Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atawaapisha Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Taasisi siku ya Jumatano May 19, 2021 kuanzia saa 4: 00 asubuhi badala ya siku ya Jumanne May 18,2021 ambayo alitangaza awali.

Rais Samia pia ataawapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wa Mahakama Kuu Jumatatu May 17,2021 kuanzia saa 9:00 Alasiri.

Viongozi hao wataapishwa katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu Dar es salam.
20210516_145131.jpg
 
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 zinatarajiwa kuanza Visiwani Zanzibar ambapo uzinduzi utafanyika kesho Jumatatu May 17,2021 katika Kijiji cha Mwehe Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi.

"Mbio za Mwenge wa Uhuru zinaendelea tena baada ya kusimama mwaka 2020 na kwa mwaka huu Mwenge utakimbizwa kwa siku 150 tu baadala ya siku 195 kama ilivyozoeleka awali"———Waziri Jenista Mhagama
20210516_150016.jpg
 
“Kwa mwaka huu Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakimbizwa katika Wilaya za kiutawala, na sio katika Halmashauri za kiutawala, tutaanza na Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar kesho May 17,2021"———Waziri Jenista Mhagama leo Zanzibar

"Mwaka huu Wakimbiza Mwenge Kitaifa watakuwa ni Wanajeshi wakiwakilisha Kambi mbalimbali kwa kuzingatia pande zote za muungano na sifa kubwa yao ni wawe Vijana”———Waziri Mhagama
20210516_150152.jpg
 
"Tunatarajia October 14, 2021 Mbio za Mwenge zitahitimishwa Wilayani Chato Mkoani Geita, kumbukumbu za uanzishwaji na uhitimishwaji wa Mbio hizi unaendana na Viongozi wetu wa kitaifa walipotokea, Mkoa wa Kusini Unguja (ambako Mbio za Mwenge zitazinduliwa kesho) ametokea Rais Samia Suluhu na Chato tutakapokwenda kuhitimisha ndipo alipozikwa Hayati Dr. Magufuli, Mungu amlaze mahali pema JPM na tunamuomba Mungu ampe afya na umri mrefu Rais Samia”———Waziri Jenista Mhagama akiwa Zanzibar leo
20210516_180547.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom