”Nikiwa nimelala uso ukiwa umeegemea meza maalumu ya kukanda, nilisubiri kwa hofu. Mtaalamu wa kuchua kwa kutumia kisu, Elsa, kwa bashasha alikuwa ameshika visu viwili. Hii ni kwasababu wakati mwendo wa kukata unatarajiwa katika kuukanda mwili, katika hii, visu hufanya mithili ya ukataji.”
Ingawa inaonekana kuwa hatari,"masaji ya kisu" au "tiba ya kisu", inaaminika kuwa na nguvu za uponyaji na ni aina ya dawa ya Wachina ambayo inadhaniwa kuwa na zaidi ya miaka 2,000.
Elsa alianza kwa kutumia mikono yake kuukanda mwili wangu.
Kisha visu baridi, vya chuma vilianza kupita, juu ya mgongo wangu, mikono na kichwa changu. Nisingejua kuwa visu vilikuwa kazini kama haikuwa sauti ya visu vilivyokuwa vinagongana mara kwa mara.
Cha kushangaza, watu wengi husinzia baada ya kukandwa na visu kwa dakika 70.