Utafiti uliofanywa nchini Marekani umegundua kuna aina kadhaa za kucha zenye muonekano mbalimbali ambapo kila muonekano unatabiri upungufu au ongezeko la kitu fulani katika mwili wa binadamu.
Aina ya Kwanza ni kucha zenye vidoti vidoti vyeupe, utafiti umebainisha kuwa mtu mwenye kucha zenye muonekano huu ana upungufu wa madini mwilini aina ya Calcium na Zinki, lakini pia vidoti huashiria ugonjwa wa Alegy, ugonjwa huu hutokea pale ambapo mwili kutokupatana na baadhi ya vitu au chakula matokeo yake ukikutana na vitu hivyo mwili humwaga sumu ambayo hudhuru eneo fulani la mwili lililokutana na kitu hiko ambapo wengine huwashwa na kuvimba, wengine hutoka vipele huku wengine hutokwa na vidonga au majipu kila mtu ana namna yake ambayo anaweza kudhurika na vitu ambavyo havipatani na mwili wake.