Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Wanatuonesha Matumbo, Tunaangalia Akili Hatuzioni
.....viongozi wanang'aa, ngozi imepakwa mafuta mazito na nywele wamezitengeneza vizuri, kifupi wamenawiri na wakija kutuhutubia hotuba zao zinazibwa na matumbo yao makubwa kiasi kwamba wanachoongea akili huioni. Ni rahisi kuona matumbo yao kuliko kuelewa wanachoongea. Matumbo yao yako mbele, yametuna kututua vifungo, wanaongea wanatema mate sababu mashavu yamenona mate hayana pa kukaa. Wanatuambia kuna faida imetengenezwa na makampuni ya umma, mabilioni ya gawio serikali imepata mwaka huu kama mwaka jana na faida wengi hatuioni hadi tuangalie matumbo ya viongozi. Tafasiri unavyoweza.

Ni rahisi kumtambua mtu anayekudanganya, mwangalie tumboni. Ukimwangalia machoni atazidi kukudanganya utaona anakuambia ukweli maana ana uzoefu wa kudanganya na zaidi kila wakati anapanga namna bora ya kukudanganya na kuingia mikataba kwa jina lako, mikataba ambayo wewe mhusika hutoweza kuiona ukianza kulipa madeni na faida utaiona kwenye tumbo la kiongozi aliyesaini kwa niaba yako. Anakuambia ili usihoji, nyuma kazungungwa na askari wenye silaha kumlenga kila atakayenyoosha mkono kutaka ufafanuzi maana askari wanakula makombo. Tafasiri unavyoweza

Kwa rasilimali tulizonazo, watu na ardhi, Tanzania yetu haihitaji hisani (charity) katika kuboresha maisha ya wananchi, inahitaji viongozi na mfumo mzuri wa kufuatilia na kuiwajibisha serikali. Waandishi wa kitabu Why Nations Fail, sio kitabu cha kubuni bali utafiti wanaungana na nguli Dambisa Moyo kueleza kuwa faida ya misaada na magawio tunayoisoma magazetini kila siku haionekani kwa sababu ya wachache kujineemesha wenyewe (ufisadi) na kuzidi kuwajaza ujinga wananchi ili wasihoji. Tafasiri unavyoweza.

Tumesoma serikali ya Korea itajenga daraja DSM, hizi ni habari njema kama utajua kilichomo ndani ya mkataba, tatizo kubwa tulilo nalo sisi ni kutokuwepo kwa mfumo unaojumisha washika dau wote katika masuala ya maendeleo, inataka kuonekana ni nguvu ya watu wachache ndo wajinasibishe kuleta maendeleo kwa kutuaskinisha wengi. Wanatutenga kwenye kujua yaliyomo ndani ya mkataba, wanakula cha juu na kwenye kulipa wanatukamua hadi utumbo mwembamba. Ipo siku tutaamka wengi na tutayafungua matumbo ya watawala kuangalia kama tumboni kuna akili. Tafasiri unavyoweza
 
Asante binamu
 
binamu nimecheka kwa sauti eti umekonda wewe wa kutokula wewe

...ha hahaha, jameni, yaani huamini! Sikuwa nakula kabisa ugali, nilikuwa mwendo wa vitumbua, mchana biriani na usiku wali. Ugali sikuwa nakula kuonesha masikitiko kwanini wamekuban.

Kwanini lakini walikuban, kama utapenda kushare , na kama hupendi basi sitojali
 
Binamu jamani vitumbua gani hivyo tulikuwa mmu uko ndio ban ilipotupatia hakuna kosa la ajabu mods waliamua tu
...ha hahaha, jameni, yaani huamini! Sikuwa nakula kabisa ugali, nilikuwa mwendo wa vitumbua, mchana biriani na usiku wali. Ugali sikuwa nakula kuonesha masikitiko kwanini wamekuban.

Kwanini lakini walikuban, kama utapenda kushare , na kama hupendi basi sitojali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom