"Tunakuomba Rais Samia katengeneze amani na suluhu ya Taifa hili, mioyo ya Watu inavuja damu, msione aibu kuomba radhi pale mlipowakosea Watu, tunatambua kwenye Serikali yako Mama Samia wako wale Mawakala waliotumika kutesa Watanzania”
“Tunasikia kauli zako za kurejesha matumaini lakini haitoshi kwasababu unafahamu kwa miaka mitano mlibadilisha kanuni, sheria ili kuminya uhuru wa Vyombo vya Habari, uhuru wa Vyama vya siasa, Demokrasia, kuminya haki za Biashara, kuwatesa Wafanyabiashara wetu kwa kupitia kodi”
“Mama Samia kabla sijakutana na wewe na Viongozi wenzangu wa CHADEMA anza kuwekeni utaratibu wa kulitengamanisha Taifa kwa kurekebisha sheria zote ambazo ni kandamizi zinawaumiza Watanzania ili tukafanye ushindani wa haki na iwe haki kwa Watu wote"
"Nawaomba CHADEMA Watanzania wengi mna hasira na mnatamani kulipiza kisasi, Mimi kama Kiongozi wenu nasema, siku ambayo mtageuka kuwa Chama cha kulipiza visasi kwanza niondoeni Mbowe kama Mwenyekiti kwasababu siwezi kuwa Mwenyekiti wa Visasi, lazima tumuweke Mungu kwenye Uongozi wetu na Mungu ametuambia tusiwe Watu wa visasi” ——— Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa Arusha leo.