Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210424_073604.jpg
20210424_073625.jpg
 
Nchini Vietnam Mtu anaejiandaa kuoa lazima ahakikishe kwanza anapeleka kwa Wakwe zake cheti cha Daktari kinachoonesha yupo vizuri kiakili kabla ya kuoa, lengo ni kuwaondoa Wazazi wasiwasi kuwa Mtoto wao anakwenda kwenye mikono salama, Wanawake hushauriwa kupima pia.
20210424_124756.jpg
 
Kama ilivyo kwa Nchi mbalimbali duniani vivyo hivyo kwa ukraine kutazama video au picha za ngono ni kosa la jinai lakini Mtu hatohukumiwa au kupigwa faini iwapo tu alifanya hivyo baada ya kushauriwa na Madaktari kwa ajili ya matibabu, sheria hii ilisainiwa rasmi July 07,2009 na Rais Victor Yushchenko, kikawaida kwa anayekamatwa akitazama video za ngono Nchini humo adhabu ni kifungo cha miaka mitatu au faini ya hadi Pounds 69 (zaidi ya Tsh. laki mbili )
20210424_125046.jpg
 
Katika kuhakikisha Watanzania wanakumbushwa kuchukua tahadhari dhidi ya utabiri wa uwepo wa kimbunga Jobo, Mamlaka ya hali ya hewa ilisema jana kuwa kimbunga hicho leo Jumamosi mchana April 24 kilitarajiwa kuwa umbali wa kilometa 125 Mashariki mwa Mafia.

Taarifa hiyo ilisema pia usiku wa leo ambao ni wa kuamkia Aprili 25, kinatarajiwa kuendelea kupungua nguvu kikiwa katika mwambao wa Pwani ya Tanzania.

Vipindi vya upepo mkali unaofikia kilometa 50 hadi 60 kwa saa, mawimbi makubwa baharini pamoja na ongezeko la mvua kwa maeneo ya ukanda wa Pwani vinatarajiwa kujitokeza.

Maeneo yanayotarajiwa kupata athari za moja kwa moja kutokana na kimbunga Jobo ni Kisiwa cha Mafia, Lindi, Dar es Salaam, Unguja, Mtwara, Tanga na Pemba.
20210424_125200.jpg
 
Mtu mmoja amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na fisi katika Kijiji cha Mikumbi Wilayani Newala Mkoani Mtwara, Taarifa zinasema tukio hili limeongeza hofu kwa Wananchi kutokana na kuwepo kwa makundi ya fisi.

DC wa Newala Aziza Mangosongo, amesema ofisi yake imepokea taarifa hizo na anawasiliana na Wizara husika ili kuweza kutatua changamoto hiyo iliyozua hofu kwa Wananchi wa Vijiji vitano vya Mikumbi, Mkongi, Mdenga, Miyuyu na Chilangala.

“Tembeeni kwa makundi hali sio nzuri fisi wameua Mtu mmoja ila tuendelee na uzalishaji mali, wanaokwenda shambani watembee kuanzia watatu au zaidi na kwa upande wa Wanafunzi pia wasitembee mmojammoja ikibidi Wazazi wawasindikize Shuleni”———DC Newala.
20210424_125326.jpg
20210424_125307.jpg
 
Katika kuhakikisha Watanzania wanakumbushwa kuchukua tahadhari dhidi ya utabiri wa uwepo wa kimbunga Jobo, Mamlaka ya hali ya hewa ilisema jana kuwa kimbunga hicho leo Jumamosi mchana April 24 kilitarajiwa kuwa umbali wa kilometa 125 Mashariki mwa Mafia.

Taarifa hiyo ilisema pia usiku wa leo ambao ni wa kuamkia Aprili 25, kinatarajiwa kuendelea kupungua nguvu kikiwa katika mwambao wa Pwani ya Tanzania.

Vipindi vya upepo mkali unaofikia kilometa 50 hadi 60 kwa saa, mawimbi makubwa baharini pamoja na ongezeko la mvua kwa maeneo ya ukanda wa Pwani vinatarajiwa kujitokeza.

Maeneo yanayotarajiwa kupata athari za moja kwa moja kutokana na kimbunga Jobo ni Kisiwa cha Mafia, Lindi, Dar es Salaam, Unguja, Mtwara, Tanga na Pemba. View attachment 1762387
Na kuna binadamu washaanda usiku wa Jobo ni kwenda kujirusha tuu...

😅😅
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom