Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kufuatia uwepo wa ubovu wa baadhi ya barabara Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa Abubakar Kunenge ameelekeza TARURA kuhakikisha inaanza ujenzi na ukarabati wa barabara Muhimu zenye mashimo ili kuondoa kero na usumbufu kwa wananchi.
20210513_131549.jpg
20210513_131612.jpg
20210513_131644.jpg
 
Waislamu kwenye mataifa mengi duniani leo wanasherehekea sikukuu ya #Eid #al-#Fitr huku mataifa kadhaa yakiwa bado yameweka vizuizi vikali vya kukabiliana na janga la virusi vya corona.

Saudi Arabia, ambako ndiko kuliko misikiti miwili mitukufu ya Makkah na Madina, ilitangaza kwamba leo utakuwa mwanzo wa siku tatu za Eid, baada ya kukamilisha siku 30 za mfungo.

Nchi nyengine ambazo zinaadhimisha Eid leo ni Qatar, Jordan, Misri, Algeria, Syria, Muungano wa Falme za Kiarabu na Tunisia. Kwa upande wa Afrika Mashariki, Rwanda na Uganda zinaadhimisha pamoja na sehemu nyengine za ulimwengu hivi leo.

Lakini kwa Tanzania, ikiwemo Zanzibar, eid rasmi ya kiserikali ni kesho Ijumaa, kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Kiarabu kama vile Oman. DW Kiswahili inasema Eid Mubarak .
20210513_131826.jpg
 
MALAWI YATAKA KUGEUKIA KILIMO CHA BANGI

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ameonya hii leo kuwa mauzo ya zao la Tumbaku ambalo linaongoza kuliingizia taifa hilo fedha za kigeni yameshuka na kuhimiza wakulima kugeukia zao la bangi ambalo mwaka uliopita kilimo chake kimeidhinishwa kwa matumizi ya viwanda na matibabu .

Chakwera ameyasema hayo hii leo, wakati alipolihutubia taifa na kudai kwamba kwa muda mrefu, Malawi imekuwa ikitegemea Tumbaku kama zao kuu la biashara lakini utegemezi huo kwa sasa unatishiwa na kupungua kwa mahitaji ya Tumbaku duniani.

Bunge la Malawi lilipitisha muswada mwezi Februari mwaka jana wa kuhalalisha kilimo na usindikaji wa bangi katika matumizi ya matibabu na viwandani lakini bado inakataza bangi kutumiwa kama kilevi.
20210513_132003.jpg
20210513_132019.jpg
 
Watafiti nchini Tanzania kutoka chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) wamesema kuna uwezekano mkubwa kwa panya kutumika kutambua maambukizi ya virusi vya corona, Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi nchini humo.

Dkt.Georgies Mgode, mtafiti kutoka SUA ameliambia gazeti hilo kuwa wana imani kuwa panya wanaweza kutambua virusi vya corona kwa ufanisi mkubwa kwa sababu tayari wameona mafanikio ya jinsi panya wanavyoweza kutambua mabomu yaliyojificha ardhini na kutambua vimelea vya kifua kikuu.

"Vipimo vya virusi vya corona kwa sasa ni ghali na vinatoka nje ya nchi, lakini kwa kutumia panya itakuwa rahisi na itapunguza maumivu kwa wanaopimwa kwa vifaa."
20210513_132148.jpg
 
View attachment 1783125
Sawa!
 
Waislamu kwenye mataifa mengi duniani leo wanasherehekea sikukuu ya #Eid #al-#Fitr huku mataifa kadhaa yakiwa bado yameweka vizuizi vikali vya kukabiliana na janga la virusi vya corona.

Saudi Arabia, ambako ndiko kuliko misikiti miwili mitukufu ya Makkah na Madina, ilitangaza kwamba leo utakuwa mwanzo wa siku tatu za Eid, baada ya kukamilisha siku 30 za mfungo.

Nchi nyengine ambazo zinaadhimisha Eid leo ni Qatar, Jordan, Misri, Algeria, Syria, Muungano wa Falme za Kiarabu na Tunisia. Kwa upande wa Afrika Mashariki, Rwanda na Uganda zinaadhimisha pamoja na sehemu nyengine za ulimwengu hivi leo.

Lakini kwa Tanzania, ikiwemo Zanzibar, eid rasmi ya kiserikali ni kesho Ijumaa, kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Kiarabu kama vile Oman. DW Kiswahili inasema Eid Mubarak .View attachment 1783119
Minal faidhina
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili .
20210513_203239.jpg
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili, pamoja na hilo Rais amefanya teuzi mbalimbali kama inavyoonekana.
20210513_204432.jpg
 
Mtangazaji na Mwandishi wa Habari maarufu wa Kenya Larry Madowo amesajiliwa na CNN kuwa Mwandishi wao makazi yake yakiwa ni Nairobi Kenya kwa sasa ikiwa ni kazi aliyoipata muda mfupi baada ya kung'ara kwenye usajili mwingine wa BBC America ambao ulimfanya ahamie Marekani.

Deborah Rayner, Makamu wa Rais wa CNN anaesimamia ukusanyaji wa Habari Kimataifa ambae pia ni Mhariri anaesimamia Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika ndiye aliyetangaza usajili huu mkubwa wa Madowo ambae amekua Mfanyakazi wa BBC Amerika Kaskazini akiripoti Habari kubwa za Marekani kama janga la COVID 19, Uchaguzi Mkuu 2020 na maandamano ya kupinga kifo cha George Floyd.

Larry Madowo ambae alianza kazi ya utangazaji akiwa na miaka 20 ni miongoni mwa Vijana wanaotajwa kuwa na umahiri mkubwa na Vipaji vya hali ya juu kwenye Utangazaji Afrika na ametunukiwa Tuzo mbalimbali kwa umahiri huo huku akiwa anamiliki Master's ya Biashara na Uchumi kutoka Columbia University New York Marekani.

"Nimefurahia kuripoti habari mbalimbali za Marekani na sehemu nyingine za dunia na sasa ni faraja kurejea nyumbani kuripoti habari za Kenya na Afrika kwa ujumla, ni heshima kujiunga na Timu yenye vipaji ya CNN" amesema Madowo ambae amewahi kufanya kazi na NTV Kenya na CNBC.
20210513_204547.jpg
 
Hizi ni picha kutoka Wami linapojengwa Daraja jipya baada ya Daraja linalotumika sasa lililojengwa mwaka 1959 likiwa na urefu wa Mita 88.75 kutokidhi mahitaji ya sasa na kupelekea kusababisha ajali kila siku kwasababu ya wembamba wake unaofanya hata Magari mawili yashindwe kupishana.

Daraja hili jipya lina urefu wa Mita 510 na upana wa Mita 11.85 na linajengwa umbali wa Mita 670 pembeni ya Daraja la zamani huku gharama ya ujenzi wake ikiwa ni Tsh. Bilioni 67.779, ujenzi huu unagharamiwa na fedha za Serikali kwa 100% .

Mhandisi wa Matengenezo wa TANROADS Mkoa wa Pwani Eng. Wilicis Mwageni, amesema ujenzi umefikia 50.05% na unatarajiwa kukamilika September mwaka huu———“Daraja hili likikamilika Magari yatapishana na kutakuwa na njia za watembea kwa miguu kila upande, ajali zitapungua”
20210513_213028.jpg
20210513_213053.jpg
20210513_213145.jpg
20210513_213330.jpg
 
Attachments

  • 20210513_213028.jpg
    20210513_213028.jpg
    72.3 KB · Views: 4

Similar Discussions

Back
Top Bottom