Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,906
M/kiti wa CHADEMA Freeman Mbowe leo kwenye kongamano la BAVICHA Tabata amezungumza kuhusu hitaji la Katiba mpya ———> “Katiba yetu ina mapungufu, miaka mitano iliyopita imetupa funzo kubwa ukiwauliza wa CHADEMA na wa CCM wote wamejifunza, jambo muhimu ambalo ni Katiba mpya iliyo bora"
“Tunapendekeza kuwe na Bunge la Katiba na lisiwe Bunge hili linaloendelea sasa wala wasituambie Bunge hili la sasa ndio liunde Katiba, ichukuliwe rasimu ya Warioba na Katiba na kisha iundwe rasimu ya Katiba mpya, sio gharama na tukiamua tutapata Katiba mpya mwkaa huu”——— Freeman Mbowe.
“Mapendekezo ambayo tungemwambia Mama kwenye mkutano na yeye, kwanza tunapendekeza Katiba Mpya, Mama aunde Tume ya Katiba na isiwe Tume ya CCM wala CHADEMA peke yake iwe Tume shirikishi itakayotambua makundi muhimu”
“Madai ya Katiba tutadai asubuhi, mchana hadi usiku, kama wanataka tukae mezani turidhie kama wasiporidhia tutakutana Barabarani, hatutoridhia kushiriki Uchaguzi wowote bila kuwa na Katiba au Tume ya Uchaguzi”
“Katiba ni mali ya wananchi na sio mali ya Viongozi, miongoni mwa mambo ambayo Rasimu ya Katiba ya Warioba ilibainisha ni kupunguza majukumu ya Rais , Warioba alipendekeza tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Tuwe na Mgombea Huru” ———Mbowe.