Makapuku Forum

Makapuku Forum

TUOMBE:

Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa Majeshi nakushukuru sana kwa siku ya leo Jumanne Tarehe 24 Julai 2018 Asante kwa Upendo na Huruma isiyo na mwisho kwetu wako wengi walitamani kuiona siku ya leo hawajaweza Mfalme wa Amani.

Tunaomba Toba kwa yote tunayokosa kwa mawazo,maneno, matendo na kutotimiza wajibu mbalimbali uturehemu twakusihi.
Endelea kutupigania Baba Endelea kutupa haja za moyo yetu sawasawa na mapenzi yako.

Navunja hila zote za shetani zinazodhoofisha kazi ya Mungu ambayo umeianza ndani yetu.
Baba Asante kwa uponyaji kwa wagonjwa wote endelea kuwaimarisha miili na roho na uwape tumaini la kudumu.Roho Mtakatifu tunakuomba kaa nasi utuongoze.

Tunakabidhi kazi za mikono yetu Bariki mashamba,kazi za ofisi,ujasiriamali na tusaidie tuweze kuwa waaminifu katika kazi zetu.

Imarisha maisha ya ndoa kila mwanandoa achukue majukumu
yake ,imarisha mahusiano yote yawe ya kukupendeza na yalete matokea mazuri kwa watu wote.

Tunawaombea watoto wetu na wajukuu wetu wa kike na kiume wafaulu mitihani yao matokeo yao yawe mazuri, wapate ajira,wapate vyuo waimarishe imani zao Baba watoto hawa ni zawadi njema toka kwako Baba tunakushukuru sana kwa zawadi hii njema, endelea kuwaimarisha afya zao miili na roho zao zikuzalie matunda mema.

Wabariki wasafiri wote waende na kurudi salama majini ,nchi kavu,angani ukawe dereva wa kila chombo kukawe salama.
Tunaibariki siku ya leo tunaomba yote katika jinanla Yesu Kristo Amen.

JUMANNE NJEMA YA BARAKA DAMU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom