Tafasiri Unavyoweza: Maktaba Si Vitabu na Utulivu Pekee
.....library offers more services, they are more than just books. Nimeanza na kiinglishi kuonesha mazingira tuliyozoea kuitafasiri maktaba. Tafasiri unavyoweza. Tumekuwa na mazoea ya kuhusisha maktaba na elimu, well, kuna ukweli katika hili. Maisha yetu tunayoishi yamejaa kila aina ya 'machafuko' na changamoto (chaos and challenges) ambazo inabidi tuzitatue. Na ujue kabisa si kila changamoto unayokutana nayo maishani utategemea mwingine akutatulie, nyingi unatatua mwenyewe.
Tafasiri unavyoweza, utulivu unaokutana nao maktaba una maana moja kubwa, watu wanatulia kufikiri. Kelele unazokutana nazo maktaba zina maana kubwa, watu wanatoa mawazo yao kupitia ushairi, sinema, ghani na ngano. Umestuka eeh, kuona nimeongeza kelele maktaba!! Eeh, maktaba sahihi ina sehemu maalum kwa wewe kwenda na kupiga 'makelele'. Na hapo ndo hoja yangu ya kutafasiri ninavyoweza inakuja. Maktaba ni zaidi ya vitabu.
Changamoto na machafuko tunayokutana nayo ni darasa tosha la kuturudisha maktaba kujua wengine walikabiliana nayo vipi. Kumbuka wewe si wa kwanza kwenye kila tatizo au changamoto. wewe si wa kwanza na hautokuwa wa mwisho hivyo jitahidi kutumia muda kidogo kutembelea maktaba ujifunze mengi. Na kama huwezi kutembelea basi unaweza kusaidia maktaba iliyo karibu nawe kwa kuchangia muda na rasilimali. Tafasiri unavoweza, nchi huru hii.