Kutoka Hospital ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye ibada ya kuaga mwili aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara TANROADS Injinia Patrick Mfugale.
Mfugale alifariki juzi tarehe 29 June 2021 katika hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma baada ya kuugua ghafla akiwa kwenye kikao cha kazi, mwili wake utasafirishwa hadi Dar es salaam kwa ajili ya heshima za mwisho na atazikwa tarehe 05 Julai 2021 Ifunda mkoani Iringa.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu leo amepokea taarifa ya CAG inayohusu matumizi ya fedha zilizotolewa BOT kati ya Mwezi January na March mwaka huu 2021 ambapo taarifa hii inatokana na agizo alilolitoa Rais Samia March 28,2021 wakati akipokea taarifa ya CAG kwa mwaka 2019/2020.
CAG Kichere amesema katika ukaguzi uliofanyika imebainika kuwa fedha zilizotolewa BOT katika kipindi hicho zilifuata taratibu zote isipokuwa baadhi ya malipo yaliyokuwa yanatoka Hazina Kuu kwenda katika Taasisi mbalimbali za Serikali yalibainika kuwa na mapungufu.
Mapungufu hayo ni pamoja na baadhi ya ya Taasisi kama vile Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kufanya malipo mara mbili kwa kazi moja au kuchelewa kutumia fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya malipo husika.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.