Makapuku Forum

history in making
 
Itakua walikua na mazungumzo ya faragha sana...

Hutokea sana hii...
 
Rihanna ametangazwa kuwa ni sasa ndiye Mwimbaji wa kike tajiri zaidi duniani na ametangazwa na Forbes kuwa sasa ana thamani ya $ 1.7 bilioni na amejipatia pesa nyingine kupitia bidhaa zake za urembo za Fenty Beauty.

Rihanna pia amepata utajiri wake kutoka kwa kampuni yake ya nguo ya ndani, Savage x Fenty ambayo inaripotiwa kuwa na thamani ya $ 270m.

Imekuwa ni miaka mitano tangu Rihanna atoe albamu ambapo licha ya Mashabiki kumtaka aachie migoma mipya na album RiRi ameonekana kuwa busy sana na biashara zake zisizo za muziki.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kifo cha aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa kimeacha pengo Serikalini na Bungeni kwani Marehemu alikuwa mchapakazi, mwadilifu na mtulivu katika utendaji kazi wake.

Amesema hayo leo Jumatano Agosti 4, 2021 alipokwenda nyumbani kwa Marehemu Kwandikwa, Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani kutoa pole kwa familia.

“Mchango wake wa utendaji katika Serikali na Bunge ni mkubwa sana alifanikiwa kuwavutia wengi kwa tabia yake ya upole, unyenyekevu na uzingatiaji wa taratibu na sheria za utumishi kila alipopangiwa kufanya kazi hivyo kifo chake ni pigo kwa Taifa”———-Majaliwa

Majaliwa ameishukuru Familia kwa kuridhia maombi ya kutaka mazishi yafanyike Jumatatu ijayo ili kuwapa nafasi waombolezaji wakiwemo wabunge kupata nafasi ya kusafiri kutoka waliko na kushiriki katika kutoa heshima za mwisho na mazishi.
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani-Siasa, Victoria Nuland amekutana na Viongozi wa Vyama Vikuu vya upinzani Tanzania vya CHADEMA, ACT, CUF na NCCR.

Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani imesema ujumbe wa mkutano huo ulikua ———> “Wakati wote Marekani imesimama na itaendelea kusimama ikitetea haki na uhuru wa kimsingi”
 
Maandamano yamefanyika Nchini India baada ya kifo cha Raia mmoja wa Congo DR ambaye ni Mwanafunzi anaesoma Nchini humo ambaye amefariki akiwa chini ya ulinzi wa Polisi, Waafrika sita wamejeruhiwa kwenye maandamano haya yaliyofanyika kwenye mji wa kusini wa India wa Bengaluru.

Polisi mmoja amenukuliwa akisema Joel Shindani Malu (27) alizuiliwa na Polisi Jumapili kutokana na kuhisi anafanya biashara ya dawa za kulevya na hiyo ni baada ya kumkuta na vidonge vya maradhi ya kisaikolojia ambapo sasa kufuatia kifo chake Raia kadhaa wa nchi za Kiafrika walifanya maandamano nje ya kituo cha Polisi.

Gazeti la Hindu limesema Watu hao walioandamana walikuwa Wanachama wa "Pan African Federation" kundi ambalo lilianzishwa kulinda haki za Wanafunzi wa Kiafrika kwenye Mji huo, Waandamanaji hao pia walipinga taarifa za Polisi kwamba Malu amekufa kutokana na maradhi ya moyo.

Polisi wamefungua uchunguzi juu ya kifo hicho huku wakidai kwamba Mwanafunzi huyo alikuwa akiishi kinyume cha sheria Nchini India kwani hati yake ya kusafiria (passport) pamoja na visa vilikua vimemalizika muda wake toka mwaka 2017.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiambatana na Mkewe Mama Mbonimpawe Mpango hii leo August 4, 2021 amefika nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias John Kwandikwa Kibaha Picha ya Ndege ili kuwapa pole na kuwafariji Wanafamilia kufuatia kifo cha Waziri huyo.

Makamu wa Rais ameweka saini katika kitabu cha maombolezo na baadaye kuzungumza na Mke wa Marehemu Bi.Mareceline Kwandikwa ambapo amempa pole na kumuomba kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.

Baadaye akizungumza na waombolezaji waliojitokeza nyumbani hapo, Makamu wa Rais amemtaja Marehemu Elias Kwandikwa kama kiongozi aliyekuwa na sifa za kipekee.

Amesema Marehemu Kwandikwa alikua mcha Mungu, Mpole , Mtulivu na mtu aliefanya kazi kwa uwezo wake wote, amewataka waombolezaji kuendelea kuwa na moyo wa subira na kuwaombea faraja Familia ya Marehemu Elias Kwandikwa.
 
Polisi Dar es salaam wanawashikilia Watu wanne kwa tuhuma za kutishia Watu kwa bastola wanazozimiliki kihalali ambapo Watuhumiwa wote silaha zao zinashikiliwa na Polisi na taratibu za kisheria zitafuatwa ikiwa ni pamoja na kuwafutia umiliki wa silaha hizo.

Kamanda Muliro amesema ——— > “Watuhumiwa hao ni Isack Robert Wile maarufu Wambura,(44), Mkazi wa Sinza E, Rashid Iddi Mshana (36), Mkazi wa Mwenge, Mussa Rashid Mshana,(39), Mkazi wa Mwenge
na Ibrahim Shaibu,(52),Mkazi wa Kinyerezi”

“Mtuhumiwa wa kwanza, Isack Robert Wile (Wambura) akiwa katika Bar iliyopo Sinza alitoa silaha yake bastola aina ya Browning yenye namba TZCAR 72791 na kuanza kutishia Watu huku akiwa amelewa pombe” ——— asema Kamanda Muliro.

“Mtuhumiwa wa pili, Rashid Iddi Mshana alionekana kwenye video clip iliyosambaa kwenye mitandao akitishia, Polisi walimkamata Mtuhumiwa huyo akiwa na silaha bastola yenye risasi 10 ndani ya magazine ikiwa inamilikiwa na kaka yake aitwae Mussa Rashid Mshana”

“Mtuhumiwa wa tatu Mussa Rashid Mshana anatuhumiwa kwa kosa la uzembe ambapo alimwachia silaha mdogo wake ambaye ni Rashid Iddi Mshana ambae alijirekodi akitishia Watu kwa silaha na kutuma clip kwenye mitandao ya kijamii”

“Mtuhumiwa wa nne, Ibrahim Shaibu Aug 1 saa 12:00 jioni maeneo ya Vijibweni Kigamboni alimtishia kumuua kwa silaha jirani yake aitwae Chacha Mwita walipokuwa wanagombania mipaka ya kiwanja katika maeneo yao, Mtuhumiwa alikamatwa akiwa na silaha bastola aina ya LUGER ikiwa na risasi 06” ——— asema Kamanda Muliro.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia Watu wanne kwa tuhuma za kumuua Shabani Amiri Mbalali(20), Mchunga Mbuzi, Mkazi wa Chamazi.

“Watuhumiwa hao ni Anold Peter Kavishe 36, Jastin Joseph (32), Selemani Hamisi (39), Joyce John (39)

“Tarehe 31/07/2021 majira ya saa 11:30 jioni Shabani Amiri akiwa anachunga mbuzi maeneo ya Chamazi Vigoa aliuwawa na watu wasiofahamika na kuibiwa mbuzi watano na kisha mwili wake kufukiwa kwenye shimo”

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam lilianza ufuatiliaji mara moja na kufanikwa kuwakamata Watuhumiwa hao wakiwa na vielelezo kadha, Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo” ——— asema Kamanda wa Kanda Maalum Muliro Jumanne.
 
Jeshi la Polisi Dar es salaa limesema Madereva 6 wa pikipiki waliokamatwa baada ya kupita kwenye barabara ya mabasi ya mwendokasi watafikishwa Mahakamani, Madereva hao 6 ni miongoni mwa Madereva 118 wa Pikipiki waliokamatwa na Polisi kwa makosa mbalimbali Dar es salaam ambapo pikipiki zilizokamatwa kwa makosa mengine ya usalama barabarani zitakaguliwa na kulipa faini.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Jumanne Muliro amesema “Operasheni ya kukamata bodaboda ilianza tarehe Aug 2 na imefanikiwa kukamata pikipiki 118 zilizofanya makosa mbalimbali ya usalama barabarani kama ambayo ni kutovaa kofia ngumu(Helment) pikipiki 43, kupakia abiria zaidi ya mmoja (mshikaki) pikipiki 17, kutokuwa na leseni ya udereva pikipiki 20, kupita taa nyekundu Pikipiki 24”
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na Novemba Mosi, 2021 itakuwa siku yake ya mwisho baada ya kuitumikia kampuni hiyo yenye wateja katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika taarifa yake Vodacom imeeleza kuwa Bodi ya wakurugenzi iko katika mchakato wa kumpata mrithi wa Hendi, ambaye ameitumikia kampuni hiyo kwa miaka mitano, na pindi atakapopatikana na kuidhinishwa atatangazwa.
 
“Wabunge wanakatwa kodi ya ajira (PAYE) kwenye mishahara yao kila mwezi na kuwasilishwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa mujibu wa sheria kama ilivyo waajiriwa wengine wote wanaopata mishahara. “ Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipakodi na Mawasiliano, Richard Kayombo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…