Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wakati Marcelo Bielsa alipoanza kuwa Kocha wa Leeds United, aligundua kuwa shabiki wa kawaida lazima afanye kazi masaa 3 ili kupata pesa ya kulipia tiketi ya mechi.

Kwa hiyo siku moja aliwaita wachezaji wake wote pamoja na kuwaambia kuwa waokote takataka katika uwanja wa mazoezi kwa masaa matatu.

Alifanya ivo kwasababu alitaka wajifunze kufahamu jinsi mashabiki wanavyofanya kazi kutimiza mapenzi yao kwa timu hiyo.
20210429_194546.jpg
 
Ana di Pištonja, au Baba Anujka, alikuwa muuaji hatari huko Yugoslavia, ambaye alifanya mauaji kati ya 50-150 kupitia "dawa za mapenzi" ambazo aliwauzia wanawake waliokua na shida katika ndoa zao.

Wanawake walipewa dawa hizi, zilizochanganywa na sumu bila wao kujua na kwenda kuwapa waume zao, ambao walifariki siku nane baada ya kutumia dawa izo.

Alikamatwa mwaka 1928 akiwa na umri wa miaka 90 lakini aliachiliwa baada ya miaka nane kwa sababu ya uzee.
20210429_194643.jpg
 
Agha Mohammed Khan alikua muanzilishi wa Qajar dynasty huko Iran.

Usiku mmoja wakati wamepiga kambi nje ya ngome ya Shushi, Agha Mohammad Khan aliletewa tikiti, alikula nusu alipomaliza, akaamuru ile nusu nyingine ihifadhiwe atakula kesho. Watumishi wake watatu wakala ile nusu iliyobaki, kesho yake wakati Agha Mohammad Khan alipotaka aletewe ile nusu iliyobaki, ilibidi wamuambie kwamba imeliwa.

Alikasirishwa sana na tabia ile, akaamuru wauawe. Kwa kuwa siku hiyo ilikuwa Ijumaa (Siku Takatifu katika Uislamu), aliamuru kunyongwa kwao kuahirishwe hadi siku inayofuata na kuwaamuru warudi katika majukumu yao.

Kwakuwa watumishi hao walikua wanajua kwamba Agha Mohammad Khan hashindwi kutimiza ahadi zake, haswa katika kuua mtu, waliamua kumuua kabla hajawaua! Waliingia ndani ya hema lake wakati amelala na kumchoma kisu kifuani akafa.
20210429_195051.jpg
 
Mwaka 2016 Julio Macias Gonzalez Kijana wa miaka 17 raia wa Mexico alifariki baada ya kupigwa Love Bite na mpenzi wake.

Baada ya uchunguzi Madaktari walisema kitendo hicho kilipelekea damu kusafiri hadi kwenye ubongo.

Wazazi wa kijana huyu walitupa lawama zote kwa binti aliyekua mpenzi wa mtoto wao ambaye baada ya tukio ilo inaaminika aliwekwa mafichoni kwaajili ya usalama wake.

Pia wazazi walieleza kuwa mara kadhaa walishawahi kumkataza kijana wao kuwa na uhusiano na binti huyo ambaye alikua na miaka 24, miaka 7 zaidi ya Julio lakini hakuskia.

Ukiachana na hii kesi ya Julio, Mwaka 2010 mwanamke wa miaka 44 kutoka New Zealand aliripotiwa kudhulika kwasababu hii pia.

Wazee wa maLove bite ujumbe wenu huo
20210429_195212.jpg
 
Florence Irene Ford alifariki akiwa na umri wa miaka 10, Wakati wa mazishi Mama yake alifanya ombi la kushangaza, aliomba jeneza la binti yake liwekewe dirisha dogo na ngazi kaburini kuelekea chini kwenye jeneza.

Kabla ya kufariki, Florence, aliyezaliwa Septemba 3, 1861, alikuwa anaogopa sana dhoruba. Mara tu kukiwa na dhoruba, alikuwa akimkimbilia mama yake, ambaye alimfariji kwa kumkumbatia hadi dhoruba hiyo ipite.

Mwaka 1871, akiwa na umri wa miaka 10, Florence alikufa kwa homa ya manjano. Mama yake akiwa amefadhaika, alitamani mwanae asizikwe, kwani bado alikuwa anataka kumfariji wakati wa dhoruba, hata alipokuwa amekufa.
20210429_195321.jpg
 
Aaron Chervenak mwanaume kutokea Las Vegas, Marekani mwenye umri wa miaka 39 kwa sasa. Mwaka 2016 alisafiri kutokea Las Vegas mpaka Nevada katika ukumbi wa sherehe wa The Little Vegas Chapel ili kufunga ndoa na simu yake ya mkononi(smartphone).

Aaron alisema kuwa alipofika tuu mjini Nevada aliwasiliana na moja ya makanisa yaliyopo mjini hapo ili kuona kama yatakubali kufungisha ndoa yake hiyo isiyo ya kawaida, na alifurahi sana baada ya kuona ilikuwa rahisi kwake kukubaliwa.

Simu yake hiyo aina ya iphone ilionekana ikiwa imevalishwa kava (cover) jeupe na ikasimamishwa kwenye stand ndogo maalumu kwa simu na kuwekwa karibu naye mbele ya kanisa. Kulikuwa na wageni wachache tuu waliohudhuria ndoa hiyo japo baadae uongozi wa kanisa wa jimbo la Nevada ulisema kuwa hawaitambui ndoa hiyo.

Wakati wa ndoa hiyo kanisani hapo mfungishaji alisema kuwa anamtakia Aaron furaha na nyakati nzuri katika ndoa yake hiyo akiwa na simu yake kama mkewe, na baadae akamuuliza mbele ya kanisa kama anaahidi kumheshimu na kumfariji mkewe huyo, Aaron akasema Ndio.

Ulipofika wakati wa kuvishana pete Aaron alichukua simu yake na kuingiza kidole chake ndani ya pete ambayo ilikuwa imeunganishwa na kava (cover) la simu hiyo kumaanisha kuwa simu hiyo ilikuwa imemvisha pete bwana Aaron. Baada ya ndoa Aaron alimbeba mkewe huyo huku akionekana mwenye furaha akitoka kanisani.
20210429_195425.jpg
 
Anaitwa Nadia Matievskaia ni raia wa Minsk, Belarus, anatimiza umri wa miaka 23 mwaka huu, amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na ubunifu wake katika sanaa ya uchoraji. Bibie huyu Ni mchoraji maarufu ambae anachora kwa kutumia Matiti.

Hapo awali hakuwahi kufikiria kama atakuja kuwa mchoraji mkubwa kiasi alichofikia. Ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuwa Mwanamuziki na baadae alikuja kugundua kuwa ana kipaji kingine cha kuchora. Ajabu zaidi hatumii mikono kuchora, anatumia chuchu za matiti yake, anachovya rangi na kuchora .
.
Nadia anasema kuwa hajawahi kuingia darasani kusomea fani hii ya uchoraji, na imekuwa ni kazi inayomuingizia pesa nyingi kwakua anachora picha nyingi kwa namna hiyo na kuziuza kwa watu mbalimbali.
20210429_195531.jpg
 
Hii ni teknolojia ya kuhifadhi miili ya watu waliokufa, inahifadhi mwili kwenye kiwango cha baridi kali sana ili usiweze kuharibika kwa matumaini kwamba ipo siku moja watafufuliwa.

Hatua za kuhifadhi mwili kwa ajili ya kuufufua baadae huanza ndani ya dakika chache baada ya moyo kusimama kwa kuuhifadhi kwenye baridi kali na kutumia kemikali ambazo zinazuia mwili huo kutoharibiwa na barafu. Wataalamu wanaamini mtu anaweza kukaa humo miaka milioni 24 bila kuharibika

Kwa teknolojia iliyopo sasa uwezo wa kuamsha wafu hao bado haupo lakini wataalamu wanaamini miaka ijayo kitu hicho kitawezekana. Wataalamu wa cyronics wanaamini watu waliohifadhiwa watakuja kufufuliwa na teknolojia ya hali ya juu miaka 100 mpaka 500 ijayo kutokana na kukua kwa fani za bioengeneering, nanotechnology na nanomedicine.

Mtu anayehifadhiwa akiwa na miaka 15 baada ya miaka 100 au miaka 200 mbele atakua na umri ulele wa miaka 15 yaani bado kijana.

Wataalamu walioanzisha teknolojia hii wanaamini kwamba kifo ni hatua fulani ya maisha ambayo mtu anapitia kabla ya kufika mwisho wa maisha hivyo hatua hii inaweza kuzuiliwa.

Mpaka mwaka 2014 gharama ya kuhifadhi mwili wa mtu anayehitaji ilikua milion 400 za kitanzania kwa kipindi chote utakachohifadhiwa pamoja na ghrama ya kufufuliwa. Kwa sasa teknolojia hii ipo nchi mbalimbali zilizoendelea kama marekani, urusi,canada, ufaransa na kadhalika.

Dr.james bedford alikua binadamu wa kwanza kuhifadhiwa mwaka 1967 na mpaka mwaka 2014 miili 250 ilikua imehifadhiwa nchini marekani huku zaidi ya watu 1500 wakijiandikisha kuhifadhiwa siku wakifa pia.
20210429_195639.jpg
 
Mwaka 2019 huko Madrid, Hispania kijana mwenye umri wa miaka 26 aliyefahamika kwa jina la Alberto Sánchez Gomez alikamatwa na Polisi kwa kosa la kumuua mama yake mzazi María Soledad Gómez aliyekua na miaka 66.

Uchunguzi wa Polisi ulianza baada ya mama huyo kutoonekana mwezi mzima. Polisi walifika nyumbani kwake kwaajili ya kuchunguza baada ya kupewa taarifa na majirani, walipofika walikuta nyama nyingi chumbani kwa Alberto. Polisi walipofanya uchunguzi waligundua kuwa nyama ile ni ya binadamu.

Baada ya kukamatwa Alberto alikiri kuwa ni kweli alimuuwa mama yake, akamkatakata vipande na kuanza kula nyama akisaidiana na mbwa wake.

Ripoti ya polisi ilisema kuwa Alberto alikuwa mtumiaji mkubwa wa dawa za kulevya.
20210429_195751.jpg
 
Mwaka 1828, Sarah Goodridge ambaye alikua mchoraji, alichora picha ya matiti yake akampa Seneta wa Marekani Daniel Webster ili kumshawishi amuoe.

Kwa kipindi hicho Daniel Webster alikua anatarajiwa kutaka kuoa baada ya kufiwa na mke wake.

Licha ya juhudi za Sarah lakini Daniel Webster alioa mwanamke mwingine.

Familia yake iliitunza picha hio kwa zaidi ya miaka 50 ndipo miaka ya 1980's waliamua kuiuza na kuwekwa kwenye jumba la makumbusho.View attachment 1767660
Asa mbona umefunika machuchu aseeeee?
 
Hahhahaha

Anaitwa Nadia Matievskaia ni raia wa Minsk, Belarus, anatimiza umri wa miaka 23 mwaka huu, amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na ubunifu wake katika sanaa ya uchoraji. Bibie huyu Ni mchoraji maarufu ambae anachora kwa kutumia Matiti.

Hapo awali hakuwahi kufikiria kama atakuja kuwa mchoraji mkubwa kiasi alichofikia. Ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuwa Mwanamuziki na baadae alikuja kugundua kuwa ana kipaji kingine cha kuchora. Ajabu zaidi hatumii mikono kuchora, anatumia chuchu za matiti yake, anachovya rangi na kuchora .
.
Nadia anasema kuwa hajawahi kuingia darasani kusomea fani hii ya uchoraji, na imekuwa ni kazi inayomuingizia pesa nyingi kwakua anachora picha nyingi kwa namna hiyo na kuziuza kwa watu mbalimbali.View attachment 1767908
Khaa... 😅
 
Mwaka 2019 huko Madrid, Hispania kijana mwenye umri wa miaka 26 aliyefahamika kwa jina la Alberto Sánchez Gomez alikamatwa na Polisi kwa kosa la kumuua mama yake mzazi María Soledad Gómez aliyekua na miaka 66.

Uchunguzi wa Polisi ulianza baada ya mama huyo kutoonekana mwezi mzima. Polisi walifika nyumbani kwake kwaajili ya kuchunguza baada ya kupewa taarifa na majirani, walipofika walikuta nyama nyingi chumbani kwa Alberto. Polisi walipofanya uchunguzi waligundua kuwa nyama ile ni ya binadamu.

Baada ya kukamatwa Alberto alikiri kuwa ni kweli alimuuwa mama yake, akamkatakata vipande na kuanza kula nyama akisaidiana na mbwa wake.

Ripoti ya polisi ilisema kuwa Alberto alikuwa mtumiaji mkubwa wa dawa za kulevya.View attachment 1767920
Disgusting...🤮🤮🤮
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom