Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema ni marufuku kwa Nchi yake kupokea chanjo ya Corona kutoka Marekani na Ulaya, huku akisema kama kutakuwa na ulazima wataagiza chanjo kutoka Mataifa mengine.

“Marekani na Nchi za Ulaya hasa Uingereza hawaaminiki kabisa, wanaweza kuleta chanjo kumbe ndio zikawa zinaeneza maambukizi zaidi” - Ayatollah

“Hata Ufaransa hatutaki chanjo zao miaka ya 1980 na 1990 waliwahi kuwa na skendo ya kusambaza damu yenye virusi vya UKIMWI” - Ayatollah
20210109_112014.jpg
 
Meya wa Jiji la Mwanza Costantine Sima ametoa saa 24 kwa Mfanyabiashara Sajady Ahmed kuvunja jengo alilolijenga bila kutafa taratibu za ujenzi wa mipango miji unaotaka maeneo ya katikati ya Jiji kujengwa majengo ya ghorofa na sio mafupi kama alivyofanya yeye>> “Serikali haijalala kiasi hicho, kibali kilitoka Jiji kuzuia ujenzi lakini umekiuka sharti, nimeagiza jengo livunjwe ndani ya saa 24 na gharama za uvunjaji ziwe juu yako”
20210109_113457.jpg
 
Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kuwa hatohudhuria kwenye sherehe za kuapishwa kwa Joe Biden kuwa Rais Mpya wa Marekani, Joe Biden amesema ni jambo zuri kwa Trump kutofika maana huenda anaweza kuharibu shughuli kama atakuwepo.

Marais watatu Wastaafu wa Marekani Barack Obama, George Bush na Bill Clinton wote kwa pamoja wamethibitisha kuwa watashiriki kwenye zoezi hilo la kuapishwa kwa Joe Biden.

Trump atakuwa Rais wa kwanza tangu Andrew Johnson 1869, kugoma kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais anayemkabidhi kijiti.
20210109_113915.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom