Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210502_044416.jpg
 
Mwaka 2013 vyombo mbalimbali vya habari kama CNN na mtandao wa the sun wa uingereza viliripoti taarifa ya mwanamke raia wa Australia aliyefariki baada ya kushambuliwa na jogoo bandani alipoenda kukusanya mayai ya kuku wake.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 76 ambae jina lake halikuwekwa wazi alishambuliwa na Jogoo mguuni na kusababisha damu nyingi kumtoka na kupelekea kifo chake.
20210502_044859.jpg
 
Mwanaume mmoja kwa jina la Ma Van Nhat raia wa Vietnam, mwaka 2017 alienda hospital baada ya kusumbuliwa na tumbo muda mrefu. Baada ya kufanyiwa vipimo aligundulika ana mkasi tumboni ambao ulisahaulika alipokuwa amefanyiwa upasuaji.

Upasuaji huu ulifanyika baada ya kupata ajali ya gari mwaka 1998 na bila Kujua wakasahau mkasi tumboni. Mkasi huo ulikuja kugundulika na kutolewa miaka 18 baadaye, mwaka 2017 siku alipoenda hospitali. Mkasi ulikutwa ukiwa na kutu.
20210502_045010.jpg
 
"MUNGU NI MKUBWA" ndilo neno lililotoka kwenye vinywa vya watu wengi baada ya kupata habari kuhusu tukio hili.

Mwaka 2019, Madaktari wa kituo cha matibabu cha Federal Medical Centre, Owerri, Nigeria walifanikiwa kuokoa maisha ya mwanaume mwenye umri wa miaka 35, Fundi ujenzi ambae alianguka kutoka juu ya ghorofa hadi chini na kuangukia kwenye nyundo iliyozama shingoni mwake na kutokea upande wa pili, kama jinsi picha inavyoonekana hapo juu pichani.
20210502_045103.jpg
 
Kuanzia miaka ya 1900's katika nchi za kiyaudi kuna aina ya ndoa zilianzishwa zinazoitwa shvartse khasene (Black Weddings). Ndoa hizi hufungwa na watu ambao wazazi wao wamefariki.

Kama mzazi au wazazi wako walifariki,
ndoa yako inaenda kufungiwa makaburini
huko huko ambapo wazazi wako walipozikwa.

Walikua wanafanya hivi kama njia ya kuomba msaada kutoka kwa wafu katika kumaliza majanga yaliyokua yanawakumba.
20210502_045213.jpg
 
Baada ya kifo cha binti yake Faviola aliyefariki mwaka 2018 akiwa na umri wa miaka miwili, Saundra Gonzales alianza kuona maajabu baada ya baadhi ya vitu kama maua na midoli aliyokuwa anaweka katika kaburi la mtoto wake kuanza kupotea bila kufahamu nani aliyekua anachukua.

Saundra akaamua kufunga kamera kwa siri ili kutaka kujua vitu hivyo vinapoteaje katika kaburi la mwanae.

Baada ya kufunga kamera kilichoonekana kurekodiwa katika kamera hiyo ni video ya msichana mdogo akiwa anacheza cheza kando ya kaburi hilo, baada ya Saundra kuitazama video hiyo vizuri aligundua kuwa binti huyo anayeonekana ni binti yake aliyezikwa.

Pia katika video nyingine ilionyesha binti huyo mdogo akiwa na mwanaume mrefu katika maeneo hayo ya makaburi. Hakuna uchunguzi uliofanikiwa na kutoa majibu kuhusu tukio hilo la ajabu.
20210502_045309.jpg
 
Huko nchini Thailand, kipindi hicho inaitwa Siam, kulikua na binti anaitwa Sunanda Kumariratana, alikuwa ni malkia wa Siam kuanzia mwaka 1877 akiwa na umri wa miaka 17 tu, hii ni baada ya kuolewa na mfalme Rama V wa Siam.

Sasa bwana Katika nchi hii ya Siam kulikuwa na sheria kali ambayo ilikuwa watu hawaruhusiwi kumgusa malkia, mfalme au hata mtu yoyote kutoka katika familia ya kifalme na kama ikitokea umemgusa basi moja kwa moja adhabu yako ni kifo. Ilikikuwa ni kosa kubwa sana mtu wa kawaida kumgusa mtu kutoka familia ya kifalme.

Siku moja mwaka 1880 malkia Sunanda akiwa na miaka 19 tu, yeye na binti yake walizama wakati boti yao ya kifalme ikiwa njiani kuelekea katika Ikulu ya Bang Pa-In Royal. Mashuhuda wengi wa ajali hiyo wakiwemo walinzi wake hawakuthubutu kabisa kumgusa malkia na kumsaidia wakati akizama, walishuhudia anakufa kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ajali. Toka siku hio sheria ikabadilishwa.
20210502_045436.jpg
 
Nadhani wengi wetu humu tushawahi kusikia au kushuhudia vile vimbwanga vya vyoo vya shuleni, wanafunzi kuona vitu vya ajabu, kusikia sauti za ajabu na harufu za pirau chooni. Sasa bwana sio bongo tu hadi nchi za wenzetu huko mambo haya yapo.

Huko Japan kuna Hanako-san, Hanako-san ni mzimu wa msichana ambaye anasumbua katika vyoo vya shule. Maelezo kuhusu sura na mwili wake hutofautiana, lakini anaelezewa huonekana amekata nywele na kuvaa sketi nyekundu.

Maelezo kuhusu asili ya Hanako-san pia yanatofautiana kulingana na vyanzo tofauti tofauti. Kuna wanaosema kuwa Hanako-san alikuwa mtoto aliyeuawa na mzazi mnyanyasaji katika choo cha shule; Wengine husema, alikuwa msichana aliyejiua katika choo cha shule na wengine wanadai alikuwa mtoto aliyedondokewa na ukuta wa choo wakati wa Vita vya pili vya dunia.

Inasemekana Hanako-san mara nyingi anaonekana katika vyoo vya wasichana. Ukitaka kumuona unabisha hodi mara tatu katika mlango wa choo au kuita jina Hanako-san ndipo anaitika.

Kulingana na hadithi hiyo, mtu anaebisha hodi au kumuita Hanako-san anaweza kuona damu, mkono au Hanako-san mwenyewe. Hanako-san anaweza kumvuta mtu huyo kwenye choo na kusababisha kifo kwa mtu huyo au Mtu huyo anaweza pia kuachwa bila
kudhuliwa lakini anaweza kuwa anamuona Hanako-San akiangalia kwenye kioo.
20210502_045553.jpg
 
Mwaka 1974, Mary Livingstone raia wa Uingereza, baada ya kifo cha mume wake ambaye alikuwa mtangazaji maarufu wa Radio & TV Jack Benny, alipokea maua mekundu. Baada ya siku kadhaa tena alipokea maua mengine aliyoletewa kila siku. Mary alianza kufatilia ili kujua ni nani alikuwa akimtumia maua hayo.

Baada ya kufatilia alikutana na muuzaji wa maua alimwambia kuwa maua hayo ametumiwa na Benny (mume wake) na kumueleza kwamba Benny kabla ya kifo chake alikua amelipia maua apelekewe mkewe kila siku katika maisha yake yote.

Mwaka 1983 Mary alikufa kwa maradhi ya moyo.
20210502_045710.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom