Makapuku Forum

Makapuku Forum

FB_IMG_1610124455719.jpg
 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI David Silinde amemkabidhi Mwalimu Mkuu wa Ikhanoda Secondary, Wilayani Singida, Omary Selestine kwa Polisi na TAKUKURU baada ya kugundua matumizi mabaya ya fedha za umma katika ujenzi wa bwalo la chakula la wanafunzi wa shule hiyo.

Hayo yamejiri baada ya Silinde kufanya ziara katika shule hiyo kukagua mradi wa lipa kutokana na matokeo ambao shule hiyo walipewa kwa ajili ya ujenzi wa bwalo lakini mpaka sasa fedha zaidi ya milion 50 zimetumika huku ujenzi ukiwa katika hatua ya msingi.

"Huwezi nunua bati za milioni 70 unataka kujenga nini?, au unanunua tofali kwa Tsh. Elfu 5 ni tofali aina gani?, mchukueni huyu mwalimu na kamati nzima ya ujenzi wakaeleze wametumiaje fedha za ujenzi wa mradi huu”-Silinde

Silinde pia amemsimamisha kazi Mwalimu Mkuu huyo na kuvunja kamati ya ujenzi ya shule hiyo na kumvua madaraka Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo baada ya kushindwa kusimamia ujenzi wa bwalo la chakula katika shule hiyo.View attachment 1672371
Upigaji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom