Tafasiri Unavyoweza: Nguvu Unayo, Itumie
Ankal wangu ana usemi wake ambao napenda niutumie leo kwenye kipengele hiki cha kutafasiri unavyoweza. Usemi wenyewe ndo huo kwenye kichwa cha habari (title). Kila mwenye uwezo, ana nguvu. Hapa nieleweke kabisa nguvu nazoziongelea hapa ni zaidi ya nguvu za mwili. Nimesema haya ili kuiweka sawa tafasiri ya nguvu uliyonayo ninayoingelea hapa, sio utafasiri kwa kuweka nguvu za kike au za kiume, kichwa cha nyoka hakibebi mzigo.
Naongelea nguvu uliyonayo ambayo unayo inayoweza kushawishi, kubadili masuala yanayokuzunguka na kubadili tabia (social power). Nguvu hii ninayoiongelea hapa huzaliwi nayo, unaipata kupitia kuwa na utambuzi sahihi (well informed), na ukiikosa nguvu hii basi ni bila shaka utajikuta unapelekwapelekwa bila kujua unakopelekwa ndiko au siko unakotaka kwenda. Mtu mwenye taarifa ana nguvu, kubali au kataa, hawezi kunyanyaswa kijinga, anajua haki zake na wajibu wake kwa jamii. akienda kupiga kura anaiambia kura yake ifanye nini anachokitaka na wala haongozwi na mapenzi yakishabiki.
Tafasiri unavyoweza, social power unaihitaji sana kama unavyohitaji nguvu nyingine za mwili. Ukikosa nguvu ya ushawishi basi tambua kuwa kitakachoumia ni nguvu zako za mwili. Tafuta maarifa uweze kuzifanya nguvu za mwili ziwe na maana kwenye jamii. Tafasiri unavyoweza