Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Sylvain Ore ambaye anamaliza muda wake May 31,2021.

Rais Samia ameipongeza Mahakama hiyo ambayo Makao yake Makuu yapo Arusha kwa kazi inazozifanya na amemhakikishia Ore kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kutoa ushirikiano ikiwemo kushughulikia changamoto mbalimbali kwakuwa inatambua umuhimu wa majukumu yake.

Kuhusu Tanzania kufuta tamko la kuruhusu Taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs) na Watu binafsi kupeleka mashauri yao moja kwa moja katika Mahakama hiyo, Rais Samia amesema Tanzania Italiangalia jambo hilo lakini kwa sasa msimamo haujabadilika.
20210527_171027.jpg
 
Mitandao ya Kijamii ya Facebook na Instagram imewaongezea Watumiaji wake kipengele cha kuchagua kuficha idadi ya likes wanazopata kwenye post mbalimbali wanazoziweka na tayari kimeanza kufanya kazi hata kwa Watumiaji wa Tanzania.

Majaribio ya Watumiaji kuficha likes zao yalianza kufanywa na Mitandao hii toka mwaka 2019 wakiamini kipengele hiki pamoja na sababu nyingine kitawasaidia Watu kuitumia mitandao hii kwa uhuru pasipo kuhofia kama wamepata likes nyingi au la, ni kipengele cha hiari ambapo Mtumiaji akificha likes Watu wanaom-follow hawatoona idadi ya likes bali majina ya baadhi ya walio-like post yake lakini yeye ataona idadi.

Kipengele hiki kinapatikana kwenye upande wa kulia wa post ambako kikawaida huwa tunakwenda hapo tunapotaka kufuta post, ku-edit, ku-copy link pamoja na mambo mengine, Je kwa walichofanya Instagram kwa hii option unawapa asilimia ngapi kwa kutisha?
20210527_171227.jpg
 
Imefahamika kwamba hakuna ukweli wowote kuhusu taarifa za Rais Mstaafu Mh. Jakaya Kikwete kuumwa kama zilivyosambazwa jana, vilevile wakati habari hizo zinasambazwa hiyo jana May 26 Mstaafu JK alikua Nungwi Znz kwenye hoteli ya Kodoti Villas.

Mstaafu Mh. Kikwete amekuwepo kwenye Hoteli hiyo kwa wiki nzima kwa ajili ya muendelezo wa kuandika kitabu chake na anaendelea na ratiba zake za kila siku kama kawaida.

Hizi ni picha zikimuonesha baada ya mazoezi ya kutembea kilometa 5.4 (ambayo hufanya kila asubuhi) akiwa na Farasi wanaofugwa kwenye Hoteli hiyo, pembeni ni Walimu wawili wa mafunzo ya farasi, pamoja na picha nyingine na Wanafunzi.

Kwenye picha ya mwisho kwenye swipe ni Mh. Kikwete baada ya kurejea Dar es salaam jana mchana jijini na leo May 27 2021 saa sita mchana amewatunuku shahada mbalimbali wanafunzi wa chuo kikuu katika mahafali ya 51 duru ya 1.
20210527_201845.jpg
20210527_201909.jpg
 
Polisi wa Katavi wamethibitisha kutokea kwa kifo cha Mwanamke aitwae Farazia Nzigiyimana, Mhutu mwenye umri wa miaka 60 ambae alikua Mkulima wa Kijiji cha Kabanga, Kabungu, Wilayani Tanganyika ambae inaaminika ameuwawa na Mume wake aitwae Nestory Ntibigimana (62) usiku wakiwa wamelala.

"Ilikua saa tisa usiku Mwanaume huyo alimuua Mke wake kwa kumpiga na kitu chenye ncha butu kichwani na sehemu ya paji la uso, Mume wake pia ni Mhutu, baada ya tukio Mtuhumiwa alitoroka lakini akakamatwa, tulipomuhoji Mwanaume huyu akasema alifanya hivyo kwa sababu alikua anahisi Marehemu amekua akimloga" ——— RPC Benjamin Kuzaga.
20210527_202030.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa ahirisho la mwisho katika kesi ya kuchapisha maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inayomkabili msanii wa vichekesho, Idris Sultani na wenzake wawili.

Hatua hiyo imetokana na upande wa mashtaka kushindwa kupeleka mashahidi mahakamani kwa miezi mitano mfululizo, tangu Desemba 8, 2020 kesi hiyo ilipotakiwa ianze kusikiliza ushahidi.

Uamuzi huo umetolewa leo, Alhamisi Mei 27, 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kuendelea.

Hakimu Ruboroga amesema tarehe ijayo kama upande wa mashtaka hawatapeleka shahidi mahakamani hapo ataifuta kesi hiyo.
20210527_202223.jpg
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya Viongozi wa UWT Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige.

“CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu, Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyokiuka katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM” ——— Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi.

Kauli hii ya CCM imetolewa saa chache baada ya vurugu kutokea kwenye mazishi ya Mfanyabiashara Kuzola Madoda wa Arusha ambako Mbunge Magige alizuiwa geitini wakati akitaka kuingia katika eneo la maziko.
20210528_184554.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom