Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Ujinga Si Kutojua K Tatu Pekee

Ninapenda kuandika kuhusu masuala ya elimu, ninapenda harakati za elimu, inaweza kuwa ni kwa sababu nilishika chaki kidogo. Ninaamini elimu sio tu ufunguo wa maisha bali jamii kubwa iliyoelimika ina nafasi kubwa ya kuendelea kuliko jamii ambayo haina watu walioelemika. Aliyeelimika, tunamuita msomi, anajipa nafasi ya kufikiri kabla ya kuchukua maamuzi yoyote, anahoji jamii anayoiishi na zaidi mwenye kuelemika anapenda ukweli. wengi wa walioelimika hawajidhalilishi kwa kusemasema uongo na ufisadi. Tafasiri unavyoweza.

Ujinga kwa maana iliyozoeleka kwa wengi ni ile hali ya kutojua kusoma na kuandika. Na sisi watanzania tukaongeza na kuhesabu (3 K), tukawa na kusoma, kuandika na kuhesabu. Kwa kweli awamu zote zilijitahidi kuondoa na kufuta ujinga miongoni mwa jamii pana, sasa suala la kujua kusoma, kuandika , kuhesabu si tatizo la kusema sana maana tunaandikisha watoto wengi shuleni kuelemishwa.

Pamoja na jitihada hizi bado kuna changamoto ambayo inamfanya mwenye elimu kuwa mjinga, hii ni ile hali ambayo mtu anayejua kusoma, kuandika na kuehsabu anaposhindwa kuchakata kile anachokisoma na kukielewa (comprehending the meaning). Huyu anashindwa kufanya maamuzi sahihi ya kile alichosoma na hana tofauti na kasuku, anakariri maneno bila kuyachakata ayape maana na kuyaelewa ili aweze kuchukua maamuzi sahihi.

Na kwa tatizo hili la kuwa mjinga kwa kujua kusoma na kuandika ila usiweze kuyapa maana uliyosoma na kuandika (functional illiteracy) mtu unakosa sifa za kuajiriwa, wanasiasa wanakutumia wanavyotaka kwa kukulisha uongo mwingi, wanakutengenezea tatizo na wanaliongelea na wanajidai kulitatu na wewe unawaona wanafanya kazi stahili. Huna uwezo wa kuhoji. Bado tuna wajinga wengi na bahati mabya sana ndo wanaokaa mbele na kuwaziba wachache wanaotaka kuwasaidia. Tafasiri unavyoweza
Mkuu aksante kwa kifungu hiki natamani uendelee aise!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom