Jack Chan kwa asilimia kubwa kila sehemu ya mwili amewahi kuumia. Lakini Jeraha kubwa ni katika Kichwa chake ambapo mpaka sasa kawekewa Chuma (Plastic).
-
Hapo alikuwa akisimulia namna Alivyopata Ajali hiyo, Anasema Walikua wakishuti Filamu Ya 'Armour Of God', Kuna Scene ambayo alitakiwa arukie Adake Tawi la Mti.
-
Aliporukia, Lile Tawi Lilikatika...Hapo Anaelezea Alijitahidi Kudaka Matawi Mengine Lakini Yote Yakawa Yanakatika.
-
Sasa Anasema Hapo Chini Kulikua Na Camera Man Ameshika Camera Akichukua Tukio Hilo Akiwa Kaibenua Camera Juu, Ambapo Kama Angempush Kidogo Jack Basi Angeanguka Katika Hali nzuri...Lakini Jamaa Alipoona Mtu Mzima Anashuka Akabeba Camera Yake Afu Huyooo Mwendoo Akachanganya Miguu
-
Anasema Kilichomsaidia Kutokana Na Stamina Yake, Kwa Namna Alivyoanguka Ni Kama Alijipooza Sababu Ulitangalia Mkono Then Kichwa...Kwahiyo Mkono Ulikuwa Kama Sponji, Ulipunguza Nguvu Ya Muanguko...Kama Angetangulia Kichwa, Huenda Tusingekuwa Nae.
-
Namna Anavyoelekeza, Si Unajua Ukiwa Unaongea Lugha Ambayo Haupo Comfortable, Vitendo Ni Vingi Kuliko Maneno .