Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan kyobya amewataka Wananchi wa Mtwara kuchukua tahadhari kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa juu ya Kimbunga Jobo ambacho kimeendelea kuimarika na kusogea kuja uelekeo wa maeneo ya Tanzania hususani maeneo ya Lindi na Mtwara.

“Tumeambiwa kutakuwa na mvua na upepo mkali kwahiyo tuendelee kuchukua tahadhari, niwatoe wasiwasi tuendelee na majukumu kama kawaida, tutaendelea kutoa tahadhari na kukiwa na tahadhari ambayo imekithiri basi tutawaelezea nini cha kufanya”———DC Kyobya
20210423_140558.jpg
 
“EWURA wanatakiwa kutoka na kutoa Elimu ili Mwananchi na kila Mtumiaji wa maji ajue haki zake na sio tu kumkatia maji bila yeye kupewa taarifa, Mwananchi anatakiwa kusikilizwa”———Waziri wa Maji, Jumaa Aweso

“Kama Mwananchi amekatiwa maji, baadae akalipa, anatakiwa kurudishiwa maji ndani ya saa 24, lakini kumekuwa na ucheleweshaji, sasa EWURA wanatakiwa kutimiza wajibu wao kuhakikisha hili linasimamiwa na kufanyika"———AWESO
20210423_140826.jpg
 
“Tumeanzisha Timu inaitwa ‘Samia Suluhu Rescue Team’, lengo na kazi kubwa ya Timu hii ni ya kutatua matatizo ya maji Nchi nzima, na tumeweka Watalaamu wa Kada zote, kuanzia Wahandisi, Wataalamu wa Manunuzi, Wanasheria na wengineo”———Waziri wa Maji, Jumaa Aweso

“Sasa ikitokea tatizo limeshindikana kwa Wataalamu wote waliopo hadi lisubiri kuja kutatuliwa na Waziri basi Mimi nitakufa nao, ninamhakikishia Mh. Rais hakuna jambo litakaloshindikana”———AWESO
20210423_140952.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom