Makapuku Forum

Makapuku Forum

“Mh. Naibu Spika, unapowaelezea Watanzania kwamba uchumi ni wakati au ni uchumi mzuri unamaana gani? kwasababu Watanzania wetu hawa tunaowaita wanyonge na hili neno wanyonge mimi linaniudhi sana kwasababu tunataka kuwaambia Watanzania waukubali unyonge na umasikini yaani waubebe na mbeleko kabisa mgongoni”———Konchesta Rwamulaza, Mbunge viti maalum

“Watanzania sio wanyonge, wakielekezwa wanaweza kufanya kazi yao vizuri na Nchi yetu ikapata maendeleo kwahiyo haya mambo ya kuitwa Watanzania wanyonge inanikera sana ”———Rwamulaza
20210409_202404.jpg
 
Rapper maarufu wa Marekani DMX amefariki leo Hospitalini New York, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kwamba Rapper huyo amefariki leo akiwa na umri wa miaka 50, aliwaishwa Hospitali wiki iliyopita baada ya kuripotiwa kuzidisha matumizi ya dawa za kulevya. RIPDMX
20210409_202528.jpg
 
Kufuatia maelekezo aliyoyatoa Rais Samia Suluhu Hassan yanayohusu Tasnia ya Habari Tanzania, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amekutana na Mmiliki wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea.

Kubenea amefika Ofisini kwa Waziri leo April 9, 2021 baada ya mapema wiki hii Bashungwa kutoa fursa kwa Wamiliki wa Magazeti yaliyofungiwa kufika Ofisini kwake kwa majadiliano zaidi.

Waziri Bashungwa ametoa wito kwa Wadau wa Tasnia ya Habari kuunga mkono dhamira ya Rais Mama Samia kuona haki ya uhuru wa habari inaendana na wajibu na uzingatiaji sheria, kanuni na misingi ya Taaluma ya Habari.
20210409_202628.jpg
 
TotalCAFChampions League KUNDI B

FT | Mamelodi Sundowns 0-2 CR Belouizdad
️ Amir Sayoud 29’
️ Amhed Gasmi 45’

FT | TP Mazembe 2-1 Al Hilal Club
️ Mohamed Ouattara 18 [OG]
️ Isaac Tshibangu 76’

️ Eid Mugadam 2’

CR Belouizdad imeungana na Mamelodi Sundown kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
20210409_202813.jpg
 
Kwa kutambua mchango wake ndani ya Simba, Mwenyekiti wa Bodi, Mohammed Dewji (moodewji) amemchagua Prof. Philemon Sarungi kuwa mshindi Tuzo ya Heshima (Lifetime Achievement) ambayo itatolewa kwenye hafla ya Tuzo za Mo Simba 2021 ambazo zitafanyika mwishoni mwa msimu.

Mzee Sarungi aliwahi kuwa mlezi wa klabu na mmoja wa wapenzi wakubwa wa Simba ambaye wakati yuko Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikuwa anawasaidia sana wachezaji wetu kwenye matibabu na hasa wakati George Masatu alipoumia alipokuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.
20210409_203529.jpg
 
Rapper maarufu wa Marekani DMX amefariki leo Hospitalini New York, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kwamba Rapper huyo amefariki leo akiwa na umri wa miaka 50, aliwaishwa Hospitali wiki iliyopita baada ya kuripotiwa kuzidisha matumizi ya dawa za kulevya. RIPDMXView attachment 1747795
One of my favourite rapper...

Rest in peace, rest in power...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom