Makapuku Forum

Makapuku Forum

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya Viongozi wa UWT Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige.

“CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu, Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyokiuka katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM” ——— Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi.

Kauli hii ya CCM imetolewa saa chache baada ya vurugu kutokea kwenye mazishi ya Mfanyabiashara Kuzola Madoda wa Arusha ambako Mbunge Magige alizuiwa geitini wakati akitaka kuingia katika eneo la maziko.
20210528_184701.jpg
 
Ujerumani imesema inatambua visa vya kikatili na mauaji yaliyofanywa na tawala zake za kikoloni dhidi ya jamii za Herero na Nama nchini Namibia, mauaji ambayo kwa sasa yanatajwa kuwa mauaji ya halaiki.

Zaidi ya miaka 100 tangu mauaji hayo kufanyika, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Mass amesema Serikali ya Ujerumani inataka kuisaidia Namibia na vizazi vya wale waliouawa kwa kuwapa euro bilioni moja kama ishara ya kutambua maovu waliyotendewa.

Ujerumani pia itatoa dola bilioni 1.3 kusaidia katika miradi ya ujenzi na maendeleo, imeripotiwa kwamba kati ya mwaka 1884 na 1915, Ujerumani ilitumia mbinu za kikatili kuukabili uasi katika koloni lake la wakati huo lililoitwa Ujerumani Kusini na Magharibi mwa Afrika ambapo inakadiriwa kuwa kati ya Waherero 65,000 na Wanama 20,000 waliokuwa wakiishi eneo hilo waliuawa.
20210528_184803.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Dkt. Phumzile Mlambo Ngcuka Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake (UN Women), Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo May 28, 2021.

Katika mazungumzo yao Dkt. Phumzile amemshukuru Rais Samia kwa namna anavyounga mkono juhudi za kupigani masuala ya Wanawake na ameahidi kuwa UN itamuunga mkono katika juhudi hizo.
20210528_184949.jpg
 
Rais wa Syria Bashar al-Assad ameshinda muhula wa nne madarakani kwa kupata asilimia 95.1 ya kura zote zilizopigwa.

Vyama vya upinzani Syria pamoja na Mataifa ya Magharibi vimemkosoa Assad na kusema kwamba uchaguzi huo ulitawaliwa na udanganyifu.

Serikali ya Assad imesema uchaguzi uliofanywa Jumatano unaonyesha kwamba Syria inaendesha shughuli zake kikamilifu licha ya mgogoro wa mwongo mzima, Vita hivyo vimesababisha vifo vya Mamia kwa Maelfu ya Watu na wengine Milioni 11 ambao ni nusu ya idadi ya watu kupoteza makazi yao.

Spika wa Bumge Hammouda Sabbagh alitangaza matokeo jana na kusema kwamba asilimia 78 ya Watu walijitokeza kupiga kura ambayo ni zaidi ya Wasyria Milioni 14.
20210528_185530.jpg
 
UNAAMBIWA:

Utafiti wa Duke University Medical Center, Durham, North Carolina na mtandao wa Healthline unaeleza kuwa pombe haimfanyi Mtu asahau kilichotokea ila kinachotokea baada ya Mtu kulewa ubongo hugoma kabisa kutengeneza kumbukumbu mpya.
20210528_185650.jpg
 
UNAAMBIWA:

Serikali nchini Korea Kaskazini chini ya Kiongozi Mkuu wake Kim Jong Un imepiga marufuku Watu kuvaa suruali za kubana (Skinny Jeans), kutoboa masikio, pua na maeneo mingine mwilini pamoja na kunyoa kiduku kwa kupunguza nywele pembeni na kuziachia kubwa kwa nyuma kwa kile wanachosema lengo ni kuzuia tamaduni za Magharibi kujipenyeza nchini humo.

Chombo cha Habari cha Korea Kusini Yonhap New Agency kimesema majirani zao hao wanasema watachukua hatua zaidi kudhibiti tamaduni za Ulaya na America kuharibu vizazi vyao, Nchi hiyo imezuia pia Watu kutengeneza, kusambaza na hata kutazama video za ngono.
20210528_185747.jpg
20210528_185805.jpg
20210528_185821.jpg
 
UNAAMBIWA:

Puma waliwahi kumlipa Pele USD 120,000 (Tsh. Milioni 278.2) ili afunge viatu vyake mwanzoni mwa Mechi kwenye Kombe la Dunia 1970 ili Dunia nzima itazame wakati Pele akifunga viatu vyake kutoka Brand ya Puma kama sehemu ya matangazo ya biashara yao.
20210528_190851.jpg
 
Nyota wa rap, DMX alikuwa amepania kurejea kwa nguvu katika muziki kabla ya kifo chake kilichostua, na sasa albamu yake iko tayari kwa ajili ya kuachiwa leo Ijumaa Mei 28, 2021.

Lakini, rapa huyo aliyefariki akiwa na miaka 50 alitamba katika miaka ya tisini na mwanzoni mwa milenia hii akiwa na albamu tano zilizoshika nafasi ya juu katika chati za nyimbo baada ya kuzinduliwa, hajaweza kuona albamu yake mpya ya "EXODUS" ikiingia sokoni ikiwa imetayarishwa na Def Jam Recordings.

Kuna hisia za ukombozi katika albamu hiyo yenye nyimbo 13, mada ambayo inagusa hisia baada ya kifo cha msanii huyo.
Alifariki Aprili 9 akiwa hospitalini ambako aliwekewa mashine ya kumsaidia kuendelea kuishi kwa karibu wiki moja baada ya kupata shambulio la moyo.

20210528_191335.jpg
 
Askari polisi, Isaya Kawogo amefariki dunia baada ya kuzama katika Ziwa Victoria wakati akimkimbiza mtuhumiwa wa ujambazi.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Mei 28, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu akibainisha kuwa tukio hilo limetokea eneo la Mwisenge manispaa ya Musoma.

Amesema askari huyo pamoja na wenzake wakiwa doria walikutana na mtuhumiwa huyo na kuanza kumkimbiza.

“Yule mtuhumiwa alijitosa ziwani na askari aliamua kumfuata huko huko ziwani lakini akiwa katika harakati za kumkamata alinasa kwenye nyavu na kuzama. Mtuhumiwa alifanikiwa kuimbia,” amesema kamanda huyo.
20210528_191431.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linawashikilia askari wanne wa Jeshi la Akiba la Mgambo kwa tuhuma za kumpiga na kumuua, Liberatus Mkomed (40) mkazi wa kijiji cha Kumhasha.

Akizungumza leo Ijumaa Mei 28, 2021 Kamanda wa Polisi mkoani humo, James Manyama amesema tukio hilo limetokea Mei 23, 2021 saa tatu usiku katika kijiji cha Kumhasha wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma.

Amebainisha kuwa askari hao waliingilia ugomvi wa kifamilia kati ya Mkomed na mkwewe, Scolastica Bakunda na kuanza kumshushia kipigo mwanaume huyo kwa kutumia fimbo na chuma maeneo mbalimbali mwilini.

Amesema baada ya kufanya tukio hilo, askari hao walikimbia na kwenda kujificha lakini juzi Mei 26, 2021 walikamatwa na polisi.

"Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Wilaya ya Kibondo Mei 24, 2021 na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi," amesema Manyama.

Ameeleza kuwa upelelezi wa tukio hilo unaendea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu kukamilika.
20210528_191737.jpg
 
Kwa mara ya tatu msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz amechanguliwa kuwania tuzo za BET 2021 katika kipengele cha ‘Best International Act’ zitakazotolewa Juni 28, 2021.

Diamond anachuana na Wizkid, Burna Boy, Emicida, Headie, Aya Nakamura, Youssoupha na Young T & Bugsey.

Mwaka 2014 Diamond alitajwa kwa mara ya kwanza kuwania tuzo hizo na kuwa msanii wa kwanza Tanzania kufikia hatua hiyo. Aliwania kipengele Best International Act Africa lakini ushindi ulikuja kwenda kwa Davido wa Nigeria.

Mwaka 2016, Diamond akatajwa tena kuwania kipengele hichohicho huku washindani wake wakiwa ni Wizkid, Yemi Alade, AKA, Cassper Nyovest na Black Koffie ambaye ndiye alitangazwa kuwa mshindi.

Baada ya kutochaguliwa kuwania BET 2017, Diamond akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Juni 21, 2017 alisema lazima mwaka 2018 atachaguliwa kwani 2017 alishindwa kwa kuwa alikuwa na kazi ya kuwasimamia wasanii wa WCB Wasafi hivyo hakufanya nyimbo nyingi kubwa.

Licha ya matumaini hayo makubwa Diamond alijikuta akizikosa tuzo hizo mwaka 2018 na miaka iliyofuatia hadi mwaka 2021 alipotajwa tena.

Ikiwa atanyakua tuzo hiyo Diamond atakuwa msanii wa pili Tanzania kufanya hivyo baada ya Rayvanny ambaye aliishinda Juni 25, 2017 katika kipengele cha 'Viewer’s Choice Best New International Act' baada ya kuwabwaga wasanii kama Dave, Amanda Black, Changmo, Daniel Caesar, Remi na Skip Marley.

2001 na huandaliwa na kituo cha TV cha Black Entertainment Television, lengo la kuanzishwa kwake ni kusherehekea mafanikio ya kazi za Wamarekani weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji, michezo mengineo hasa upande burudani.
20210528_191833.jpg
 
Polisi Mkoa wa Mara wamesema tayari wanamshikilia Mwanaume aitwae Manyama Daraya (37) Mkazi wa Kata ya Kwangwa Wilaya ya Musoma kwa tuhuma za kumuua Mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miezi kwa kumpiga tumboni.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara Longinus Tibishimwamu amesema May 25, 2021 jioni, Baba huyo alikuwa amembeba mwanae baada ya Mama yake kwenda shambani, Mtoto alipoanza kulia akambembeleza kwa kumpiga.

"Mtoto alianza kulia kwa muda mrefu huku Baba yake akimbembeleza kwa taratibu lakini matumaini ya Mtoto huyo kunyamaza hayakuonekana ikabidi atumie nguvu kwa kumpiga tumboni ili anyamaze na kupelekea mauti ya mwanae, alipoona amefariki akamchimnia kaburi ili amzike ambapo alifumwa na majirani”———RPC Mara.
20210529_174222.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom