Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Tukubaliane Tatizo, Tukubaliane Tatuzi

....kuna mengi yanendelea katika uga wa siasa na utawala hapa kwetu, mengi sana na mengiyayo yanafurahisha na kuonesha dalili za kutugawa. Chukulia suala la ajali kwa mfano, ajali za barabarani zipo na wanasema hajali haina kinga ila unaweza kupunguza ajali hizi kwa kuwa na miundombinu mizuri na wala si kwa kukusanyana, kufunga barabara na kufanya matambiko, hizi ni mbinu za kijima. Tafasiri unavyoweza.

siasa zetu zinaelekea kutupeleka kwenye njia inayochanganya sana, njia ambayo waziri anaona ilani ya chama ni muhimu kuliko katiba ya nchi, njia ambayo wengi wanaona tatizo na wachache wenye madaraka hawaoni kuwepo kwa tatizo. Tuna ombwe la uongozi, ndiyo, uongozi safi unaotanguliza maslahi mapana ya taifa na si maslahi mapana ya wachache kichama au kiitikadi fulani. Uongozi unaoamini katika kupiga mateke, kujitoa katika kulinda usalama wa raia na kujiona unafaaa zaidi kutumikiwa kuliko kutumikia wananchi. Tafasiri unavyoweza.

Inapofikia wakati tunashindwa kukubaliana kuhusu kuwepo kwa tatizo fulani basi kama jamii lazima wachache wasimame watuambie kuwa kuna mahali tumekosea hatujui tunaitakia nini jamii yetu. Watu makini huweza, na hakuna ubaya katika kutokubaliana kuhusu namna ya kutatua tatizo lililo mbele yetu, kila mmoja anapendekeza mbinu yake ya kutatua tatizo lakini pale tunashindwa kukubaliana kuhusu kuwepo kwa tatizo basi hapo hatuhitaji mtaalamu wa magonjwa ya akili atuambie kuwa tunaumwa kichaa. Nikutakie wiki njema na yenye mafanikio, kipe kichwa chako kazi, kisiishie kubebwa na mabega tu. Tafasiri unavyoweza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom