Makapuku Forum

Makapuku Forum

Cristiano Ronaldo tayari yuko Jijini Manchester tangu jana na pichani yupo na mchezaji mwenzake wa zamani ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Manchester United, Darren Fletcher

Ataanza mazoezi wiki ijayo na timu
Screenshot_20210904-141328_Instagram%20Lite.jpg
 
Wizara ya Afya imesema imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hii inayozunguka mitandaoni kuwa, Mtaalamu wa Afya katika kituo ambacho bado hakijatambuliwa amemshona Mgonjwa jeraha kisha akalifumua kutokana na Mgonjwa huyo kushindwa kulipia gharama za matibabu.

Wizara ya Afya imesema ikiwa hili limetokea nchini Tanzania, basi ni ukiukwaji mkubwa wa huduma za kitabibu, hivyo Wizara inaomba wenye taarifa za wapi huku au kituo gani wawasilishe mara moja kwa namba ya huduma kwa mteja 199 ya Wizara ya Afya au watume ujumbe mfupi kwenye namba ya Waziri wa Afya ya 0734124191.
Screenshot_20210904-143528_Instagram.jpg
 
: • “Watanzania wengi wanalalamika vitambulisho hatujapata tumeandikishwa, nitoe taarifa kwamba Serikali kupitia NIDA inaendelea vizuri na mchakato wa kutoa vitambulisho vya Taifa, mpaka sasa NIDA wameshatoa vitambulisho Milioni 9.4 na kati ya hivi Milioni 8.5 vimeshahakikiwa na vimepelekwa kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kupewa Wahusika na kati ya vitambulisho milioni 8.5 Watanzania ambao wameshachukua vitambulisho vyao ni Milioni 7.2”

“Kuna vitambulisho Milioni 1.3 bado vipo kwenye Ofisi za Wasajili, sasa baadhi ya Watanzania ambao wanalalamika hawajapata vitambulisho vyao ni hawa ambao hawajaenda kuvichukua, Serikali inatoa wito kwa Watanzania wote ambao mlijisajili muende mkafuate vitambulisho vyao wavitumie” ——— asema Msemaji Mkuu wa Serikali
Screenshot_20210904-143702_Instagram.jpg
 
“Tangu zoezi la chanjo lianze zaidi ya Watanzania 325,000 sawasawa na asilimia 31.5 ya chanjo zilizoletwa wameshapokea chanjo, zoezi linakwenda vizuri Watanzania wanaendelea kujitokeza kupata chanjo na Serikali inaendelea kuhimiza ambao hawajachanja wakachanje lakini msisitizo ni kwamba jambo hili ni hiari”——— asema Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa.
Screenshot_20210904-143842_Instagram.jpg
 
Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dar es salaam (DART) imetangaza ruti mpya ya Mabasi ya Mwendokasi ambayo yameanza kutoa huduma kuanzia Morroco hadi Kawe kupitia Barabara ya Old Bagamoyo jijini Dar es salaam.

Hii ni route ya tatu kwa Mabasi hayo kuanza kutoa huduma kwa siku za hivi karibuni baada ya kutangaza route ya Shekilango, Bamaga hadi Mwenge na route nyingine ya kuanzia Morroco hadi Mwenge.
Screenshot_20210904-144016_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom