Aseee, inafikirisha sanaMnamo mwaka 1815 mtu mmoja anayeitwa Diderici alivaa nguo za bosi wake, ambaye alikufa kwa kiharusi, akavaa wigi na akaenda benki kujaribu kutoa pesa kutoka katika akaunti ya marehemu.
Mpango wake ulishindikana. Diderici alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi. Alikuwa anatumikia kifungo chake katika gereza la Prussia, Weikselmünde. Kulingana na rekodi za gereza, wakati Diderici pamoja na wafungwa wengine walipelekwa ndani ya uwanja kwa matembezi, kitu cha kushangaza kilianza kutokea: mwili wake ulionekana ukiwa mtupu (uchi) na mwishowe alitoweka ndani ya hewa nyembamba kama moshi.
Hii ilitokea mbele ya wafungwa na walinzi ambao walishangaa sana. Wakati wa mahojiano, mashahidi wote walisema kitu kimoja. Haikuweza kuelezeka na kuingia akilini kilichotokea. Mwishowe viongozi wa gereza walifunga kesi hiyo na wakachukulia kama "mapenzi ya Mungu". Tangu siku hiyo Diderici hakuwai kuonekana tena mahali popote.View attachment 1771420
Mkuu Shunie hongera sana, unaubeba vizuri uzi huuMnamo mwaka 1815 mtu mmoja anayeitwa Diderici alivaa nguo za bosi wake, ambaye alikufa kwa kiharusi, akavaa wigi na akaenda benki kujaribu kutoa pesa kutoka katika akaunti ya marehemu.
Mpango wake ulishindikana. Diderici alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi. Alikuwa anatumikia kifungo chake katika gereza la Prussia, Weikselmünde. Kulingana na rekodi za gereza, wakati Diderici pamoja na wafungwa wengine walipelekwa ndani ya uwanja kwa matembezi, kitu cha kushangaza kilianza kutokea: mwili wake ulionekana ukiwa mtupu (uchi) na mwishowe alitoweka ndani ya hewa nyembamba kama moshi.
Hii ilitokea mbele ya wafungwa na walinzi ambao walishangaa sana. Wakati wa mahojiano, mashahidi wote walisema kitu kimoja. Haikuweza kuelezeka na kuingia akilini kilichotokea. Mwishowe viongozi wa gereza walifunga kesi hiyo na wakachukulia kama "mapenzi ya Mungu". Tangu siku hiyo Diderici hakuwai kuonekana tena mahali popote.View attachment 1771420
Hatujambo moud za kwakoHamjambo kwenye uzi huu
Mwaka 2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano (115) mpaka miaka hiyo 17.
Atakapotoka na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69, jina lake anaitwa CARL GUGASIAN au maarufu kama 'The Friday Night bank robber'!
Jambo lililowashangaza wengi na ulimwengu wote ni jinsi gani binadamu mmoja aliweza kutekeleza matukio 50 ndani ya miaka 30 akiwa peke yake na FBI washindwe kujua identity yake wala kuwa na hata mbinu ya kuweza kumzuia au kumkamata.
ALIWEKA DHAMIRA AWE "MUHALIFU MWELEDI"
Baada ya kutoka jela Carl alidhamiria sasa kuwa ni lazima awe muhalifu mwenye weledi wa hali ya juu kiasi kwamba atafanikiwa katika kila tukio na hatoweza kukamatwa na akadhamiria kama anataka kufanikiwa aibe fedha nyingi kwa wakati mmoja basi sehemu sahihi ya kuiba ni bank na kama anataka kweli awe muhalifu mweledi anatakiwa ajue namna sehemu hizo (majengo na mifumo) zinavyofanya kazi, afahamu namna ya kutumia silaha na kujihami... INAENDELEA next post...
Baada ya kuweka dhamira hiyo Carl akachukua hatua ya kwanza na alichofanya ilikuwa ni kujiunga na Chuo kikuu cha Villanova ambapo alisomea Uhandisi wa umeme.
Pia mtaani alipokuwa anaishi alijiunga na kituo cha kufundisha mafunzo ya kujihami (karate and judo) ambapo alifanikiwa kupata mkanda mweusi (third degree black belt)
Moja kati ya vitu vilivyomsaidia Carl kufanya matukio ya uhalifu kwa mafanikio ni uwezo wake wa kuweka mkakati wa utekelezaji jinsi gani atakavyofanikisha azma yake! Ni dhahiri kuwa mafunzo ya kijeshi aliyoyapata yalimsaidia sana kuwa mwanamkakati mzuri wa kiufundi wa matukio! Carl alikuwa anatumia hadi miezi kadhaa katika kupanga utekelezaji wa tukio moja tu..
Baada ya kuamua ni bank gani atafanya tukio, Carl alianza tafiti juu ya tukio lenyewe atakavyolitekeleza... Kwanza kabisa Carl alianza kwa kusoma mandhari yanayozunguka bank na interest yake kubwa inaelezwa kuwa alitafiti zaidi msitu ambao unakuwa karibia na bank..
Baada ya kuufanyia tafiti msitu, inaelezwa kuwa Carl alikuwa anageukia kuitafiti bank yenyewe na wafanya kazi wake.. Kuhusu bank, angetafiti je hiyo bank inafungwa na kufunguliwa saa ngapi, ni siku zipi huwa wanachelewa kufunga, ni siku gani wanakuwa na kiasi kikubwa cha fedha n.k! Kisha akimaliza hapo anageukia kuwatafiti wafanyakaxi wa bank husika..
Baada ya kumaliza kufanya 'tafiti' zake Carl alienda hatua ya pili ya maandalizi ambapo ilikuwa ni kuandaa 'makazi na stoo' yake ya muda katika msitu uliopo karibu na bank ambapo alichimba handaki dogo kwa ustadi mkubwa na kulificha kabisa kwa juu mtu asiweze kujua kwa namna yoyote ile.. Moja ya wapelelezi ambao walihusika kufanikisha kumkamata Carl anaeleza Bw.
Ndani ya handaki kulikuwa na kila kitu ambacho angekihitaji, silaha, nyaraka za 'research', kifurushi cha kujikimu (survival kit), madawa ya dharura (first aid kit), vinyago vya kuficha sura (masks), fedha taslimu, majarida ya mazoezi ya kawaida na kijeshi na vitu vingine vingi..
Baada ya kumaliza maandalizi haya ya msingi Carl alijichimbia katika maktaba ya umma ya Philadelphia ambapo ndio alipafanya kama ofisi yake kwani inaelezwa kuwa alikuwa na mazoea ya kutumia muda mwingi hapo akifanya 'tafiti' na angekuwa hapo kwa wiki kadhaa ili ku-fainalize mpango wake na kufanya conclusion ya jinsi atakavyotekeleza tukio lenyewe..
Matukio yote ambayo Carl aliyafanya alikuwa anayetekeleza mwezi October au November ambapo maeneo mengi yanakuwa yapo kwenye kipindi cha winter au autumn ambapo kunaambatana na baridi kali pamoja na jua kuzama mapema!
Pia matukio yake yote aliyatekeleza siku ya ijumaa na hii ndio iliyomfanya apewe jina la 'The Friday Night bank robber'..
Uchaguzi wake wa muda wa kufanya tukio ulimpa advantage kadhaa.. Kwanza kipindi cha winter na autumn jua linazama mapema kwa maana ya kwamba katika Masaa yale yale ambayo bank zinakuwa zinafungwa lakini katika kipindi hiki cha majira ya mwaka giza linakuwa limeanza kuingia hivyo inampa mwanya mzuri kufanya tukio.. Pia kufanya tukio ijumaa ilimaanisha kuwa ndio siku nzuri kwa bank kuwa na kiwango kikubwa cha Cash.. Lakini pia alitumia sababu ya kisaikolojia kuwa ijumaa wafanyakazi wanakuwa distracted kutokana na weekend kuanza hivyo umakini unakuwa mdogo..
Kwahiyo alichokifanya Carl kwanza ni kupaka 'harufu' kwenye nyumba zote zilizo karibu na bank ili kuwachanganya mbwa wa polisi wakija kujaribu kutafuta trail ya alikoelekea!
Carl alikuwa anasubiri dakika 5 kabla bank haijafungwa ndipo alikuwa anavamia! Hii ilimpa possibility nzuri kuwa ndani kulikuwa na wafanya kazi pekee au Wateja wachache sana wamebakia..
Akishavamia bank alitoa bastola na kuamuru watu walale chini na wasimuangalie! Mashahidi wanaeleza kuwa kwa ustadi mkubwa (labda kutokana na mazoezi ya karate) Carl aliruka kutoka alipo mpaka kwenye droo za ma-teller na kuweka fedha zote alizozikuta humo kisha kwa ustadi ule ule aliruka tena mpaka upande wa wateja na kuwaamuru tena kwa msisitizo wasimuangalie na kabla hawajang'amua kinachoendelea Carl alikuwa tayari ashatoka nje ya bank na kutokomea katika msitu ulio karibu..
Carl anaeleza mwenyewe kuwa akiingia ndani ya msitu alikuwa anakimbia kwa dakika kadhaa kama kumi hivi mpaka mahala ambapo anakuwa ameficha baisikeli kisha anaendesha mpaka ndani ndani kabisa ya msitu kulipo na handaki lake, akifika kwenye handaki kila kitu anakiacha hapo; fedha alizoiba, masks, nguo, gloves etc kisha anavaa nguo nyingine za kawaida anaendesha baisikeli anaondoka!
Carl anasema alikuwa anacha wiki au miezi ipite mpaka stori kuhusu tukio la ujambazi zianze kufifia ndipo anarudi kwenye ule msitu na kuchukua 'hela zake'... Baada ya hapo maisha yanaendelea na anaanza 'tafiti' kwa ajili ya tukio linalofuata.. KUKAMATWA NA MAZINGAOMBWE YA HUKUMU
Kukamatwa kwa Carl kulikuwa kwa bahati mbaya mno!..
Kuna watoto walikuwa wanacheza katika msitu uliopo karibu na nyumbani kwao! Wakiwa ndani ya huo msitu waliokota PVC tube/pipe iliyokuwa imefichwa.. Baada ya kuifungua ndani walikuwa ilikuwa na bastola na vitu vingine kadhaa vinavyotia shaka. Wale watoto wakawataarifu wazazi wao na wazazi wao wakashauri vipelekwe polisi! Baada ya vitu hivyo kupelekwa polisi, vikachunguzwa na kukakutwa ramani..
FBI walitumia alama za vidole walizozikuta kwenye ile handaki na pia walitumia kijarida kidogo kinachohusu kituo cha mafunzo ya karate kumtrack down Carl mpaka wakampata.
Baada ya kukamatwa na kesi kufikishwa mahakamani ilikuwa ni dhahiri kuwa Carl atahukumiwa kifungo cha maisha au aghalabu miaka 115 pasipo uwezekano wa kupata parole kutokana na mashitaka yanayomkabili lakini mwisho wa siku Carl alikubaliana deal na FBI kuwa awaeleze nukta kwa nukta kuhusu matukio yote 50 aliyoyafanya, pia akubali kushirikiana na FBI kutengeneza programu maalum kuwasaidia maafisa wa FBI kutambua namna ya kuwabaini 'serial criminals', na pia awaelekeze kuhusu saikolojia ya ku-plan matukio ya uhalifu yaliyo perfect.!
Carl akakubaliana na masharti yote haya na mahakama ikapunguza adhabu yake kutoka kifungo cha maisha mpaka kifungo cha miaka 17 bila parole..
Hivyo basi ikifika 2021 Carl Gugasian anarudi uraiani! Inaelezwa kuwa huko gerezani Carl ni mtu mnyoofu mno na ni mfungwa wa kuigwa na ameendeleza desturi yake ya kupenda mazoezi hivyo yuko katika afya njema sana na wengi wanaamini atafika 2021 akiwa salama salimini na naamini kabisa Hollywood wanaomba usiku na mchana atoke salama.
Watu wa makapuku huwa mnafanya kazi sangapi za kuwaingizia kipato? Nimehoji hivyo kwa sababu muda wote mko busy texting kati hii forum.
Hivi kapuku ni mnyonge?