Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210512_075602.jpg
20210512_075624.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameondoka asubuhi hii kwenda nchini Uganda ambapo leo May 12, 2021 atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika uwanja wa sherehe wa Kololo Jijini Kampala.

Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kuapishwa leo kuendelea kuiongoza Uganda kwa muhula wa sita baada ya kushinda uchaguzi wa January 14, 2021 kwa kuwashinda wagombea wengine kumi katika nafasi ya Urais (akiwemo Robet Kyaluganyi maarufu Bobi Wine) kwa ushindi wa 58% ya kura zote.
20210512_112539.jpg
 
Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kuapishwa baadaye leo kuiongoza Uganda hii ni baada ya kushinda uchaguzi wa January 14, 2021 kwa kuwashinda wagombea wengine kumi katika nafasi ya Urais (akiwemo Robet Kyaluganyi maarufu Bobi Wine) kwa ushindi wa 58% ya kura zote.

Museveni ataiongoza Uganda kwa miaka mengine mitano, ikiwa ni muhula wake wa sita madarakani tangu alipoingia madarakani January 1986 kwa mapinduzi ya kijeshi, hadi utakapofika uchaguzi mwingine 2026 atakuwa madarakani kwa miaka 40, sawa na miongo minne, wakati huo akiwa na umri wa miaka 81.

Museveni yupo kundi moja na Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang, Rais wa Cameroon Paul Biya, Rais wa Jamhuri ya Congo (Brazzaville) Denis Sassou Nguesso, na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki ambao mi Marais wakongwe Barani Afrika ambao hadi sasa bado wapo madarakani, kwa Afrika Mashariki Museveni anaongoza kwa kuwa Rais aliyekaa madarakani wa muda mrefu.

Ikulu ya Uganda imesema Marais takribani 10 wamethibitisha kushiriki shughuli za uapisho wa Museveni akiwemo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye tayari ameondoka Tanzania kuelekea Uganda.
20210512_112852.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe nchini Uganda ambapo baadaye leo atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni katika uwanja wa Kololo Jijini Kampala.

Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kuapishwa leo kuendelea kuiongoza Uganda kwa muhula wa sita baada ya kushinda uchaguzi wa January 14, 2021 kwa kuwashinda wagombea wengine kumi katika nafasi ya Urais (akiwemo Robet Kyaluganyi maarufu Bobi Wine) kwa ushindi wa 58% ya kura zote.
20210512_113115.jpg
 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewathibitisha Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Viti Maalum, Najma Giga na Mbunge wa Mufindi Kusini David Mwakiposa Kihenzile kuwa Wenyeviti wa Bunge.

Zungu na Najma Giga walikuwa Wenyeviti pia kwenye Bunge lililopita huku Kihenzile akichukua nafasi hiyo kwa mara ya kwanza.
20210512_121211.jpg
20210512_121229.jpg
20210512_121244.jpg
 
Miaka michache iliyopita kununua na kuuza mbegu na mayai ya uzazi lilikuwa jambo lisilofahamika nchini Kenya.

Ila kwa sasa imekuwa biashara inayokua kwa kasi kwa wenza wanaoshindwa kupata mimba na wanawake ambao hawajaolewa wakitafuta watoto kupitia njia ya urutubishaji wa mayai nje ya mwili (IVF), ambapo mbegu na yao hurutubishwa maabara na kuwekwa kwenye tumbo la uzazi.

Nchini Kenya, wanaume sasa wameamua ni wakati wa kuwa watoaji wa mbegu na wanawake wakichagua kuwa watoaji wa mayai.

Mtaalamu wa tiba aliwahi kutania kwamba, “hii itaepusha nafasi ya mwanamke kuchukua mtoa shahawa anayefanana na mwanaume waliyeachana au rafiki yake wa siri.”

Kwa mkupuo mmoja wa mbegu kwa mwanaume wa Kenya hulipwa kati ya Sh3,000 za Kenya (sawa na Sh65,000) hadi Sh10,000 (karibu Sh217,000).

Wanaume katika eneo la Afrika Mashariki kwa mfano Tanzania wanapata Ksh10,000 kama fidia. Ikiwa mwanaume wana sifa nzuri zaidi fidia hufikia hadi Ksh25,000 na Ksh30,000 (Sh651,000).
20210512_125028.jpg
 
Serikali ya Tanzania imesema inatarajia kuanza kutoa huduma ya upandikizaji wa mimba (IVF) kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22.

Huduma hiyo inaanza ikiwa ni miaka miwili sasa imepita tangu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuanza maandalizi ya utoaji wa huduma hiyo ikiwemo kusomesha wataalamu na kuandaa jengo litakalotumika kutolea huduma hiyo.
20210512_125243.jpg
 
"Nawatakia kheir Wauguzi wote katika kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani. Serikali inatambua na kuthamini mchango wenu katika jamii. Nawaahidi kuwa tutaendelea kuboresha mazingira na maslahi yenu ya kazi ili mtimize majukumu yenu vizuri na kwa usalama. Chapeni kazi, tunawategemea."
20210512_125415.jpg
 
Rais Yoweri Museveni tayari ameapishwa leo kuiongoza Uganda hii ni baada ya kushinda uchaguzi wa January 14, 2021 kwa kuwashinda wagombea wengine kumi katika nafasi ya Urais (akiwemo Robet Kyaluganyi maarufu Bobi Wine) kwa ushindi wa 58% ya kura zote.

Museveni ataiongoza Uganda kwa miaka mengine mitano, ikiwa ni muhula wake wa sita madarakani tangu alipoingia madarakani January 1986 kwa mapinduzi ya kijeshi, hadi utakapofika uchaguzi mwingine 2026 atakuwa madarakani kwa miaka 40, sawa na miongo minne, wakati huo akiwa na umri wa miaka 81.

Museveni yupo kundi moja na Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang, Rais wa Cameroon Paul Biya, Rais wa Jamhuri ya Congo (Brazzaville) Denis Sassou Nguesso, na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki ambao mi Marais wakongwe Barani Afrika ambao hadi sasa bado wapo madarakani, kwa Afrika Mashariki Museveni anaongoza kwa kuwa Rais aliyekaa madarakani wa muda mrefu.

Marais zaidi ya 10 kutoka Mataifa mbalimbali wameshiriki shughuli za uapisho wa Museveni akiwemo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
20210512_134434.jpg
 
Wakazi wa jimbo la Bihar magharibi mwa India wamekuta karibu miili 40 ya Binadamu iliyokwama na kuelea kwenye kingo za Mto Ganges ikitokea mji wa Uttar Pradesh, imeelezwa kuwa ni Wagonjwa waliofariki kwa COVID-19 na familia zao hazikuweza kugharamia maziko.

India ni miongoni mwa Nchi zinazoteseka na covid 19 duniani ambapo mpaka sasa ina Wagonjwa milioni 23.3, waliopona milioni 19.4 na waliofariki laki mbili na elfu hamsini na nne.
20210512_134541.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika uwanja wa Kololo Kampala nchini Uganda katika sherehe za Uapisho wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Rais Museveni ameapishwa leo kuiongoza Uganda kwa muhula wa sita mfululizo, hii ni baada ya kushinda uchaguzi wa Jan 14, 2021 kwa kuwashinda wagombea wengine 10 katika nafasi ya Urais (akiwemo Robet Kyaluganyi maarufu Bobi Wine) kwa ushindi wa 58% .
20210512_181713.jpg
20210512_181729.jpg
20210512_181803.jpg
 
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha kwenda Jela miaka minne Lameck Essau Meza (38), Mkazi wa Sikonge baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua bila kukusudia Mke wake, Dafroza Paul.

Lameck Meza alimpiga Mkewe na kumsababishia kifo chake, hii ni kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa Mahakamani.

Upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kwamba hii ni Mara ya pili kwa Lameck kuua bila kukusudia kwani alishawahi kusababisha kifo cha Mke wake wa kwanza kwa kumpiga na alihukumiwa kifungo cha miaka minne pia.
20210512_183924.jpg
 
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha kwenda Jela miaka minne Lameck Essau Meza (38), Mkazi wa Sikonge baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua bila kukusudia Mke wake, Dafroza Paul.

Lameck Meza alimpiga Mkewe na kumsababishia kifo chake, hii ni kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa Mahakamani.

Upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kwamba hii ni Mara ya pili kwa Lameck kuua bila kukusudia kwani alishawahi kusababisha kifo cha Mke wake wa kwanza kwa kumpiga na alihukumiwa kifungo cha miaka minne pia. View attachment 1782280
duuuh historia ndo inamtafuna
 
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally amesema hakuna taarifa za kuandama kwa mwezi leo na hivyo Waislamu wataendelea kufunga na kujiandaa na Sikukuu ya Eid Ijumaa May 14, 2021.

Sherehe za Eid El- fitr kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es salaam, swala ya Eid itaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 1:30 asubuhi.

Baraza kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limesema Baraza la Eid litafanyika katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa 8:00 mchana, Mgeni Rasmi anategemewa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
20210513_044204.jpg
 
Dereva wa Bodaboda Rogers John Kesi (17) mkoani Kilimanjaro ameuwawa na Abiria aliemkodisha kwa ajili ya kumpeleka nyumbani kwake, RPC Amon Kakwale amethibitisha.

“Ilikua ni May 10 2021 saa kumi na mbili alfajiri Polisi tulipata taarifa za kuuwawa kwake, alikodiwa kituoni Kiborloni na Mteja kumpeleka kwenda nyumbani kwake Mnazi Shani Tours, baada ya kufika Abiria ambae ni Mtuhumiwa aliingia na Rogers nyumbani ili kumuonesha mzigo wa kuubeba”

“Wakati Rogers akiwa kwenye harakati za kuuchukua mzigo huo ambao ni meza, Abiria ambae ndiye Mtuhumiwa aitwae Sifaeli maarufu Godson (21) Mmasai alimtokea kwa nyuma na kumpiga nyundo kichwani kwake na Marehemu akadondoka chini”

“Baadae Sifaeli alichukua waya na kumnyonga nao na alipohakikisha kwamba Rogers amekata roho alimpigia simu Rafiki yake wakashirikiana kuubeba mwili na kuuweka kwenye mifuko ya sandarusi, wakauweka kwenye pikipiki hiyohiyo na kwenda kutelekeza kandokando ya barabara kuu ya Moshi -Himo” ——— RPC Kakwale.
20210513_044324.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom