Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,121
- 1,249,294
Matatizo yanayosababishwa na msongo wa mawazo huwa ni makubwa sana na athari zake huwa ni maamuzi magumu kwa muathirika. Mazoea ya kitu au hali ndio humpelekea mtu kutokukubali matokeo ya kile alichokizoea pindi kinapokuwa kimekwenda kombo. Kawaida ya akili zetu upenda na utamani kudumu na hali moja tu kila siku. Sasa inapotokea hali tofauti na ile iliyozoeleka na akili ndio pale mtu anapochukuwa maamuzi mazito hata ya kujitoa uhai wake. Msongo wa mawazo umesababisha vifo vya watu wengi sana duniani masikini na matajiri. Wapo waliojiuwa kwa aina tofauti tofauti ya mauwaji kwasababu ya msongo wa mawazo. Lakini ifahamike kuwa hakuna dawa hospitalini unayoweza kupewa ili kudhibiti au kuondoa kabisa mawazo akilini hilo halipo. Tiba ya masongo wa mawazo ni kuleta mawazo chanya kinyume na yale yanayokutatiza. Tatizo sio kuwaza bali tatizo unachokiwaza ni nini na kinapokelewa vipi na akili yako. Ukihisi kuna kitu kinakutatiza akilini mwako kamwe husikubali ukitolee maamuzi kwa haraka wala ukiamue ukiwa na mawazo yako tu binafsi, jitahidi uwashirikishe na wengine ili yale mawazo yao yaweze kukusaidia pia kwenye maamuzi yako. Kwasababu unapowaza wewe binafsi na ukatoa maamuzi wewe binafsi kuna hatari kubwa ya kutoa maamuzi ya makosa na yenye madhara, kwasababu wakati huo unaowaza akili yako nayo inamsukumo wa hasira na mfadhahiko kwa jambo lilokufika. Sasa lazima umtafute mtu mwengine ambae yeye yupo kwenye hali nyengine ndio akushauri kuhusu jambo lako, hapo unaweza kuamua kwa busara na faida. Jiepushe kutoa maamuzi ya kitu ukiwa na hasira sana na wala usije hata siku moja ukatoa maamuzi ya kitu ukiwa na furaha sana. Hivi sio vipindi vizuri kwa maamuzu bora. TAFAKARI KWA KINA Habari ngumu kuilainisha kwake ni kuikubali kuwa ni ngumu






