Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,081
- 464,043
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo May 3, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo.
Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma ambapo Rais Mstaafu Obasanjo ametoa salamu zake za rambirambi kwa Rais Samia kufuatia vifo vya waliokuwa Marais wa Tanzania ambao ni Hayati Benjamin Mkapa na Hayati Dkt. Magufuli.
Obasanjo amempongeza pia Rais Samia kwa kupokea kijiti cha kuwa Rais wa Tanzania na amemtakia heri katika majukumu yake, katika mazungumzo yao wamezungumzia hali ya usalama Afrika na umuhimu wa Wakuu wa Nchi kujadiliana na kutafuta suluhisho la mipango migogoro ambayo inasababisha vifo vya Watu wasio na hatia hasa Wanawake na Watoto
Viongozi hao wamezungumzia masuala ya maendeleo hasa katika uchumi na kusisitiza umuhimu wa Nchi za Afrika kuongeza ushirikiano na kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji.

mtoto mlito