Makapuku Forum

Makapuku Forum

Hahhahaha jiwe bwana
Screenshot_20181215-064524.jpeg

"Hata mimi tangu nasoma shule hadi leo nafahamu kuwa Bendera ya Taifa ina rangi ya njano, na sio rangi ya dhahabu. Rangi hiyo ya njano inawakilisha madini yote. Nimeamua kufuta barua ya Wizara ya Elimu, na kama kuna mabadiliko, yafanyike kuzingatia taratibu zote, kwa kuwa jambo hili ni la kitaifa na sio la mtu mmoja."- Rais Dkt Magufuli
 
Mshambulizi wa klabu ya Liverpool ya Uingereza na Misri Mohammed Salah ndiye mshindi wa tuzo ya mwanakandanda bora wa BBC mwaka huu AFOTY2018.

Bingwa huyo wa tuzo ya mwaka uliopita alipigiwa kura na mashabiki wake kote barani Afrika na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo hili mara mbili tangu mwaka wa 2004 Jay Jay Okocha alipotetea taji lake.
Screenshot_20181215-064833.jpeg
 
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango amesema nchi inapita kwenye kipindi kigumu kidogo kutokana na wafadhili kupunguza kutoa misaada. Kufuatia hali hiyo, amewataka wanaokusanya mapato kuhakikisha wanasimamia kwa nguvu zote zoezi hilo.

Chanzo: Nipashe
Screenshot_20181215-064957.jpeg
 
BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imepewa jukumu la kulipa fidia kwa waliokuwa wateja wa benki tano zilizofungiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Richard Malisa aliyasema hayo jana alipokuwa akiwasilisha mada ya Bodi ya Bima ya Amana na Ufilisi wa Mabenki na Taasisi za fedha: Mafanikio na Changamoto, wakati wa warsha ya waandishi wa habari za uchumi na biashara jijini Dodoma.

Alisema TPB imepewa jukumu hilo tangu mwezi Oktoba mwaka huu, ikiwa ni hatua ya kurahisisha ulipwaji wa fidia hizo zinazotolewa na Bodi ya Bima ya Amana , ambapo benki hiyo ina matawi mengi nchini yatakayorahisisha kuwafikia walengwa.

Kwa muujibu wa Malisa, benki zilizofungiwa mwaka huu ni tano, ambazo ni Meru Community Bank, Njombe Community Bank, Kagera Farmers’ Cooperative Bank, Efatha Bank Limited pamoja na Covenant Bank for women Tanzania Ltd.
Screenshot_20181215-065546.jpeg
 
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ametoa siku saba kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kumpa taarifa juu ya maendeleo ya mradi wa Stendi ya Mabasi ya Mbezi- Luis, kinyume na hapo, TZS bilioni 50.9 zilizotengwa kwa ajili ya mradi huo, zitapelekwa katika halmashauri nyingine.
Screenshot_20181215-065653.jpeg
 
hapoo sawaa na mm nilianzaa kukosaa iman na mwl wangu wa primary
Hahhahaha jiwe bwana View attachment 968484

"Hata mimi tangu nasoma shule hadi leo nafahamu kuwa Bendera ya Taifa ina rangi ya njano, na sio rangi ya dhahabu. Rangi hiyo ya njano inawakilisha madini yote. Nimeamua kufuta barua ya Wizara ya Elimu, na kama kuna mabadiliko, yafanyike kuzingatia taratibu zote, kwa kuwa jambo hili ni la kitaifa na sio la mtu mmoja."- Rais Dkt Magufuli
 
Anafaaaa
Mshambulizi wa klabu ya Liverpool ya Uingereza na Misri Mohammed Salah ndiye mshindi wa tuzo ya mwanakandanda bora wa BBC mwaka huu AFOTY2018.

Bingwa huyo wa tuzo ya mwaka uliopita alipigiwa kura na mashabiki wake kote barani Afrika na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo hili mara mbili tangu mwaka wa 2004 Jay Jay Okocha alipotetea taji lake.
View attachment 968487
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom