Baada ya kutokea kwa kifo cha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini Tanzania (TANROADS) Injinia Patrick Mfulage leo, imeelezwa kwamba kifo chake kimetokea baada ya kuanza kuugua ghafla wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi Jijini Dodoma, taarifa zaidi kukujia.
Mahakama ya Katiba nchini Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha miezi 15 aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo, Jacob Zuma baada ya kumkuta na hatia ya kukaidi agizo la kufika Mahakamani ili kutoa ushahidi kuhusu shutuma za rushwa wakati wa utawala wake.
Mahakama ya Katiba nchini Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha miezi 15 aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo, Jacob Zuma baada ya kumkuta na hatia ya kukaidi agizo la kufika Mahakamani ili kutoa ushahidi kuhusu shutuma za rushwa wakati wa utawala wake.
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Donald Wright leo amezungumzia kauli aliyoitoa jana Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi huo leo imemnukuu Balozi Wright akisema ———> “Tangazo la Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Tanzania inajiandaa kuwezesha chanjo za COVID-19 ziweze kupatikana kwa wale wote watakaozihitaji ni hatua muhimu itakayoisaidia Tanzania na dunia kutokomeza COVID-19, Marekani ipo tayari kusaidia”
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla, amepokea Mabasi 70 ya Mwendokasi kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ya usafiri kwa Wakazi wa Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa kupokea Mabasi hayo RC Makalla amesema anafurahishwa kuona mafanikio hayo yamepatikana ndani ya siku 100 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambapo amesema upatikanaji wa magari hayo utaenda kutatua kero za Wananchi.
RC Makalla amesema Serikali imejipanga kutatua changamoto ya Mafuriko Dar es salaam hususani eneo la Jangwani ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu wa kusimama kwa huduma za usafiri nyakati za mvua.
Changamoto nyingine ambazo RC Makalla amezipokea kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa UDART na kuahidi kuzipatia ufumbuzi ni kero ya Bodaboda na magari binafsi kuingia kwenye Barabara za Mwendokasi na Wafanyabiashara kuendesha biashara zao kwenye Barabara za Mwendokasi.
Basilla Mwanukuzi jana June 28, 2021 amekabidhiwa ofisi rasmi ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Kisa Gwakisa ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe.
Baada tu ya makabidhiano ya ofisi DC Basilla ameanza kazi kwa kuonana na Wadau mbalimbali na kuanza kushughulikia masuala muhimu ya maendeleo yaliyokuwa juu ya dawati la DC.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo June 29, 2021 akitokea Jijini Dar es salaam.
Akiwa Dar es salaam jana Rais Samia alifanya Mkutano na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari Ikulu na leo anatarajia kuhudhuria Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa utakaofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma.
Basi kampuni ya Ulamaa T 330 DGB lililokua likisafiri kwenda Arusha kutokea Mwanza limepata ajali alfajiri ya leo kwa kuacha njia na kugonga nyumba eneo la Mkolani darajani Mwanza.
Imeelezwa kwamba ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na Watu 6 ambapo hakuna taarifa za kifo bali Majeruhi tu ambao wamepelekwa Hospitali ya Butimba.
Chanzo cha ajali kinaelezwa kuwa ni baada ya Dereva wa Basi kulikwepa gari dogo kulikosababisha gari kuacha njia baada ya kushindwa kulimudu, taarifa zaidi kukujia.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.