Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Utengano ni Udhaifu

...umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Na kwa tafasiri sisisi ya kiingereza tulisema, unity is strength, disunity is weakness, hizi zilikuwa zile enzi za kundi la umri wangu ambalo shule za chekechea (kindergarten) ziliitwa vidudu na ni shule za masister tu ndo walikunywa uji, wengine saa nne mnarudi nyumbani na wenzenu wanaingia, tuliwaita wa saa nne makombo. Nimekumbuka kitu, tafasiri unavyoweza.

Inataka kuonekana sasa kuwa kama ni kawaida, mazoea. Vipo viashiria vingi tu ambavyo vinaonesha kuwa tunaanza kujitenga kisa tu tunatofautiana kiitikadi za vyama vya siasa na kiimani. Hii si afya ya taifa na jamii inayotaka kuendelea. Kumbuka tu kuwa jamii inayokinzani ndiyo huwa na uwezo wa kuendelea. Hatuwezi kuwaza mamoja, hata mapenzi hayako namna hii, itakuwa nchi na watu wake!!!!. Tafasiri unavyoweza.

Tunapotofautiana kimtizamo kama taifa maana yake nini? unaweza kutafasiri unavyoweza, hili halina ubishi. Tunajenga nyumba moja hatuwezi kugombania kunyang'anyana fito. Nchi hii ni yetu sote na kama ni yetu sote kwanini ionekana sasa kuwa ukipingana na uutawala uliopo wewe si mzalendo!? Huu hautakuwa utawala wa kwanza kuwa na upinzani na hautakuwa wa mwisho, upinzani umekuwepo tangu enzi za chama kimoja, soma pata taarifa sahihi. Upe ubongo wako kazi.

Tafasiri unavyoweza, nataka tu nikukumbushe kuwa UNFPA wanasema mwaka 2038 tutakuwa Watanzania milioni 90, wenzetu wanaona mbali na kupanga namna ya kusaidia ongezeko hili la idadi ya watu, sisi bado tuangombana na itikadi za vyama na kutaka kujitanabaisha chama hiki ni bora zaidi ya hiki. Nchi huru hii, tafasiri unavyoweza, umoja ni nguvu utengano hauwezi kukufanya uwe na nguvu hata siku moja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom