NANI KUONDOKA NA CROWN?
NI siku saba (7) pekee zimesalia kabla ya nchi kusimama kwa muda kupisha pambano kubwa la masumbwi, litakalowakutanisha mabondia nguli wa uzani wa Super Middle (Kg 76) nchini, Dullah Mbabe na Twaha Kiduku.
Wawili hao watakutana Ijumaa ijayo Agosti 20, katika ukumbi wa ubungo Plaza Dar es salaam, katika pambano lao la tatu la marejeano lililopewa jina la 'PAYBACK NIGHT' wakiwania gari ya kisasa aina ya Crown.
Dullah Mbabe ambaye alipoteza pambano lililopita lililowakutanisha wawili hao amesema:"Twaha sio bondia, Twaha ni mbeba vyuma tu, hawezi kuwa bondia, mashabiki wangu wasiwe na wasiwasi tutashinda mapema tu."
Kwa upande wake Twaha Kiduku, amesema:"Naendelea vizuri na mazoezi, naomba mashabiki wangu waniombee na wategemee ushindi, Dullah Mbabe ni bondia mzuri lakini tutashinda kwa uwezo wa mungu."
Kesho tarehe 14 mabondia hao watakutana kwenye zoezi la 'FACE OF OF' mjini Morogoro, ambapo kutakuwa na mapambano 12 yatakayopigwa, huku pambano la Joseph Mchapeni na Dani Mwanafyale likisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa ngumi.
View attachment 1890957