa kwenye foleni pamoja na Mdhamini wa klabu hiyo, Ghalib Saidi Mohammed (GSM) wakitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Zacharia Hans Poppe leo Karimjee jijini Dar. View attachment 1936257
simba na yanga sio uadui
 
Tatizo mnaaminishwa sana vitu vya kipumbavu kuliko uhalisia, timu imara ya kushindana inaandaliwa kwa mikakati na siyo blabla, mpira una ABC's zake na lazima ziheshimike, uliwahi kuona wapi tangu dunia inaumbwa timu inawaacha kwa mkupuo magolikipa wake wawili tegemezi?

Lazima tukubaliane vilabu vyetu havina watu sahihi (watalaam) wanaofanya maamuzi, mipango endelevu pamoja na uchumi wa kuviwezesha kusajili wachezaji wenye uwezo wa kuja kuvisaidia kupata matokeo mazuri ya papo kwa papo kama wengi tunavyotaka, matokeo yake tunajikita kusajili wachezaji wenye majina makubwa badala ya kusajili wachezaji bora.View attachment 1936301
watajuana wao kwa wao
 
Wenyewe mashabiki wa Arsenal wanasema Patrick Viera apewe timu maana ni kama Mikel Arteta

Viera ameliongoza chama lake Crystal Palace, weekend iliyopita kuvunja rekodi ya Nuno ya mechi tatu bila anawachelewesha
Screenshot_20210914-070907_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

KUNA KITU YANGA WANAPASWA KUJIFUNZA KWA SIMBA

Asubuhi nilisema kitu kuhusu GRB MODEL, nikasema ndio cycle sahihi kwa timu zetu huku Kusini mwa Jangwa, nikasema Simba ndio mfano mzuri wa hii kitu

Nikasema kwenye GRB MODEL kuna kitu kinaitwa GROWTH, nikimaanisha UKUAJI

Hapa kwenye Growth kuna vitu viwili vikubwa kwanza ni USAJILI! Ambapo nikasema Kuna saini ambazo wachezaji wanakuja kuikuza timu na baadhi wanakuja kukua na timu

Yanga wapo hapa! Na Simba waliwahi kuwepo hapa! Nilitaja saini za Yanga (rejea makala ya nyuma) ila kwa Simba walipokuwa hapa walileta watu wa kuikuza timu ambao wameproove sehemu kama Yanga walivyofanya msimu huu

Simba walileta watu kama Aishi Manula, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, John Bocco, Meddie Kagere, Chama na wengine ili waje kuikuza timu, ndipo hatua hii ya GROWTH, na ikamea vizuri sana

Ijapo wengi mlipiga kelele kuwa wanasajili wazee, lakini ndio ilikuwa inahitajika experienced players, ambao watakuja kuleta vitu viwili QR (Quick Reshuffle) na IS (Instant success) iwapo watafanikiwa

Kwenye hatua hii niambie Simba iliajiri Makocha wangapi? Unaweza kuona ndani ya miaka minne Simba wamesajili Makocha watatu tu na mmoja aliomba kuondoka!

Ikiwa na maana hatua hii ya GROWTH inatambulika kama ENTREPRENEUR PHASE! Unawekeza kwenye MUDA sambamba na RISK TAKING! Ni kitu ambacho Simba walifanya ila Yanga hawataki kufanya, wao wanatimua Makocha na kubadili vikosi

Ukitoka kwenye hii phase ndipo unakuja kwenye R! Ni RESULT ORIENTED! Ndani kuna ushindi na mataji! Hapa ndipo Yanga anapawaza bila kufata process

ITAENDELEA......
Screenshot_20210914-071201_Instagram.jpg
 
View attachment 1936743
Simba rahaaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom