Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Longinus Tibishimwamu amethibitisha kifo cha Askari Polisi mmoja aliyekua doria ya kawaida kando ya Ziwa Victoria Mwalo wa Makoko, Kata ya Makoko Mkoani humo.

Kifo cha Askari huyo kilitokea wakati akipambana na Mhalifu aliyekimbilia kwenye maji ziwani ambapo RPC Tibishimwamu amesema Muhalifu huyo inadaiwa alikuwa Mvuvi haramu na sio Jambazi kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

“Askari huyo alimfuata ndani ya maji ili kumkamata alipojaribu kukimbia, bahati mbaya Askari akanaswa na nyavu ya samaki na kupeleka kifo chake” ——— RPC Tibishimwamu.
20210529_174733.jpg
 
Watoto wawili wa Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera wamepoteza maisha baada ya kulipukiwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.

"May 27 jioni Watoto hao ambao ni Daniel Joseph (14) na Charles Njora (16) wakiwa wanachunga ng'ombe waliokota chuma kinachodhaniwa kuwa ni bomu wakaanza kukichezea ghafla kikalipuka”

“Walijeruhiwa tumboni na mikononi likawachanachana wakafariki papohapo, tunachunguza kupata ushahidi wa kitaalmu kuthibitisha kama ni bomu na ni bomu la aina gani na pili lilifikaje maeneo hayo”———-RPC Kagera Revocatus Malimi.
20210529_174836.jpg
 
Wafanyabiashara Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma leo May 29, 2021, wameanza mgomo wakiwatuhumu baadhi ya Maafisa wa TRA kwa kuwabambikia kodi Wafanyabiashara wasiotoa rushwa kwao.

Kwenye mgomo huu Wafanyabishara hao wamesisitiza kwamba wanayo orodha ya majina ya Maofisa wote wabambikizaji na kuitaka Serikali kuingilia kati.

Tayari Mbunge wa Kasulu Mjini Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye wamefika Kasulu kufanya mkutano na Wafanyabiashara hao ili kuweka mambo sawa.
20210529_174952.jpg
20210529_175013.jpg
20210529_175032.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limemkamata na linaendelea kumhoji Fatuma Joswamu ( 23) kwa tuhuma za kumuiba Hospitalini Mtoto mchanga mwenye umri wa siku 12 tu.

“May 24,2021 saa kumi usiku alifika Hospitalini akijaribu kuwaongopea Wauguzi kuwa ni mjamzito alifunga vitambaa tumboni wakampa kitanda, asubuhi yake saa 12:45 asubuhi jirani yake akaenda nje akaacha katoto kake kachanga Mtuhumiwa akakachukua na kuondoka nacho”———RPC Kagera

"Mama aliporudi na kumkosa Mtoto wake akatoa taarifa kwa Manesi wakajulishwa Walinzi na wakazingira Hospital na kumnasa Fatuma, tulipomuhoji anasema ameolewa na Mumewe muda mrefu lakini hawajapata Mtoto na Mumewe anadai Mtoto hivyo ili kulinda ndoa yake yenye mgogoro akajifanya ana mimba, akapanga tarehe za kujifungua ndio kama hivi aibe Mtoto, tunamuhoji upelelezi ukikamilika atafikishwa Mahakamani”———Revocatus Malimi, RPC Kagera.
20210529_175132.jpg
 
Mitandao mbalimbali ya Zambia imeripoti taarifa za Kiungo wa Simba Sports Club Clatous Chama kufiwa na Mke wake Mercy Chama aliyefia Nchini kwao Zambia, taarifa fupi iliyotoka haijaeleza kwa undani chanzo cha kifo hicho, tunaendelea kufatilia zaidi na tunatoa pole kwa Chama, Ndugu, Jamaa na Marafiki.
20210529_175301.jpg
20210529_175322.jpg
 
Mitandao mbalimbali ya Zambia imeripoti taarifa za Kiungo wa Simba Sports Club Clatous Chama kufiwa na Mke wake Mercy Chama aliyefia Nchini kwao Zambia, taarifa fupi iliyotoka haijaeleza kwa undani chanzo cha kifo hicho, tunaendelea kufatilia zaidi na tunatoa pole kwa Chama, Ndugu, Jamaa na Marafiki.
20210529_175453.jpg
20210529_175542.jpg
 
Kutana na Ernest Nkwocha, Kijana wa Nigeria ambaye amejizolea umaarufu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutengeneza sanamu za Binadamu na Wanyama kwa kutumia matairi mabovu ya magari.

Hamasa yake ya kufanya ubunifu huu ilisukumbwa na hamu yake ya kutaka kuona Jiji la Lagos likiwa safi kwa kuondoa matairi yaliyotumika mitaani na sasa ndoto zake mpya ni kuufanya ubunifu huo ufike kwa Watu wengi Duniani.
20210529_175642.jpg
20210529_175702.jpg
20210529_175719.jpg
20210529_175758.jpg
20210529_175814.jpg
20210529_175832.jpg
20210529_175849.jpg
 
Serikali ya Tanzania itajenga chuo cha ufundi Mkoa wa Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 5000 ili kuongeza wigo na fursa za upatikanaji wa ujuzi na maarifa.

Akizungumza leo Jumamosi Mei 29, 2021 katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa chuo hicho uliofanyika jijini Dodoma, katibu mkuu wa Wizara wa Elimu, Dk Leonard Akwilapo amesema ujenzi wa chuo hicho utagharimu zaidi ya Sh17 bilioni kupitia mradi wa Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi (ESPJ) unaosimamiwa na wizara hiyo.
20210529_180717.jpg
 
Taarifa za kusikitisha ni kwamba mke wake kiungo wa Simba Clatous Chama amefariki leo nchini Zambia.

Taarifa zilizothibitishwa na kocha wa zamani wa Yanga na raia wa Zambia, Noel Mwandila ni kwamba mke wa Chama aitwaye Mercy amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.
20210529_180823.jpg
 
Kikao maalumu cha ushauri cha Mkoa wa Geita, kimeridhia kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Chato na kupendekeza mkoa huo mpya kuwa na wilaya tano, huku mkoa mama wa Geita ukibaki na wilaya tatu

Kikao pia kimeridhia hifadhi ya Taifa ya Rubondo kutoka Geita na kwenda mkoa mpya wa Chato.

Kikao hicho kilichokuwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, kimependekeza mkoa mama wa Geita kubaki na wilaya tatu ambazo ni Geita, Mbogwe na Nyang’wale.
20210529_180911.jpg
 
Wakazi wa mtaa wa Bugando jijini Mwanza wamevamia nyumba ya mwenyekiti wa mtaa huo wakishinikiza awasilishe Sh1.2 milioni walizochangishwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara na ofisi ya mtaa.

Akizungumza na Mwananchi Digital mkazi wa mtaa huo, Matiko Mwiteki amesema walikuwa wakichangishwa Sh1,000 kila Jumamosi kufanikisha ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa mita 300 kwa kiwango cha changarawe.

"Tunahofu kwamba fedha tulizochanga zimeliwa kwa sababu mwenyekiti kila tukimwambia atoe fedha hizo ili tununue vifaa vya kujengea barabara anatupiga chenga wakati mwingine anatumia lugha ya ubabe kutushinikiza tusifuatilie," amesema Mwiteki.

Jeni Yusuph amesema kutokana na jiografia ya eneo hilo kuwa na mlima mrefu, wakazi wa eneo hilo wanalazimika kubeba wagonjwa mgongoni au kwa kutumia machela kuwapeleka hospitali.

"Hapa ni karibu na hospitali ya Bugando lakini wajawazito wanapozidiwa tunalazimika kuwabeba mgongoni ili tuwapeleke hospitali kwa sababu huku magari hayafiki wala pikipiki," amesema Jeni.

Akijibu tuhuma hizo mwenyekiti huyo, Jumah Masanja amekana kutumia fedha hizo akiahidi kwamba fedha hizo hazitatolewa kama utaratibu wa kutoa fedha benki hautazingatiwa.
20210529_181102.jpg
 
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza katika kikao cha wadau wa mbegu za pamba kilichofanyika jijini Dodoma leo. Kikao hicho kilikuwa kwa ajili ya kujadili jinsi ya kupata mbegu bora ili kuongeza uzalishaji nchini. Picha na Edwin Mjwahuzi
20210529_181218.jpg
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya chama hicho kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga huku akiwataka wanachama wa chama hicho kufanya kazi kwa kushirikiana
20210529_181307.jpg
 
Kocha wa Yanga, Nesredine Nabi ametoa msimamo mkali kwa mastaa watatu wa timu hiyo akiwamo nahodha Lamine Moro waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu.

Wengine ni Metacha Mnata na Michael Sarpong.

Kuhusu Mnata na Sarpong kocha huyo amesema ameuagiza uongozi kuwakata sehemu ya mishahara yao na wapewe onyo kali kama watakavyofanya vivyo hivyo kwa Lamine.

Akizungumzia hatma ya unahodha wa Moro, Nabi amesema hajafikiria kumuondoa katika nafasi hiyo ingawa anatakiwa kujitathimini na kuwa mfano bora ndani na nje ya uwanja.
20210529_181704.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom