Tafasiri Unavyoweza: Mkataba
Tunaingia kwenye makubaliano tofauti na ya kila namna mara nyingi na kila wakati. Iwe ni makubaliano yanayohusiana na makazi, mahusiano, ajira, kilimo, biashara, matumizi ya mtandao, mawasiliano na taja makubaliano yoyote ambayo umewahi kuingia au unapanga kuingia. Makubaliano haya ama unaingia na mtu mmoja au kundi (entity) kiufupi yanaitwa mkataba. Serikali yetu huingia mkataba na serikali nyingine, watu binafsi, makampuni na usisahau wananchi tunaiweka serikali madarakani kwa mkataba.
Tafasiri unavyoweza, mkataba waweza kuwa wa mdomo au maandishi. Mkataba ni makubaliano ya pande mbili au zaidi (reciprocal or mutual agreement) kukubaliana au kutokubaliana kufanya jambo mahsusi. Mkataba mzuri ni wa maandishi, huu huleta uwajibikaji na rejea ya yale mliyokubaliana, mnaweza kukaa na kufanya mabadiliko juu ya mlichokubaliana au kukataliana.
kwa kuwa mkataba ni makubaliano au kutokubaliana juu ya kitu, ukikiuka mkataba basi tegemea kulipishwa au kulipa fidia, uharibifu, usumbufu, kufilisiwa, na adhabu nyingine zinazoendana na mkataba.
Tafasiri unavyoweza, makubalianao sahihi huja kwa sababu una taarifa sahihi, hautishwi, hujachochewa, hujahemka na una akili timamu. Usiingie mkataba kama huna hayo niliyosema vinginevyo unaweza kujikuta matatizoni. Kura yako kwa chama unachokipa madaraka ni kukubaliana na sera zake, kisipotimiza mlichokubaliana basi kuna sababu gani ya kukirudisha madarakani wakati mwingine! Tafasiri unavyoweza