Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kuna kijiji nchini China, kinachojulikana kama "Long hair Village" (Kijiji cha Nywele ndefu).

Katika Kijiji hiki wanawake hukata nywele zao mara moja tu katika maisha yao, hukata nywele katika siku yao ya kuzaliwa ya 18 (wanapofikisha miaka 18).Wanafanya hivi kama sehemu ya kusherehekea kufikisha umri huo.

Utamaduni huu umetunzwa kwa zaidi ya miaka 2,000. Katika utamaduni huu kuwa na nywele ndefu huchukuliwa kama utakatifu na jambo lenye thamani zaidi.View attachment 1771212
Ndipo zinapotokea Peruvian na Brazilian hair...
 
Watu wa misri ya kale (Ancient Egyptians) waliabudu na kuheshimu sana Wanyama. Waliheshimu Wanyama kwasababu tofauti tofauti.

Mbwa walithaminiwa kwa uwezo wao wa kulinda na kuwinda, lakini Paka walichukuliwa kuwa wa kipekee zaidi.

Wamisri waliamini paka walikuwa viumbe wa ajabu, wenye uwezo wa kuleta bahati nzuri kwa watu wanaowafuga.

Kwa kuwaheshimu wanyama hawa, familia tajiri ziliwavalisha vito vya thamani na kuwalisha vyakula vya kifalme.

Jambo ambalo ni tofauti sana na maisha ya sasa, Kipindi hicho ilikuwa kama ikitokea Nyumbani Paka amekufa, watu wote wanaokaa kwenye nyumba hio wananyoa nyusi zote katika macho yao, lakini wale ambao nyumbani kwao Mbwa amekufa walikua wananyoa nywele zote mwilini hadi kichwani. Hii ilikua kama ishara ya kuomboleza na waliendelea kuomboleza hadi nywele zao zikikua.

Katika kipindi hiki Paka walikuwa maalumu sana kiasi kwamba ikitokea mtu akawaua, hata kwa bahati mbaya, alihukumiwa kifo.
20210502_172408.jpg
 
Pichani ni Tim Patch, raia wa Australia anayejulikana kwa jina maarufu la "Pricasso".

Tim Patch ni mchoraji maarufu sana huko Australia ambaye amepata umaarufu kutokana na kuchora picha kwa kutumia uume wake, korodani na matako.
20210502_172545.jpg
 
Barbara Baekeland alikua ni socialite maarufu na tajiri uko Uingereza. Aliolewa na kuachika miaka kadhaa baada ya kupata mtoto wa kiume waliemuita Anthony "Tony" ambaye alipokua alianza kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga).

Barbara baada ya kusikia kuwa mwanae ni shoga. Hakupendezwa kabisa na jambo hili, akawa anafanya kila namna ili kumtoa mwanae kwenye mambo ya ushoga. Alianza kumletea mwanae wanawake malaya wa kila aina ili afanye nao mapenzi lakini hakufanikiwa.

Mwaka 1972, baada ya kuona juhudi zake zinagonga mwamba ndipo alipoamua kuanza kumlazimisha mwanae wafanye mapenzi akiamini kufanya hivo itakua tiba ya kumkomboa mwanae kutoka kwenye ushoga. Anthony hakutaka kabisa kufanya hivo akaamua kumuua Mama yake kwa kumchoma kisu kifuani upande wa moyo.

Baada ya tukio ilo Tony alichukuliwa na kuanza kupewa matibabu akiwa chini ya ulinzi mkali hadi alipoachiwa mwaka 1980.

Alipoachiwa alienda kuishi kwa Bibi yake, lakini ndani ya wiki moja tu aliyoishi hapo, Tony alijaribu kutaka kumuua Bibi yake kwa kumchoma kisu. Alipelekwa mahakamani kwa kosa la kutaka kumuua Bibi yake. Siku ya kwenda kusikilizwa mashtaka yake mahakani Tony alikutwa amejiua mwenyewe gerezani.
20210502_172707.jpg
 
Pichani hapo juu ni Pablo Escobar na mwanae Juan.

Pablo Escobar alikua mfanyabiashara mkubwa sana wa madawa ya kulevya duniani. Alikuwa anasambaza na kumiliki soko la madawa ya kulevya kwa asilimia 80 duniani.

Sasa turudi kwenye hiyo picha apo juu. Hiyo picha ilipigwa mwaka 1981 nje ya geti la ikulu ya marekani (white house), kipindi hiko jamaa alikuwa ni muhalifu anaetafutwa sana na serikali ya Marekani (Most wanted criminal), lakini mwamba alipiga zake picha za kutosha na mapozi kama unavyoona, kisha akaondoka zake bila kustukiwa na mtu yeyote licha ya ulinzi mkali katika eneo ilo.
20210502_172836.jpg
 
Kila mwaka watu 30,000 hukusanyika pamoja katika mitaa ya Bunyol, Hispania, kushiriki pambano kubwa zaidi la nyanya duniani. Pambano linalofahamika kwa jina la "LA TOMATINA".

Kilo 125,000 za nyanya zinaletwa kupitia lori. Makombora 5 makubwa yaliyojaa nyanya yanalipuliwa angani kuanza pambano. Katika pambano hili kuna sheria mbili tu:

1) Lazima ubonyeze kila nyanya kabla ya kumtupia mwenzio kuona kama nyanya sio ngumu ili usimuumize mtu utakapomlenga.

2) Nyanya tu ndo zinazotakiwa kutupiana.
20210502_173256.jpg
 
Chung Ju-Yung, alizaliwa mwaka 1915 katika familia masikini ya kikulima huko Korea Kaskazini. Katika familia yao kulikua na watoto nane (8), yeye ndo alikuwa mtoto mkubwa kuliko wote. Huyu ndiye mwanzilishi wa Kampuni ya Hyundai.

Enzi izo akiwa kapuku (hana pesa) kabla ya kuanzisha Hyundai, alikua anaishi kijijini kwao uko Asan, alifanya majaribio matatu kukimbilia Korea Kusini lakini hakufanikiwa, Baba yake alimkamata na kumzuia. Hatimaye alifanikiwa mara ya 4 baada ya kuiba ng'ombe mmoja wa baba yake na kumuuza kwa pesa ambazo zilimsaidia kupata usafiri wa gari moshi (treni) hadi Seoul. Kipindi hiko alikuwa na miaka 16 tu.

Baadaye mnamo 1998, alituma ng'ombe 1001 kijijini kwao huko Asan, Korea Kaskazini kama malipo ya ng'ombe mmoja aliyeiba na kumuuza ili aweze kununua tiketi ya gari moshi (treni).
20210502_173420.jpg
 
Hapo juu pichani anaitwa Jason Vukovich, anayejulikana kama "Alaskan Avenger," au "Avenging Angel" yaani malaika wa kulipiza kisasi.

Juni 2016, alishambulia wanaume watatu aliowapata kwenye usajili wa majina ya wahalifu yaliyosajiliwa na serikali.

Februari 2018, Alihukumiwa kwa kutumia majina ya wahalifu yaliyosajiliwa na serikali na kuwafuatilia wahalifu hao, kuvunja nyumba zao, na kuwapiga kwa nyundo. Alihukumiwa kifungo cha miaka 23 gerezani kwa mashtaka kadhaa ya mashambulio na wizi. Walakini, watu wengi wanaamini kuwa Vukovich kweli ni shujaa.

Inaelezwa kuwa Jason alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa kijinsia alipokua mtoto. Hali ambayo ilipelekea kuathirika kiakili na kisaikolojia.

Vukovich alieleza mbele ya mahakama hadithi yake ya maisha ambayo ndiyo imeibua hasira yake dhidi ya wahalifu wa kijinsia. Vukovich alisema alikuwa akinyanyaswa kimwili na kingono na baba yake wa kambo kwa muda mrefu alipokua mtoto, hadi yeye na kaka yake mkubwa, Joel Fulton, walipoamua kutoroka nyumbani walipokuwa vijana. Kaka yake pia alithibitisha hilo mahakamani.

Tangu kufungwa kwake hadi leo hii kumekuwa na mijadala na maombi mengi ya kutaka Vukovich aachiwe huru.
20210502_173548.jpg
 
Huko nchini Scotland kuna kisiwa kinajulikana kama Kisiwa cha Majadiliano.

Kihistoria katika kisiwa hiki watu wale ambao walikuwa na mabishano au ugomvi walipelekwa kwenye kisiwa na kuachwa peke yao, wanaachiwa jibini na whisky.

Lengo la kupelekwa kwenye kisiwa hiki ni ili watu waweze kutatua shida zao wenyewe na ilikua hawawezi kuondoka hadi watakapofikia muafaka na kuelewana wote wawili.

Inaaminika kisiwa hiki kimetumika kwa namna hii kwa takribani miaka 1500 au zaidi, na katika miaka yote hiyo iliwahi kutokea kesi moja tu ya mtu kuuwawa akiwa huko.
20210502_173750.jpg
 
Huko nchini Mexico kuna kisiwa kinachojulikana kama "La Isla de las Muñecas" yaani kisiwa cha midoli. Jina hili limetokana na uwepo wa midoli mingi ya ajabu ajabu iliyoning'inizwa kwenye miti ya eneo ilo.

Simulizi hii inahusishwa na Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Don Julian ambaye ndiye alikua anaishi eneo ilo.

Don Julian alidai kuwa kisa cha kuning'iniza midoli hiyo katika miti kilianza muda mfupi baada ya kuhamia katika kisiwa hiko, alikutana na tukio la kutisha, alikuta mwili wa msichana mdogo ufukweni mwa kisiwa, na muda mfupi baada ya tukio hili, Don Julian aliona mdoli akielea majini karibu na alipokuta mwili wa mtoto yule.

Kwa kuwa alikuwa akiishi kisiwani peke yake, Don Julian alichukua mdoli yule, akamtundika juu ya mti kama njia ya kutuliza roho ya msichana yule mdogo aliyekufa. Lakini hakuishia hapo miaka iliyofuata aliendelea kutundika midoli ya kila aina.

Don Julian muda mwingine alikua akiokota midoli iliyotupwa jalalani na kuwatundika kwenye miti kisiwa chote. Alikua hachagui mdoli wa kuokota, aliokota vipande vya mdoli, visivyo na kichwa, miguu, macho yote aliokota. Kwa kawaida ni midoli ambayo inatisha ukiitazama.

Watu wengi walimuona kama ana matatizo ya akili hawakuamini kuhusu hadithi yake kuhusu msichana mdogo aliekufa, waliona ni kama hadithi ya kutungwa tu aliyoianzisha. Lakini jambo la kutisha katika hadithi hii ni jinsi mwisho wa maisha yake unavyoungana moja kwa moja na hadithi ya msichana mdogo aliyekufa.

Don Julian alikufa 2001. Mwili wake ulikutwa sehemu ile ile ambayo kila wakati alidai kuwa alikuta mwili wa msichana mdogo amekufa.
20210502_173903.jpg
 
Huko nchini Scotland kuna kisiwa kinajulikana kama Kisiwa cha Majadiliano.

Kihistoria katika kisiwa hiki watu wale ambao walikuwa na mabishano au ugomvi walipelekwa kwenye kisiwa na kuachwa peke yao, wanaachiwa jibini na whisky.

Lengo la kupelekwa kwenye kisiwa hiki ni ili watu waweze kutatua shida zao wenyewe na ilikua hawawezi kuondoka hadi watakapofikia muafaka na kuelewana wote wawili.

Inaaminika kisiwa hiki kimetumika kwa namna hii kwa takribani miaka 1500 au zaidi, na katika miaka yote hiyo iliwahi kutokea kesi moja tu ya mtu kuuwawa akiwa huko.View attachment 1771276
Tufanyae kama tunabishana Shunie tukatupwe kwenye hiko kisiwa mtu mbili tu...
 
Mwaka 1714, Meli 2 za kivita zilizokuwa zikiongozwa na Wessel na Bactmann, zilipigana kwa masaa 14, hadi meli moja ilipoishiwa silaha.

Nahodha wa Meli iliyoishiwa silaha alikuwa ni Wessel, alimtumia ujumbe mpinzani wake, kumshukuru kwa mpambano mzuri na kuomba kupewa silaha zaidi, ili pambano liendelee. Bactmann alikataa, lakini aliamua kuondoka na kumuacha mpinzani wake bila kumshambulia licha ya kuishiwa silaha.

Wessel alihukumiwa mahakamani kwa vita hii ya kiungwana kwa kosa la kutoa siri ya kuishiwa silaha kwa adui yake lakini baadae aliachiwa huru na kisha kupandishwa cheo kuwa Kapteni.
20210502_183404.jpg
 
Mwaka 1811, Tecumseh, kiongozi wa jadi marekani na vijana wake walikabiliwa na jeshi la marekani likiongozwa na William Henry Harrison. Vita vilipigwa katika Mto Tippecanoe na kumalimalizika kwa kushindwa kwa Tecumseh na kusababisha kifo cha kaka yake, Tenskwatawa. Vita hiyo ilitokana na kutetea eneo lao dhidi ya upanuzi mkubwa wa ardhi wa Marekani hadi magharibi. Tecumseh alikufa miaka miwili baadaye katika Vita vya Thames alipokua akiwasaidia Waingereza kupambana na Wamarekani.

Hapa ndo patamu sasa

Kulingana na simulizi, Tecumseh alitoa laana ambayo imewasumbua wamarekani kwa takribani miaka 200. Laana ilikuwa kwamba kila rais wa Marekani atakaechaguliwa katika mwaka unaogawanyika na ishirini na kuishia na sifuri atakufa kabla ya kumaliza kipindi chake.

Laana hii ilidhihirika mwaka 1841 wakati William Henry Harrison alipokufa kwa homa ya tumbo (typhoid) miezi michache baada ya kushinda uchaguzi mwaka 1840. Tangu wakati huo, laana hiyo hiyo ilipewa jina la "Laana ya Tippecanoe" au "Laana ya Tecumseh,".

Marais wengine waliokumbwa na laana hii ni
Abraham Lincoln, alichaguliwa mwaka 1860 na kuuawa mwaka 1865.

James A. Garfield alichaguliwa 1880, mwaka 1881 akapigwa risasi na kufa baadaye mwaka huo huo.

William McKinley alichaguliwa tena mwaka 1900. Alipigwa risasi mwaka 1901 na kufa wiki moja baadaye.

Warren G. Harding, aliyechaguliwa mwaka 1920. Alikufa kwa mshtuko wa moyo mwaka 1923. Uvumi unasema alilishwa sumu na mkewe.

Franklin D. Roosevelt, aliyechaguliwa tena mwaka 1940 kwa kipindi cha tatu, alipata kiharusi na kufa baada ya miezi 3 kuingia muhula wake wa nne mwaka 1945.

John F. Kennedy alichaguliwa mwaka 1960. Aliuawa mwaka 1963.

Ronald Reagan alichaguliwa mwaka 1980 lakini aliepuka kifo baada shambulio la risasi ya John Hinkley iliyomkosa kwenye moyo mwaka 1981.

George W. Bush alichaguliwa mwaka 2000, nae 2005 alikumbana na jaribio la kushambuliwa.
Ni Ronald Reagan na George Bush pekee ndio walionusulika kifo kutoka katika laana hii.

Mjadala kwa Sasa ni "Je, rais mteule wa Marekani 2020 bwana Joe Biden atafanikiwa kuepuka laana hii?"
20210502_183504.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom