Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,117
- 1,249,280
Mfano kama atatokea mtu muda huu na akauuliza swali hili "Je ni kitu gani tukikupa utakuwa na furah?" Naimani majibu yatukuwa mengi sana kuna wengine watasema "Ukinipa pesa nitafurahi", na kunawengine watasema "Ukinipa nyumba na magari nitafurahi", majibu yatakuwa mengi sana. Ila ukweli utabaki kuwa pale pale kuwa furaha ya moyo haitegemei nyumba wala pesa. Furaha ya moyo inategemea sana moyo wenyewe ulivyouzoesha na namna unavyoyapokea mambo katika maisha. Mfano nitakupa kuna watu wakifikwa na matatizo huwa hawawezi kabisa kufikiria utatuzi wa tatizo kwa haraka. Yani wao wakifikwa na tatizo kazi yao kubwa ni kulia na kulaumu watu waliowasababishia matatizo. Sasa kanuni za furaha zinalikataa hilo jambo kwa kiasi kikubwa sana, na zinaeleza kulipokea tatizo kwa mfumo huo ni kuongeza tatizo jengine. Siku zote ili uweze kurudisha furaha nafsini baada ya nafsi kuchafuka kwa jambo lililokusibu, unatakiwa kwanza usilikuze tatizo akilini mwako na kuliona kubwa sana. Yani kama hivi pengine umefukuzwa kazi kazini kwa kosa ambalo si haki wewe kufukuzwa kazi. Unachotakiwa kukifanya ni kulipokea tatizo kwa njia ya busara bila hamaki na hapo hapo uwanze kutafakari je nitarudi vipi kazini kwa kutaka ushauri kwa baadhi ya watu wako wa karibu. Kitendo hichi kitakupa uhuru na fikra mbadala zenye kujenga pia kitakusukuma kufanya maamuzi sahihi. Kwahiyo kikubwa tunachotakiwa kuwa nacho ninamna ya kuyapokea mambo na jinsi ya kuyatatua, hapa viwango vya furaha havitopungua ndani ya mioyo yetu. TAFAKARI KWA KINA Furaha ni chimbuko la namna unavyo yapokea mambo