Makapuku Forum

Makapuku Forum



Mikono ya kihamu ya Farhan Jr

Huwa tunasema barani Ulaya na duniani kote wenzetu wapo mbali na hakuna Afisa Habari anaepiga kelele, well tupo sahihi ila kuna kitu yatupasa tukifahamu

Sio kweli kwamba klabu duniani zinaendeshwa kwa makaratasi tu nikimaanisha Press Release pekee bali kuna watu maalum wenye vitengo maalum kwa ajili ya Mashabiki na Wanachama

Miaka kadhaa nyuma Mwanafunzi kutoka chuo cha Rotterdam School of Management, anaitwa Michael Vantoff, alifanya tafiti yakinifu kuhusu mtu anaitwa MKURUGENZI WA MASHABIKI au Meneja wa Mashabiki

Alifanya tafiti yake kwenye klabu za EPL hapo nchini England, ambazo karibia zote zina Mtu wa aina hiyo, ambae kazi yake kubwa ni kuwapa wajumbe wa bodi na Wakurugenzi hali halisi ya Mashabiki huko nje

Huyu ndie Muhamasishaji wa Mashabiki wote, huyu ndie anatumika mpaka kubalance upepo wa kimtandao (social Networks) na kuibua ari kwa Mashabiki, ni Mtu ambaye anafanya kazi nyingi za nje ya uwanja

Wale Mamelodi Sundowns wana Meneja wa Mashabiki anaitwa Alex Shokoena, yeye ndie anafatilia vikundi vya ushangiliaji, magroup ya WhatsApp na kila kitu kwa niaba ya bodi, ndio maana huwa tunasema wenzetu hatuwajui Maafisa Habari wao

Pale Yanga walikuwa na Antonio Nugaz, yule ndio kama Meneja wa Mashabiki, yeye alipaswa fanya yanayohusu Mashabiki na Afisa Mawasiliano anafanya yanayohusu klabu na Bodi

Simba kwasasa hawahitaji Afisa Mawasiliano au Habari kama Haji bali wanahitaji kuongeza nguvu kwenye kitengo cha Mashabiki na Wanachama, ndicho kitengo unachoweza kuwapa wakina Brother Mwijaku na wengine

Kwenye football panahitaji kelele, karaha na fujo ndio mtazamo wa familia ya mpira, ila wapewe watu Maalum kwenye kitengo maalum

Ulaya sio kwamba wapiga kelele hawana, bali ni watu tofauti na Afisa Habari
Screenshot_20210905-050954_Instagram.jpg
 
Hahhaha nimejichimbia huku karibu sana msalimie sana na ndugu yangu Shadeeya
Aisee, hili chimbo si mchezo kwakweli. Mtu unaweza kumaliza hata mwaka watu hawajakushtukia kama umepozi maeneo haya. Nilikua nazurura mitaa yoote ya JF ndio ghafla nakuona umeshakua mwenyeji huku kitaambo😀😀😀

Shaka ondoa Shunie, salaam kwa Shadeeya zimefika. Na hivyo walivyomsajili Manara ili awaletee ubingwa saa zote yuko anatabasamu tu😀😀😀
 
Aisee, hili chimbo si mchezo kwakweli. Mtu unaweza kumaliza hata mwaka watu hawajakushtukia kama umepozi maeneo haya. Nilikua nazurura mitaa yoote ya JF ndio ghafla nakuona umeshakua mwenyeji huku kitaambo

Shaka ondoa Shunie, salaam kwa Shadeeya zimefika. Na hivyo walivyomsajili Manara ili awaletee ubingwa saa zote yuko anatabasamu tu

Ubingwa watausikia kwenye bomba na manara wao

Huku bwana jina linawaogopesha watu ujue ila makapuku ni jina tu jamani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom