Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kilichobaki ni .....View attachment 817376
IMG_20180724_125812.jpg
 
Hakuna jambo jema unalotakiwa kulifanya kama kushukuru, sio kwa mazuri hta kwa mabaya inabidi ushukuru maana yanakufundisha usisahau siku nyingine.

Asante Shunie kwa kutuamsha kwa sala, asante mtu chake kwa mapicha ya DRC, Tumosa kwa kuchangamsha wote na zaidi asante wewe ambaye upo hapa jukwaani.

Kuna jipya?
 
Tafasiri Unavyoweza: Mamlaka, Akili Tatu Si Moja

...kawaida kipengele hiki ni siasa na jamii kila siku, siasa ni maisha na kila siku tunafanya siasa iwe sebuleni au chumbani, hapa siasa binafsi inatumika na ukitoka nje ndo tunakutana na siasa za kitaifa. Siasa za kuamua nani apate nini kwa wakati gani. Siasa za kugawanya na kuhakikisha kila mmoja anachangia maendeleo ya taifa na kufaidika na maendeleo hayo. Siasa za kujinyima uhuru wako na kumpa mtu/kikundi cha watu mamlaka ya kukuongoza na si kukutawala na ikitokea ukaanza kuona dalili za kutawaliwa, jiongeze, jua ya kwamba unaibiwa. Tafasiri unavyoweza.

Baada ya uchaguzi, washindi huunda serikali na kwa mfumo wetu, mshindi halazimishwi kuchagua aliowashinda kwenye serikali yake. Tulikubaliana hili lakini haimzuii mshindi kuchagua wapinzani kwenye serikali ili kupata mawazo mapya, mawazo tofauti kwani akili moja si sawa na akili tatu. Kuna nguvu katika utatu.

Kwa sasa tunashuhudia akili moja tu iliyo madarakani ikiamua yote, akili ya mimi mimi na mimi pekee ndo ninaweza na anayenipinga hataki maendeleo ni adui wa taifa. Umimi haujawahi kuwa na maslahi ya wengi hata siku moja, kisiasa namaanisha umimi huwa ni mbinu nzuri ya kuwaibia wananchi na kujinufaisha kibinafsi. Utashangaa kiongozi anaingia madarakani fukara akitoka ana utajiri wa kufa mtu.

Mamlaka ni nguvu unayoipata toka kwa wananchi, sio wanachama pekee. Mamlaka yamegawanyika katika sehemu tatu ambazo kiobngozi makini anapaswa azitambue. Mamlaka ni uwezo wa kushawishi wengine na wewe mwenye mamlaka kupata/kufikia lengo ulilonalo. Sasa unawezaje kuwashawishi wananchi/raia na wasio raia kushirikiana nawe katika kufikia malengo yako kama kiongozi.
Kwanza, kwa sababu ya mamlaka uliyonayo unaweza kutumia vitisho (threats) katika kufikia malengo yako. Njia hii ni dalili a kumuonesha kiongozi kama mtu mbinafsi na mwenye malengo ya kukaa madarakani na kchuma jasho la wengi kwa manufaa binafsi.
Pili, mamlaka imeaminiwa na imekabidhiwa vyungu vya fedha na hivyo mamalaka kibinafsi kabisa inajielekeza katika kuwapa wananchi fedha ili ionekane inapendwa bila kufanya chochote. Hapa hutaona shule zikijengwa, hutoona hospitali zikijengwa ila utamuona kiongozi kwenye TV akigawa hela kwa mgonjwa mmoja akatibiwe nje. Tafasiri unavyoweza.

Na tatu, mamlaka ya kuvutia wote, kushirikiana na wote katika kuhakikisha mandeleo ya taifa ni maendeleo ya wote na si kikundi cha watu wachache. Uongozi akili tatu, bahati mbaya naona akili moja tu. Tafasiri unavyoweza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom