Makapuku Forum

Makapuku Forum

“Kumekuwa na maneno yanaendelea kwamba kuna uwezekano wa kufuta Elimu ya msingi bila ada, sio kweli ni uzushi, Serikali itaendelea kutoa fedha kugharamia Elimu ya Msingi na Sekondari na tayari mwezi huu tumeshapokea zaidi ya Tsh. Bilioni 200, sera ya Elimu bila ada itaendelea kutekelezwa na sisi tutaendelea kusimamia”

“Nimetambulishwa hapa kama mnufaika na nakiri TAMISEMI imepokea kutoka hazina Tsh. Bilioni 22 .5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 90 na vitajengwa katika Halmashauri 82 za Tanzania Bara, fedha hizi tayari zmeshafika kwenye akaunti za Halmashauri husika, zitajenga vituo vya afya Katika tarafa ambazo hazina vituo vya afya”

“Nitoe maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa kupitia Sekretarieti za Mikoa kuhakikisha vituo hivi vya afya vinajengwa katika Makao Makuu ya Tarafa ambayo hazina vituo vya afya, na kama kwenye Tarafa kuna Hospitali ya Halmashauri fedha zipelekwe kwenye kata ya kimkakati ambayo haina kituo cha afya”

“Nasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri fedha hizi zikajenge majengo mapya sio kuleta ujanjaujanja wa ukarabati, sisi TAMISEMI tutasimamia kikamilifu matumizi ya fedha hizi na nawataka Wakuu wa Mikoa wasimamie matumizi ya fedha hizi, kuna ongezeko la Wanafunzi lakini pia nako tumepata fedha za kujenga madarasa 560 kutoka kwenye Bilion 7 ambayo Waziri Mwigulu ameahidi kutupa” ———-Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu
Screenshot_20210820-174602_GBInsta.jpg
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Ummy Mwalimu amepiga marufuku kutumia wakandarasi wa nje ya halmshauri husika huku akisisitiza kuwa fedha hizo zirudi kwa Watanzania kwa kuhakikisha kazi hizo zinafanywa na mafundi wa eneo husika.
Screenshot_20210820-174739_GBInsta.jpg
 
Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa tozo za miamala ya simu si michango ya kirafiki ni sheria ya Bunge iliyojadiliwa kwa miezi mitatu, na wabunge wameongelea matatizo ya wananchi.
Screenshot_20210820-175052_GBInsta.jpg
 
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) Martin Ngoga, amemuapisha James Kakooza wa Uganda kuwa Mbunge wa bunge hilo akichukua nafasi ya Mathias Kasamba aliyefariki Aprili 27, 2021.
Screenshot_20210820-175154_GBInsta.jpg
 
Mahakama ya Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka kulipa faini ya Sh8 milioni au kutumikia kifungo cha miaka minne jela katika makosa matano kati ya sita yaliyokuwa yakimkabili.
Screenshot_20210820-175258_GBInsta.jpg
 
Polisi wilayani Moroto Kaskazini mwa Uganda, wameanza kuwakamata watu wanaonunua chapati tano au zaidi, wakishuku huenda wanawalisha wezi wa mifugo katika eneo hilo huku wakidai kuwa kwa kufanya hivyo huenda kutawalazimu wezi hao kutoka mafichoni.
Screenshot_20210820-175452_GBInsta.jpg
 
"Tulipitisha tozo ya miamala, kwa kweli ndugu zenu wawakilishi hatujapitisha kitu kile kumkomoa mtu yeyote, tumepitisha kwa nia njema kabisa. Labda katika nia njema ile kuna maeneo hatukuangalia vizuri, basi tutajaribu kutizama vizuri huko tunapokwenda."- Spika Job Ndugai
Screenshot_20210820-175602_GBInsta.jpg
 
"Tuwaombe wananchi waendelee kuwa wavumilivu tujipe muda tu-engage na wenzetu kwamba, tulivyojumlisha kwetu na nyie huu mzigo umekuwa mkubwa sana kwa wananchi hivi kweli hatuwezi kuangalia nani apunguze wapi, kuna maeneo serikali imeenda kukutana juu kwa juu na watoa huduma na hii si kwa watu wa chini ni kwa watu wanaotuma miamala ya laki 8 au milioni 2"- Waziri wa fedha mwigulu nchemba
Screenshot_20210820-175741_GBInsta.jpg
 
KARIM BENZEMA IS HERE TO STAY|

Nyota wa Real Madrid, Kareem Benzema amesaini kandarasi ya miaka miwili zaidi kuendelea kuitumikia Real mpaka 2023

Baada ya Benzema kuongeza kandarasi, anaefuata ni Fede Valverde ambaye Madrid wana project nae ya muda mrefu
Screenshot_20210820-182628_GBInsta.jpg
 
Onyango atemwa Harambe Stars
.
Licha ya kufanya vizuri akiwa na kikosi cha Simba, Joash Onyango (28) hajaitwa katika timu ya Taifa inayojiandaa kucheza mechi za kufuzu kombe la Dunia Qatar 2022.
.
Onyango ambaye amejihakikishia nafasi katika kikosi cha Simba, awali alikuwa anapata nafasi kwenye timu ya Taifa lakini safari hii ameachwa kwenye mechi za kuwania nafasi ya kucheza kombe la Dunia.
Screenshot_20210820-183516_GBInsta.jpg
 
"Nimekuwa kimya kwa muda tangu mara ya mwisho nitume ujumbe wowote kwenye kurasa zangu za kijamii, ilibidi iwe hivyo kwa sababu kuna mambo nilikuwa ninakamilisha na nilikuwa nasubiri taratibu zote zikamilike, siwezi kuwaacha nyinyi kwenye giza,"
.
"Stori yangu ilianza pale nilipokuja Tanzania Mwaka 2018, sikuwa najua kwamba ningeweza kuwapata watu wengi kuweza kuongea Kiswahili lakini upendo ambao nimeweza kuupata hapa hauelezeki katika maisha yangu,"
.
"Siwezi kueleza namna ninavyohisi kuhusu Simba, kwa maneno machache ni kwamba bado ni ngumu kuamini kwamba jina langu halitatajwa na Baraka Mpenja msimu ujao ama sitavaa jezi yangu namba 17, katika timu ambayo ilikuwa ni ya nyumbani,"
.
"Asante kwa viongozi wa Simba, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mr Mo Dewji, CEO, Barbara Gonzalez, uongozi wa timu kiujumla, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenzagu pendwa asanteni kwa upendo wenu,"
.
"Kwa mashabiki nitazidi kuwakumbuka nasema asante sana nitazidi kuwasiliana nanyi kupitia mitandao ya kijamii, nitaendelea kushangilia pamoja nanyi labda ikitokea nikacheza nanyi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa heri na asanteni,"
.
- Clatous Chama.
Screenshot_20210820-183726_GBInsta.jpg
 
NABI HATAKI MZAHA YANGA
.
Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi amewataka wachezaji wake kuweka mbele nidhamu na atakaye kwenda kinyume, adhabu yake ni kukatwa dola 100 kwenye mshahara wake ambao ni sawa na Sh 230,000 za Tanzania.
.
“Kocha alisema hataki kuona wachezaji wake wakipata kadi zisizo kuwa za lazima uwanjani, lakini pia atakuwa mkali kwa wachezaji wanaochelewa kambini na mambo mengine ya kinidhamu atakuwa mkali na hatotaka masihara katika hilo, lengo lake ni kutaka kujenga nidhamu na umoja ndani ya timu,” amesema meneja wa Yanga, Hafidhi Salehe.
Screenshot_20210820-183839_GBInsta.jpg
 
DONE DEAL | Odergad ARSENAL
.
Arsenal imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo Martin Odegaard kutoka Real Madrid kwa ada ya uhamisho takribani Euro milioni 35.
.
Fundi huyo mwenye umri wa miaka 22 amesaini mkataba wa miaka minne na atavaa jezi namba 8.
Screenshot_20210820-184006_GBInsta.jpg
 
AWESU NAYE KUIBUKIA KMC
.
Kiungo fundi Awesu Awesu wa Azam FC yupo mbioni kujiunga na klabu ya KMC kwa mkopo huku mazungumzo kwa ajili ya dili hilo yakifikia pazuri.
.
Awesu amepoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha Azam FC tangu kocha George Lwandamina alipojiunga na timu hiyo, mwaka jana akichukua mikoba ya Aristica Cioaba aliyetimuliwa
Screenshot_20210820-184135_GBInsta.jpg
 
MTIBWA YAMKAUSHIA KESSY
.
Beki Hassan Kessy ameachana na Mtibwa Sugar baada ya mkataba wake kumalizika na mabosi wa timu hiyo kumkaushia kufanya naye mazungumzo juu ya mkataba mpya.
.
Licha ya kurejea nchini mwaka jana akitokea Zambia alikokuwa akicheza soka la kulipwa katika klabu ya Nkana FC, Kessy hakuonyesha kiwango bora na inaelezwa kwamba ndio sababu hasa ya wakata miwa hao kuachana naye.
Screenshot_20210820-184250_GBInsta.jpg
 
CONFIRMED | FRIENDLY MATCH
.
AS FAR RABAT SIMBA SC
Jumamosi | 21/08
12 Jioni.
Centre Sportif
.
Klabu ya Far Rabat ya Kocha Sven Vandebroeck kupitia ukurasa wake wa instagram imethibitisha kuwa Jumamosi hii itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Simba SC ya Didier Gomes.
Screenshot_20210820-184502_GBInsta.jpg
 
| Marco Asensio ARSENAL
.
Mabosi wa Arsenal wameandaa ofa ya Pauni milioni 34 ili kuangalia uwezekano wa kuipata saini ya kiungo wa Real Madrid na Hispania, Marco Asensio, 25, katika dirisha hili.
.
Mkataba wake unamalizika mwaka 2023. Alianza maisha yake ya soka Mallorca, kabla ya kusajiliwa na Real Madrid Novemba 2014.
Screenshot_20210820-184627_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom