Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210913-065154_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20210913-065216_Opera%20Mini.jpg
 
Kutoka viwanja vya Karimjee jijini Dar Es Salaam hizi ni picha nyingine za jinsi Watu mbalimbali walivyouaga mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Zacharia Hans Poppe.
Screenshot_20210913-172853_Instagram.jpg
Screenshot_20210913-173730_Instagram.jpg
Screenshot_20210913-173646_Instagram.jpg
Screenshot_20210913-173749_Instagram.jpg
Screenshot_20210913-173820_Instagram.jpg
Screenshot_20210913-174132_Instagram.jpg
Screenshot_20210913-174157_Instagram.jpg
Screenshot_20210913-174217_Instagram.jpg
Screenshot_20210913-174234_Instagram.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20210913-173506_Instagram.jpg
    Screenshot_20210913-173506_Instagram.jpg
    56.7 KB · Views: 1
Umoja wa Mataifa utafanya kongamano la kuchangisha fedha leo mjini Geneva kwa ajili ya juhudi zake za kuchangisha zaidi ya dola milioni 600 kwa ajili ya Afghanistan, Umoja huo unaonya kwamba huenda kukawa na mgogoro wa kibinadamu katika Nchi hiyo kufuatia Taliban kuchukua madaraka.

Kongamano hilo litahudhuriwa na Maafisa Wakuu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Katibu Mkuu Antonio Guterres na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas.

Hata kabla Taliban haijauchuka mji wa Kabul mwezi uliopita, nusu ya idadi ya watu nchini Afghanistan au Watu milioni 18 walikuwa wanategemea misaada, Umoja wa Mataifa unatahadharisha kwamba idadi hiyo huenda ikaongezeka kutokana na ukame na uhaba wa fedha na chakula.

Mataifa mengi ya kigeni yamesitisha utoaji wa misaada ya kifedha kwa Afghanistan kufuatia Taliban kuchukua madaraka jambo lililouwekea shinikizo kubwa Umoja wa Mataifa.
Screenshot_20210913-180903_Instagram.jpg
 
Korea Kaskazini imesema imefanikiwa kufanya majaribio ya makombora mapya ya masafa marefu, haya ndiyo majaribio ya kwanza kufanywa na taifa hilo katika kipindi cha miezi kadhaa na yanaonyesha jinsi Nchi hiyo inavyozidi kupanua uwezo wake wa kijeshi wakati ambapo kuna mkwamo wa majadiliano ya nyuklia kati yake na Marekani.

Kituo Kikuu cha Habari cha Korea kimesema leo kuwa makombora hayo ambayo yalikuwa yanaundwa kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, yamekwenda umbali wa kilomita 1,500 wakati wa majaribio hayo hapo jana na juzi Jumamosi.

Nchi hiyo imeyasifu makombora hayo ikisema ni zana zenye umuhimu mkubwa ambazo zinaafiki wito wa Kiongozi Mkuu wa Nchi hiyo, Kim Jong Un wa kuliongezea nguvu jeshi la Nchi hiyo.
Screenshot_20210913-181030_Instagram.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondono Godwin Gondwe amefanya ukaguzi wa ujenzi wa Barabara unaoendelea Wilayani humo kwa lengo kukagua utekelezaji wa bajeti mpya ya TARURA kwa mwaka 2021/22 ambapo amemshukuru Rais Samia kwa kuwapa Tsh. Bilioni 21.2 sawa na 150% kwenye bajeti hiyo.

“Tunamshukuru Rais katika mwaka 2020/2021 bajeti ya TARURA ilikuwa Bil 5.6 lakini bajeti ya mwaka huu 2021/2022 ametupa bajeti ya Bilioni 21.2 ameongeza bajeti kwa asilimia 150, haijawahi kutokea katika Wilaya yetu ya Kinondoni, sisi kama Viongozi kazi yetu ni kusimamia ndio maana niko nafuatilia”———-Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe
Screenshot_20210913-181149_Instagram.jpg
 
“Tumetoa fursa kubwa kwa Wamachinga kufanya biashara kama njia ya ajira kwao, wamekuwa wakifanya kazi katika maeneo tofauti na sasa wameenea kila mahali mpaka wanawaziba wenye maduka hawauzi Watu hawaingii ndani na hili linatukosesha kodi maana Machinga hawalipi kodi”

“Natoa wito kwa Wakuu wa Mikoa kuchukua hatua za kuwapanga vema Wamachinga ila naposema kuwapanga sitaki kuona yale ninayoona kwenye TV, ngumi kupigana, kufukuzana, vitu kumwagwa, mnaweza kuchukua hatua vizuri na kuwapanga bila kuwaudhi Wamachinga na mambo yakaenda”

“Wito wangu kwa Wamachinga wajitahidi kufuata sheria na kanuni zilizopo na wafuate yale wanayopangiwa na Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya”———-Rais Samia baada ya kuwaapisha Viongozi Ikulu, Dodoma leo
Screenshot_20210913-181528_Instagram.jpg
 
Katika kipindi cha miezi sita ya Urais wangu kuna Watu walichukulia Serikali poa, Serikali cool kwahiyo wakafanya wanayoyataka lakini hapa nilipofika nimeweka comma sio full stop, adjustment hizi (mabadiliko ya uteuzi) zinaendelea”

“Leo nimeapisha Mawaziri wanne na Mwanasheria mmoja na Wizara moja katika Wizara ambazo nimezipangua ilitakiwa Uongozi wake uwepo uape upya kwasababu sio Wizara ile ambayo waliapia nyuma, tutakavyoendelea Wizara hii nayo tutaifanyia marekebisho na watakuja kuapa”

“Mabadiliko haya (kutengua na kuteua) kutokana na jinsi nilivyoona utendaji wa Mawaziri wangu na Viongozi wengine kwenye Mawizara bado yatakuwa yanaendelea, mlioapa leo mkaanze kazi na mliopo makazini mkaendeleze kazi nami nakwenda kuendeleza kazi ya marekebisho”———-Rais Samia baada ya kuwaapisha Viongozi leo Ikulu, Dodoma
Screenshot_20210913-182003_Instagram.jpg
 
“Mawaziri wapya natumaini mtakwenda kufanya vizuri, uteuzi wenu hauna maana nyie ni wazuri kuliko waliokuwepo uzuri wenu utaonekana katika kazi, hata tuliowateua mwanzo walikuwa wazuri, nataka kuona matokeo sitaki kuwaona kwenye TV tu mnafanya hili mnafanya lile”

“Katika kipindi cha miezi sita ya Urais wangu nilijaribu kuwa mkimya na utulivu na nikawa nasoma Wizara zote yapo mengi ya kurekebisha, wapo pia ambao wakati nawasoma nao wakanisoma, wapo waliochukulia ukimya wangu na utulivu wangu kama udhaifu na wengine wakafanya kazi nzuri”

“Kipindi cha miezi sita ya Urais wangu nilikuwa najifunza, katika Uongozi kuna mbinu nyingi, Serikali yetu itaendeshwa na matendo makali na sio maneno makali, matendo makali sio kupigana mikwaju ni kwenda kwa Wananchi kutoa huduma inayotakiwa kila Mtu kufanya wajibu wake”

“Msitegemee kwa maumbile yangu haya pengine na malezi yangu kukaa hapa nianze kufoka nahisi sio heshima, na kwasababu nafanya kazi na Watu wazima naamini wanajua wanachokifanya, sitokaa nikaanza kufoka kwa maneno, nitafoka kwa kalamu” ———-Rais Samia baada ya kuwaapisha Viongozi wapya, Ikulu Dodoma leo
Screenshot_20210913-182146_Instagram.jpg
 
“Nimeamua kuvunja taboo ya muda mrefu kwamba Wizara ya Ulinzi lazima akae Mwanaume mwenye misuli yake lakini kazi ya Waziri kwenye Wizara ile sio kupiga mizinga wala kubeba bunduki ni kusimamia sera na utawala wa Wizara, nikaamua Dada yetu Dr. Tax nimpeleke huko”

“Kipindi chote tukienda SADC, Dr. Tax alikuwa anasimamia vizuri mambo yote ya usalama ndani ya region na alikuwa ana upeo mkubwa katika maeneo ya Afrika Mashariki kwahiyo kwa uzoefu alioupata katika masuala ya usalama anakwenda kutusaidia huko, yeye anajua vizuri Askari wetu waliopo Msumbiji, DRC Congo na kwanini wapo huko mifumo yao, wanavyobadiliia na pia haki zao”————Rais Samia baada ya kuwaapisha Viongozi wapya leo Ikulu, Dodoma
Screenshot_20210913-182304_Instagram.jpg
 
Msemaji wa Yanga, Haji Manara akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Zacharia Hans Poppe ambaye ameagwa leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Screenshot_20210913-182807_Instagram.jpg
 
“Nimeamua kuvunja taboo ya muda mrefu kwamba Wizara ya Ulinzi lazima akae Mwanaume mwenye misuli yake lakini kazi ya Waziri kwenye Wizara ile sio kupiga mizinga wala kubeba bunduki ni kusimamia sera na utawala wa Wizara, nikaamua Dada yetu Dr. Tax nimpeleke huko”

“Kipindi chote tukienda SADC, Dr. Tax alikuwa anasimamia vizuri mambo yote ya usalama ndani ya region na alikuwa ana upeo mkubwa katika maeneo ya Afrika Mashariki kwahiyo kwa uzoefu alioupata katika masuala ya usalama anakwenda kutusaidia huko, yeye anajua vizuri Askari wetu waliopo Msumbiji, DRC Congo na kwanini wapo huko mifumo yao, wanavyobadiliia na pia haki zao”————Rais Samia baada ya kuwaapisha Viongozi wapya leo Ikulu, DodomaView attachment 1936244
Wale waliokua wanashangaa why Tax katika wizara hiyo, waje wachukue jibu lao
 
Mjumbe wa Kamati ya Mashindano Yanga, Mhandisi Hersi Said akiwa kwenye foleni pamoja na Mdhamini wa klabu hiyo, Ghalib Saidi Mohammed (GSM) wakitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Zacharia Hans Poppe leo Karimjee jijini Dar.
Screenshot_20210913-182914_Instagram.jpg
 
Mlinzi wa kampuni ya Mast Holding Steven Felician Samandari (25) ameuawa kwa kuchoma kisu tumboni na watu wasiojulikana wakati akiwa kwenye lindo lake la baa MD Kepla wilayani hapa.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga, ACP George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hili akisema kuwa, tukio hilo lilitokea Septemba 11 saa 4 usiku mtaa wa Nyahanga.
Screenshot_20210913-183522_Instagram.jpg
 
Tendo la ndoa hufurahisha, na kadiri wakati umeendelea kusonga tangu enzi za mababu zetu, ni tendo ambalo limetokea kufurahiwa na wanaume na wanawake.

Hatahivyo wale wanaofanya tendo la ndoa wanaweza kuwa katika hatari ya kufa kifo cha ghafla, au wote wanaweza kupata maambukizi au kuugua wakati wa tendo hilo.
Screenshot_20210913-184038_Instagram.jpg
 
"Ninapenda nimuombe Waziri wa Tehama ambaye sisi Mahakama tunamtegemea sana kutusaidia kuingia katika karne ya 21, karne ambayo Rais uliwahi kusema inasukumwa na mapinduzi ya nne ya viwanda.

"Mahakama inategea mkongo wa taifa utaendelea kuunganishwa na mahakama zetu gharama za 'internet' zitashuka kwasababu hiyo ndiyo barabara iliyobaki ya kufika katika hayo mapinduzi manne ya viwanda," amesema Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma
Screenshot_20210913-184214_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom