Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,374
- 38,248
Tuzidishe busara zetu katika Matumizi ya Maji!
Makadirio ni kwamba 71% ya dunia imejaa MaJI, na yapata 95% ya Maji ya dunia ni Maji ya Bahari.
Makadirio ni kwamba 71% ya dunia imejaa MaJI, na yapata 95% ya Maji ya dunia ni Maji ya Bahari.
- Watu 780 million Duniani kote wanaishi pasi na maji safi ya kunywa!
- Barani Afrika Zaidi ya theluthi moja ya watu hawana huduma ya Maji safi na salama!
- Kati ya 25-33% ya Wachina hawapati Maji safi na salama!
- Magonjwa yanayosababishwa na Ukosefu wa Maji safi na salama Duniani yanaua watoto wa wa umri wa chini ya miaka mi5 kuliko maradhi kama Malaria na HIV kwa pamoja.
- Kwa wastani, barani Afrika Mwanamke hutembea 3.7 km kusaka Maji kwa ajili ya familia!
- Mmarekani wa kawaida anatumia dk 5 za kujimwagia Maji bafuni, hiki ni kiasi kikubwa Zaidi cha Maji kuliko Kiasi ambacho Mtu wa kawaida anatumia katika Nchi zinazoendelea hasa za afrika.
- Zaidi ya watu 130 million wa Latin America hawapati huduma ya maji safi na salama ya kunywa!
- Akiba ya Maji nchini Marekani katika Lake Mead inatarajiwa kuishiwa ifikapo 2021, kama hili litatokea, watu 22 million watahitaji chanzo kipya cha Maji!
- Pia 97.5% ya Maji ya dunia, ni ya Chumvi!
- Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, maradhi ya kuhara yameua watoto wengi Zaidi kuliko wale waliokufa katika vita vyote vilivyotokea baada ya vita ya dunia ya 2!
- Watu wapatao 27% wanaoishi miji mikubwa duniani hawana maji ya bomba majumbani!
- Katika harakati za Kutafuta Maji, wanawake wamejiweka katika hatari kubwa ya kukumbana na manyanyaso ya kingono!
- Barani AAfrika, katika kila $1 inayotumika katika kusaidia upatikanaji wa Maji, inaokoa muda wenye thamani ya $9!
- Katika Sub-Saharan Africa, asilimia 72 ya Maji yanayotumika Majumbani ni matokeo ya juhudi za Mwanamke!
- Zaidi ya nusu ya shule za Msingi katika Nchi zinazoendelea, hazina mifumo sahihi ya upatikanaji wa Maji!
- Watu wa “uswazi” katika maeneo yote ya dunia, wanatumia mara 5-10 ya Gharama za kupata Maji kuliko watu wenye nazo!
- India ina Asilimia 16 ya watu wote wa Dunia hii, Cha kushangaza India ina 4% ya Maji safi!
- Pamoja na tatizo kubwa la Maji, Afrika ina MAZIWA yapatayo 677! Afrika ina mito mikubwa 67!
- Nchini Afrika Kusini, watu kati ya 12-14 million hawana huduma ya maji safi na salama!
- Statistics South Africa katika report ya Mwaka 2016 inasomeka kuwa kaya 88.8% katika Afrika Kusini yote wamefikiwa na Maji ya Bomba Majumbani!

101-03-821.M|T|C


