Makapuku Forum

Makapuku Forum

Beki wa Azam FC Agrey Morris baada ya kutangazwa kuwa January 12 2021 ndio atastaafu kuichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa kwa kuagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki wa Taifa Stars dhidi ya Congo DR uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

AyoTV akiwa visiwani Zanzibar walitaka kufahamu Morris baada ya kutangaza kustaafu timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 36 kwa ngazi ya club atacheza hadi lini?

“Huu ni muda sahihi wa mimi kustaafu kama mimi niliachiwa kijiti na Kusi na mimi umefika muda wa kuachia vijana nafasi, umri wangu sasa hivi umesogea na vijana wanakuja kwa kasi ukiangalia kuna Sebo, Ame na Mwamnyeto kwa hiyo huu ni muda wangu sahihi kwa Azam FC nitastaafu 2022 nikimaliza mkataba wangu huu wa miaka miwili”>>> Agrey Morris

Morris ameeleza hayo na kusema kuwa amejitathmini na kuona huu ni muda sahihi kwake hakutaka acheze akiwa na heshima yake hadi kiwango kishuke watu waanze kumzomea
20210111_184611.jpg
 
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameiita hatua ya watu kukwepa kupata chanjo ya Covid-19 ni mauaji ya kujitakia akisema wale wanaokataa chanjo hiyo wanacheza na afya zao na pia maisha ya watu wengine.

Kiongozi huyo Mkuu wa kidini kwa upande mwingine amethibitisha kwamba binafsi yeye atapa chanjo hiyo mwanzoni mwa wiki ijayo huku akiwaita watu wanaopinga chanjo hiyo kuwa wenye kupingana na kifo.

Akizungumza na shirika la habari la Italia ametoa mwito kwa watu kujitokeza kupata chanjo hiyo akisema kwamba anaamini kimaadili kila mmoja anapaswa kupata chanjo.
20210111_184624.jpg
 
.....duh, umri unakimbia sana aunt. Imebidi nimgoogle kumbe kijana yuko vizuri kabisa




... Lee una vpn niendelee kushusha mamiziki ujisahaulishe na machungu uliyopewa na mwalimu mkuu kwenye mambo ya ada ha hahahaha hahahha
Anko mm kwenye ada unajua kabisa hedimasta ni mwenyekiti wa upatu hivo atachukua mzunguko wangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom