Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza kifo cha Mama Mzazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simoni Sirro Monica Tongori Nyabyamari kilichotokea usiku wa kuamkia leo April 10,2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es saalam alikokuwa akitibiwa.

Msiba upo nyumbani kwa IGP Sirro Masaki, Dar es Saalam karibu na kwa Hayati Benjamini Mkapa na ratiba ya mazishi itatolewa baadaye.
20210410_153652.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo April 10, 2021 atakutana na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Muigai Kenyatta, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
20210410_153716.jpg
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amempongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuunga mkono na kupenda michezo ambapo amekuwa akitoa wito kwa Watanzania kupenda kufanya mazoezi ya viungo na kutoa maelekezo kuwa kila Jumamosi ya pili ya Mwezi iwe siku ya kuhamasisha kufanya mazoezi ya viungo kote nchini, Bashungwa amesema Wizara yake itaendelea kusimamia maelekezo hayo.

Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo baada ya kumaliza mazoezi na mbio za taratibu (jogging) katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma ( Muungano na Dodoma Fitness) Leo April 10, 2021.

“Natoa wito kwa Ma-RAS na Ma-DAS ambao ni Wenyeviti wa Michezo katika Mikoa na Wilaya nchini kuendelea kusimamia maelekezo hayo yaliyotolewa Rais Samia Suluhu Hasssan, moja ya faida kubwa ya mazoezi ni kuimarisha afya ya mwili na hivyo kusaidia kuepuka magonjwa na kupunguza gharama za matibabu”———BASHUNGWA

Kwenye matukio ya picha ni Waziri Bashungwa akinywa uji pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, Innocent Bilakwate (kushoto) na Brown Focus kijana kutoka Karagwe ambaye aliwahi kucheza Timu ya Kagera Sugar kwenye timu ya vijana chini ya miaka 20, muda mfupi baada ya kumaliza jogging.
20210410_153838.jpg
20210410_153856.jpg
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha.

Waziri Dr.Ndumbaro ametoa maamuzi hayo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema uchunguzi huo hauhusiani na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

"Nafasi ya Mdachi itakaimiwa na Betrita James ambaye ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi TANAPA, hatuwezi kumchunguza Mtu akiwa kakalia kiti hichohicho”———NDUMBARO
20210410_153931.jpg
 
Rais Samia Suluhu leo amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta uliowasilishwa na Waziri wa Michezo, Utamaduni na Urithi wa Kenya, Balozi Dkt. Amina Mohamed.

Pamoja na kupokea ujumbe huo Ikulu Dar es saalam, Rais Samia amefanya mazungumzo na Balozi Amina kuhusiana na dhamira ya Tanzania na Kenya kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali hususani kiuchumi na kijamii.

Rais Samia amemuhakikishia Rais Kenyatta kuwa Serikali anayoiongoza ipo tayari kuendeleza mambo mazuri yote yaliyokuwa yakifanywa na Hayati Dr. John Pombe Magufuli na kutatua changamoto kati ya Tanzania na Kenya kwakuwa Nchi hizi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni Ndugu, Majirani na Marafiki wa Kihistoria.

Rais Samia amewataka Mawaziri na Wataalamu wa Tanzania na Kenya wanaounda Kamati ya Ushirikiano wa Pamoja (JPC) ambao hawajakutana tangu mwaka 2016 kukutana mara moja ili kufanyia kazi masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano.
20210410_155830.jpg
 
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amemwalika Rais Samia kufanya ziara rasmi nchini Kenya ili kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na Kenya.

Rais Kenyatta amemuhakikishia Rais Samia kuwa Kenya ipo tayari wakati wote kushirikiana na Tanzania kwa kuendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya Nchi hizi mbili.

Rais Samia Suluhu Hassan amepokea mwaliko huo kupitia kwa Waziri wa Michezo, Utamaduni na Urithi Kenya, Dkt. Amina Mohammed, ambaye ni Mjumbe Maalumu wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliyefika leo April 10, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, Dkt. Amina ameongozana na Balozi wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu.
20210410_155902.jpg
20210410_155927.jpg
20210410_155949.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo ametembelea ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Mwl. Nyerere (JNHPP) kwenye Bonde la Mto Rufiji na kufurahishwa na kasi ya ujenzi huo huku akitaka Wananchi wanaozunguka maeneo hayo wakiwemo Madiwani wapelekwe kwenye eneo hilo ili waachane na maneno ya Watu wanaopotosha kuhusu ujenzi wake.

“Kuna wengine wanaweza kuwasikiliza wale wasiopenda maendeleo kwa upotoshaji kwamba ujenzi hauendi vizuri, hauwezi kukamilika, hauna maslahi, waleteni waone Serikali ilivyodhamiria na wajue ni vipi watafaidika, waleteni wachache wawe Mabalozi kwa Watanzania wengine"———Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
20210410_175837.jpg
20210410_175901.jpg
20210410_175950.jpg
20210410_180014.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom