Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210502_170520.jpg
 
Kutokana na sababu ya kupungua kwa kiwango cha uzazi, Kijiji cha Nagoro huko Japani kilikua kina wakazi 27 tu wanaoishi, bila watoto. Watu wa mji huo waliamua kuleta midoli 270 yenye muonekano wa binadamu katika kijiji hicho ili kukifanya kijiji kionekane kina watu wengi, na sasa kinaitwa Kijiji cha Nagoro Doll.
20210502_171014.jpg
 
Hii ilitokea huko Marekani, Kocha wa timu ya basketball ya shule ya Texas high School, aliyefahamika kwa jina la Micah Grimes, alifutwa kazi baada ya timu yake kushinda mabao 100-0.

Alifukuzwa kwasababu shule aliyokuwa akiifanyia kazi ilikua ni ya dini (ya kikatoliki), hivyo baada ya ushindi huo viongozi waliona kwamba kushinda kwa kiwango kikubwa kiasi hicho bila huruma hakukuonyesha picha nzuri kiukristo na pia halikua jambo la heshima kwa wapinzani wao pamoja na mashindano.
20210502_171156.jpg
 
Kuna kijiji nchini China, kinachojulikana kama "Long hair Village" (Kijiji cha Nywele ndefu).

Katika Kijiji hiki wanawake hukata nywele zao mara moja tu katika maisha yao, hukata nywele katika siku yao ya kuzaliwa ya 18 (wanapofikisha miaka 18).Wanafanya hivi kama sehemu ya kusherehekea kufikisha umri huo.

Utamaduni huu umetunzwa kwa zaidi ya miaka 2,000. Katika utamaduni huu kuwa na nywele ndefu huchukuliwa kama utakatifu na jambo lenye thamani zaidi.
20210502_171248.jpg
 
Antoine-Augustin Parmentier, alikuwa ni mfamasia wa ufaransa.

Wakati alipokuwa akihudumu kama mfamasia wa jeshi la Ufaransa, kipindi iko wakati wa vita kati ya Ufaransa na Prussia, alikamatwa na jeshi la Prussia na akawa analishwa viazi tu wakati wote wa kifungo chake. Wakati huo nchi yake ya Ufaransa ilikuwa imekataza kilimo cha viazi na kipindi iko viazi vilikuwa chakula cha nguruwe.

Alinusurika na kutoka mikononi mwa Prussia, akiwa mwenye afya na umbo zuri lililojengeka.

Baada ya kurudi kwao alianza kuwashawishi viongozi na wananchi kula viazi na kuwaelezea sifa za viazi. Kutokana na bidii yake, Ufaransa ilitangaza viazi kuwa chakula cha binadamu mwaka 1772.

Kaburi lake huko Paris limepambwa na mimea ya viazi kama njia ya kumuenzi.
20210502_171429.jpg
 
NiHivii Mwaka 1935, wavuvi walimkamata Papa na kumuweka kwenye bwawa la kioo kwaajili ya maonesho huko Sydney, muda mfupi baada ya kumuweka humo alitapika mkono wa binadamu.

Mtaalam wa Papa alithibitisha kuwa Papa hakuwa ameukata mkono huo kwa meno yake, bali mkono huo ulikuwa unaonekana umekatwa kwa panga.

Mkono huo pia ulikuwa na tatoo, ambayo ilifahamika kuwa ni ya mtu ambaye aliripotiwa kupotea wiki chache zilizopita.

Tukio ili liliibua na kusababisha uchunguzi wa kesi ya mauaji na hatimaye kukamatwa kwa wahalifu.
20210502_171613.jpg
 
Baada ya kupata homa na kufadhaika mwaka 1392, Mfalme Charles VI wa Ufaransa alianza kupatwa na wazimu (ukichaa) ambao ulidumu maisha yake yote.

Mojawapo ya wazimu wake maarufu alikua anaamini kwamba mwili wake ulikuwa umeumbwa kwa vioo.

Mara zote alikua akiogopa na kuutunza mwili wake wa kioo usivunjike, alikua anakataa kutembe tembea, mara nyingi alikaa kwa kutulia sehemu moja kwa muda mrefu.
20210502_171724.jpg
 
Huko Nyanda za juu, Papua New Guinea zamani kuliishi kabila la watu wanaoitwa Fore. Fore walikuwa hawajawahi kuchangamana na watu kutoka sehemu nyingine hadi kufikia miaka ya 1930 Wakati watafiti walipokwenda katika kijiji chao.

Fore walikua wanakula wafu wao (ndugu zao waliokufa) badala ya kuwazika ili kuwakinga wasiliwe na minyoo na funza. Ilikua ni kama ishara ya kuonesha upendo kwao.

Fore walikumbwa na ugonjwa wa ajabu "laughing death" (kifo cha kucheka) uliokua ukiua watu wengi sana hususani wanawake na watoto . Ugonjwa huo uliitwa KURU. Kuru ni ugonjwa unaotokana na kula ubongo wa binadamu.

Takribani nusu karne ilipita tangu watu wa Fore walipoacha kula wafu wao lakini janga hilo liliendelea kudumu hadi mwaka 2012 watafiti walipotangaza kuisha kwa ugonjwa huo. Mwathiriwa wa mwisho wa kuru alikufa mwaka 2009.
20210502_171849.jpg
 
UNAAMBIWA Valentina kutokea Russia ndiye mwanamke anaeshikilia rekodi ya dunia ya mwanamke aliyezaa watoto wengi zaidi akiwa na mwanaume mmoja tu, mumewe Feodor Vassilyev.

Valentina na mumewe walizaa jumla ya watoto 69 jozi kumi na sita za mapacha (mapacha wawili wawili mara 16 ambao ni jumla ya watoto 32), seti saba za mapacha watatu (mapacha watatu mara 7 ambao ni jumla ya watoto 21) na seti nne za mapacha wanne (mapacha wanne mara 4 ambao jumla 16). Ni sawa na kusema alizaa mara 27.

Watoto hawa wote aliwazaa kwa miaka 40 tu, kuanzia miaka ya 1725 hadi 1765.

Ukiachana na watoto hao 69, inadaiwa Feodor Vassilyev (mume wa Valentina) pia alikuwa na watoto wengine 18 ambao alizaa na mke wake wa pili. Hivyo Feodor Vassilyev jumla alizaa watoto 87.
20210502_172009.jpg
 
Imani hii inaitwa Reincarnation (Kuzaliwa upya), ni imani ambayo ipo tangu miaka mingi sana, zaidi ya miaka 1000 iliyopita na bado inaaminika hadi sasa.

Reincarnation ni neno la kilatin lenye maana ya "entering the flesh again", yaani kitu kile kile lakini kinaingia sehemu mpya. Miongoni mwa watu wenye imani hii ni watu wa dini za Kihindu (Hinduism),Budha (Buddhism) na Jain (Jainism).

Wanaamini kuwa mtu anapokufa nafsi yake inabaki duniani na kutafuta mwili kwaajili ya kuzaliwa upya. Mtu anapozaliwa upya hakumbuki chochote kuhusu maisha yaliyopita na anaweza kuzaliwa upya akiwa katika muonekano ule ule wa kimaumbile (same physical appearance) au akazaliwa akiwa katika mwili mwingine.

Inaelezwa kuwa kama ukiota kuhusu maisha tofauti na unayoishi sasa, basi ni dhahiri nafsi yako ilitumiwa na mtu kabla kwa namna hiyo, au ukienda sehemu na ukahisi umeshawahi kufika au hata kuota kuna sehemu kama hiyo, ni uthibitisho kuwa mtu mwingine aliyewahi kutumia nafsi yako alifika eneo hilo.

Licha ya dini hizi kuwa na imani sawa kuhusu kuzaliwa upya, lakini zinatofautiana kuhusiana na ukomo wa idadi ya kuzaliwa upya. Kuna wanaoamini hakuna ukomo wa idadi ya kuzaliwa upya, wengine wanaamini mwisho mara 7 na wengine mara 13.

Wanaoamini ukomo wa mara 13 wanaamini mtu akishazaliwa upya mara 13 ndipo nafsi yake hupotea jumla duniani, yaani ukifa basi roho yako atazaliwa nayo mtu mwingine, naye akifa itahamia kwa mwingine hadi mkifika watu 13 nayo inapotea mazima.

Kulingana na imani hii kuna namna ya kujua wewe ni uzao wa ngapi wa nafsi yako.

Mfano mimi nimezaliwa tarehe 18.03.1996, unajumlisha namba zote katika tarehe yangu ya kuzaliwa 1+8+0+3+1+9+9+6 unapata jumla 37. Alafu unajumlisha tena namba hizi 3+7=10, Jibu unalopata ndiyo idadi ya uzao wa nafsi yako uliopo, Kwahiyo mimi ni mtu wa 10 katika uzao wa nafsi niliyonayo, nikifa atazaliwa nayo mtu mwingine wa 11 hadi ifike mwisho 13.

Wanaamini kuwa binadamu anaishi mara moja, lakini roho yake inaishi maisha 13 ndipo inapotea kabisa duniani, japo inakuwa haina kumbukumbu yoyote juu ya maisha mengine ya nyuma.

Pia inaaminika kwamba watu wanazaliwa upya ili kukamilisha yale waliyopanga kabla ya kufa.
20210502_172127.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom