Makapuku Forum

Makapuku Forum

Katika juhudi za kutaka kufahamu kipi kinauwezo kati ya ubongo wa binadamu na kompyuta, watafiti kutoka Japani walifanya jaribio hilo kupitia moja kati ya kompyuta zenye nguvu zaidi Duniani, ili kulinganisha na uwezo wa ubongo wa binadamu -

kompyuta hiyo ilikuwa na processor 705,024, RAM GB milioni 1.4, kitu kilichotokea licha ya ukubwa huo wa hiyo kompyuta ilichukua dakika 40 kufanya kazi ambayo kwenye ubongo wa binadamu ingefanywa kwa sekunde moja.
Screenshot_20181105-174302.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Steve Jobs alianza kupenda kompyuta akiwa na umri wa miaka 12 baada ya kuoneshwa moja na Larry Lang, injinia aliyekuwa anafanya kazi kampuni ya Hp.

Steve Jobs alijikuta ghafla anapenda kompyuta na alinukuliwa akisema "nilidhani kompyuta ni nadhifu. Nataka moja nianze kuichezea
Screenshot_20181105-174433.jpeg
 
Hivi ndivyo jinsi Dunia yetu inavyoonekana baada ya kupigwa picha na Parker Solar Probe, chombo ambacho kwa sasa kinaelekea kwenye Jua.

Hicho kidoti cheupe kinachong'aa ni Dunia yetu, picha hii ilipigwa umbali wa maili milioni 27 kutoka Duniani na kamera zilizofungwa kwenye Parker Solar Probe wakati chombo hicho kilipogeuzwa kuangalia kilipotokea wakati kikiwa kinaelekea kwenye Jua.

Parker Solar Probe chombo chenye thamani ya dola bilioni 1.5 (takribani trilioni 3.4) kitaenda kulichunguza Jua kwa undani zaidi na kutupatia majibu ya jinsi Jua linavyofanya kazi na linavyosaidia sisi kuweza kuishi huku Duniani. Chombo hicho kitatumia miaka 7 na hakitarajiwi kurudi tena Dunia.
Screenshot_20181105-174622.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Umoja wa Ulaya unasema umemuita mjumbe wake nchini Tanzania Balozi Roeland van de Geer, kwa mashauriano pamoja na kutathmini upya uhusiano wake na nchi hiyo kutokana na kuongezeka kwa ukiukaji wa haki za binaadamu Tanzania.
Screenshot_20181105-174923.jpeg
 
Nilikumiss pia jamanii....saizi nimerudi ila kwa kunyapianyapia, niko kulea!
Hahhahah we mwanamke nimekumiss sana magazeti yapo panda juu utakutana nayo ya asubuhi

Ebu kwanza umejiiba kurudi au umeruhusiwa kurudi mazima
 
"Ninakiweka kifaa changu cha kusisimua kwenye kitanda changu na huwa ninakitumia kila siku!! .

Kiukweli ninahisi kama nimepiga hatua mpya katika kujamiiana", Leanne alisema. Je kifaa cha kujisisimua kinaweza kukuzuia kufurahia mapenzi?

Hahhaha acha dyudyu iheshimiwe napenda dyudyu mie shikamoo dyudyuuuuu
Screenshot_20181105-175059.jpeg
 
Vikwazo vikali zaidi vya Marekani dhidi ya Iran vimeanza kutekelezwa Jumatatu tarehe 5: 11: 2018.

Rais Donald Trump alirejesha vikwazo vyote vilivyotolewa baada ya makubaliano ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa na Ulaya Urusi na China.

Vikwazo hivyo vinalenga mauzo ya mafuta, usafiri kwa njia ya baharini na mabenki ambavyo vyote ni muhimu sana kwa uchumi.

Jeshi la Iran nalo limesema kuwa litafanya mazoezi ya kijeshi leo Jumatatu na Jumanne kuonyesha uwezo wake wa kijeshi.
Screenshot_20181105-175240.jpeg
 
Jeshi la Uingereza litaanza kuwasajili makurutu kutoka Kenya Australia Fiji Sri Lanka ilikujaza upungufu wa takriban wanajeshi 8,200.

Hii ni baada ya wizara ya ulinzi kufanya mabadiliko ya sheria ilikuruhusu watu kutoka kwenye jumuiya ya madola kujiunga
Screenshot_20181105-175405.jpeg
 
Uganda itakuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kutoa chanjo ya ugonjwa wa Ebola bila ya kuwa maambukizi ya ugonjwa huo ndani ya mipaka yake .

Wizara ya afya ikiwemo shirika la afya ulimwenguni WHO limeunga mkono hatua hiyo kutokana na sababu ya tishio la kusambaa kwa ugonjwa huo kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hasa upande wa Mashariki ulipo mji wa Beni.
Screenshot_20181105-175551.jpeg
 
Dada watatu wa Nigeria walioshika mimba wakati mmoja Marekani wamevutia maelfu ya watu mitandaoni baada ya kuchapisha picha zao wakiwa pamoja.

Watatu hao, Chika Okafor, Onyeka Ufere na Ogechi Babalola walizaliwa Nigeria ingawa kwa sasa wanaishi Marekani, waligundua kuwa walikuwa wajawazito wakati mmoja.

Wameambia BBC kwamba hawakufahamu jinsi kisa chao kilivyokuwa cha kipekee.
Wote wameolewa, na wanatarajia kujifungua watoto wao wakiwa wameachana kwa wiki kadha tu.
Screenshot_20181105-175654.jpeg
 
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia Kamati ya Maadili limemfungia kutojihusisha na soka maisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu ya kimaadili.

Makosa matatu ambayo yamemtia hatiani Wakili Kuuli ni kusambaza nyaraka za shirikisho kinyume na kanuni na taratibu, kutoa maelezo yanayoonesha kuwa na mgongano wa kimaslahi kwa kuwapa watu wasiohusika na pia kufanya vitendo vinavyoshusha hadhi ya shirikisho.
Screenshot_20181105-180329.jpeg
 
Wananchi wameishauri serikali kutoikubali teknolojia ya uhandisijini wa mazao (GMO), kutokana na athari zake kwa mimea asilia na wanyama, lakini pia kuleta utegemezi kwa sababu mbegu za GMO hazirudiwi kupandwa zikatoa mazao. Kwa sasa serikali inafanyia majaribio mbegu hizo.
Screenshot_20181105-180456.jpeg
 
Kwa mujibu wa utafiti wa TDHS 2015/16, wastani wa mwanamke mmoja mjamzito hufariki kila baada ya saa moja nchini#Tanzania ambapo ni sawa na vifo 916 kwa mwezi. Novemba 6 mwaka huu, Makamu wa Rais, Samia Suluhu atazindua kampeni iliyopewa jina 'Jiongeze Tuwavushe Salama' ili kupunguza vifo vya wajawazito nchini.
Screenshot_20181105-180631.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom