Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amemtaka Mbunge wa Mbogwe, Nicodamus Maganga ahudumie Wananchi akizingatia utaratibu wa Nchi na iwapo anataka kulipwa kwa dola kama alivyoongea Bungeni juzi basi ahamie katika Nchi zinazofanya hivyo.
Kwenye mahojiano na millardayo Chongolo amesema ———> “Wananchi wamemtuma Mbunge kuwasemea changamoto zao zikiwemo za maji, elimu, umeme, barabara, hospitali, mazingira ya kufanyia biashara na huduma nyingine za jamii kama Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020/2025 inavyoainisha na sio kujizungumzia yeye binafsi, huo ni ubinafsi na CCM kamwe haitovumilia”
Mbunge Maganga alisimama Bungeni juzi na kuwataka Wabunge kuwaeleza Wananchi ukweli kuwa mishahara na posho wanazolipwa hazitoshi na hata jana akiongea na millardayo alisisitiza ———> “Mitandaoni tumekuwa tukitukanwa sana kuwa tunalipwa na hela yetu haikatwi kodi, wamesahau kuwa mpaka huyu kuitwa Mbunge amepitia njia gani”
“Vilevile huyu Mbunge anafuatwa na Watu wangapi kwa mfano Mimi naishi jimboni kila asubuhi lazima utakuta Wananchi huyu Mtoto ameishiwa damu, wengine ukawasalimie Hospitali utaona aibu tu kuwachangia, sasa ukiangalia mshahara wa Mbunge ni Milioni 3.8” ——— Maganga.
View attachment 1828735View attachment 1828736