Tafasiri Unavyoweza: Wakumbuke Wabaya na Wazuri
Ni Ijumaa leo kama ulikuwa umesahau, na ninapokukumbusha sio kwamba najaribu kujaza aya kwa maneno yasiyohusika. Utaelewaje ninachoandika kama tu kwa kuanzia hujui leo ni lini. Tafasiri Unavyoweza.
Ni jambo zuri kuwa na kumbukumbu, ndiyo, tunaweka kumbukumbu ya Watu, vitu na masuala ya kibinafsi au familia. Kama taifa tunaweka kumbukumbu na kuzisheherekea baadhi. Lakini, mara nyingi sana tunasheherekea zile kumbukumbu nzuri tu na kuzisahau zile mbaya. Hatukumbuki mabaya labda kwa kuwa yanaleta majonzi moyoni. Kama tunaweza kukumbuka mazuri yaliyofanywa na watu kitaifa na tunaenda mbali zaidi kwa kuandaa makongamano inakuwa shida wapi tukiandaa kumbukizi kwa watu tuliowapa jina baya kwa ''mabaya" tunayodhani walifanya. BTW, ubaya au uzuri wa mtu ni tafasiri ya mtu na mtu.
Tafasiri unavyoweza, hapa tujitafakarishe kuwa jamii yetu inapaswa kuwakumbuka wote tunaodhani wamefanya mazuri na tuwakumbuke wote tunaodhani walifanya mabaya. Tuwape heshima.